Saturday, December 2, 2023

KICHAA MPELELEZI 41 $ 42

 



SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 41&42


Doctor Shedy alikunywa pombe nyingi🍾kupita kiasi na kulewa chakari mithili ya mlevi wa mataputapu, nikiwa sina hili wala lile mara ghafla😨 Doctor Shedy akaanza kuropoka mbele ya Mr Michael na wanajeshi wengine, "Watanzania hasa wapare na wachaga wanapenda hela sana 😀 yani mtu yuko radhi akane damu yake ili apate mabilioni ya pesa, hcho ndicho alichokifanya Brighton ila kawaida ya sisi walevi ni wasema kweli acha tu ukweli usemwe, vipimo vya DNA vya mtoto wa Cara vinaonyesha baba wa mtoto ni Mr. Brighton" aliropoka Doctor Sheddy na kumfanya mr. Michael apigwe na butwaa na kutoa macho😳 kama mtu aliyepokea habari mbaya za kuogofya, "Mbona wewe doctor hueleweki, sasa kama mtoto ni wa Brighton kwanini ukanibambikizia mimi ee" aliuliza Michael huku akiwa amekunja uso wake 😩kwa hasira. "Wewe nawe kwahiyo kukuambia ukweli mapema ni kosa, au ulitaka ulee mtoto wa kidume mwenzio kisha huko baadae ushagharamika ndio uje kuujua ukweli😜?" Doctor Sheddy alimuuliza Mr. Michael kwa sauti ya kilevi wakati huo nilikuwa nimeduwaa sana🫢baada ya doctor Sheddy kuvujisha siri. Haraka Mr. Michael akamkunja tai Doctor Sheddy, "Sema ukweli kwanini uliamua kunidanganya, na ole wako usiseme ukweli nakwambia hizo pombe zitakuisha leo☹️" aliongea Mr Michael huku akiwa amemkaba Doctor Sheddy shingo yake kwa kumshika tai. "Niachie basi niseme" Doctor Sheddy alijitetea "Haya sema" Mr Michael alimwambia kwa kumkoromea. "Ukweli ni kwamba Mr. Brighton ndiye aliyeniambia kwamba ikitokea vipimo vya DNA vikaonyesha mtoto ni wake basi nisimtaje yeye bali nikutaje wewe kwasababu kama nitamtaja yeye kuna uwezekano wa yeye kukosa hela alizoahidiwa kulipwa kwa kigezo kwamba atahisiwa kwamba kuna njama anazopanga dhidi ya jeshi na pia ataonekana anashirikiana na majambazi mpaka akafikia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Clara hivyo aliniomba nimfichie siri na pia akaniahidi akilipwa atanikatia fungu kidogo kwa kazi niliyoifanya ya kumfichia siri." Doctor Sheddy alitoboa siri wakati huo mkuu wa vikosi vya jeshi na wanajeshi wengine walikuwa wakisikiliza kwa umakini �sana.


"Lione vile yani kama lizwazwa hapo tayari limeshaunguza picha yani tena halijalewa hili huenda limefanya makusudi maana kawaida ya wabongo hatupendani, wivu na chuki ndio vinatusumbua hapo limeona nimewekewa mabilioni ya pesa kwenye akaunti yangu likajisikia wivu " Niliongea kimoyomoyo huku nikimtazama Doctor Sheddy kwa hasira sana🥺 na machozi yakinilengalenga. Mkuu wa vikosi vya jeshi akamnyamazisha Dr. Sheddy pamoja na Mr. Michael na wanajeshi wengine ambao walikuwa wakiendeleza minong'ono. Baada ya wote kukaa kimya mkuu wa jeshi akaanza kuongea "Nchi yetu inapinga vikali sana kitendo cha mtu kutoa rushwa ili apate cheo au kitu fulani anachokihitaji, kwa hili ni dhahiri kabisa kwamba Mr. Brighton atakuwa anashirikiana na Clara kwa namna moja au nyingine, na huenda kuna mpango anausuka ndio maana akawa anajipendekeza kwetu, kwa maana hiyo aswekwe mahahusu mara moja ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake😨" alisema mkuu wa vikosi vya jeshi na kuwaamuru wanajeshi wawili wanikamate na kuniweka ndani ya gari nipelekwe mahabusu. Pale nikaona sasa nisipojitetea kufa na kupona nitaswekwa gerezani hivi hivi naona, na kwa jinsi wazungu wasivyotupenda sisi waafrica naweza kupewa hata kesi ya uhaini kwenye taifa la watu na nisiwekewe dhamana, basi wakati wale wanajeshi wananifuata ili wanikamate, nilinyanyuka mara moja nilopoketi na kuanza kukimbia🏃🏿‍♂️ walianza kunikimbiza huku wakiniftatulia risasi, nilikimbia kwa kupindapinda nikizikwepa zile risasi zisinipate😁, nilipotoka tu nje ya kambi ya Jeshi kuna jaamaa alikuwa anataka kupaki pikipiki yake nje ya duka moja, kabla hajaizima nilimpiga kikumbo akadondoka pembeni, nikamnyang'anya pikipiki🏍️ na kuanza kukimbia nayo , nilivuta mafuta nikiwa kwenye mwendo mkali sana maana nyuma yangu nilikuwa nakimbizwa na gari dogo la kijeshi, hapo nikajiongeza kupita njia za vichochoro ambapo lile gari la kijeshi 🚔 haliwezi kupita, hapo nikakatiza vichororo kadhaaa na kuwaacha kwenye mataa😀 Nilikimbia na kutoka kabisa maeneo ya makazi ya watu na kwenda kujificha maeneo ya porini chini ya daraja kubwa sana, niliwasha simu yangu  haraka, na kumpigia mdogo wangu ambaye yupo Tanzania kwa whatsap call, nikafanya utaratibu wa kuhamisha zile bilioni sabini kutoka kwenye account yangu kwenda kwenye account yake ya benki. 


Niliendelea kukagua simu yangu mara nikautana😳 na picha zangu kwenye vyanzo vya habari vya marekani wakiwa wamenipost kila kona wakiambatanisha kichwa cha habari kilichosomeka "JAMBAZI MWENYE ASILI YA KITANZANIA ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSHIRIKIANA NA MAJAMBAZI WENGINE KWA KOSA LA KUVUNJA MABENKI NA KUSABABISHA MAAFA YA MAMIA YA WATU, yoyote atakaefanikisha kupatiana kwake atapatiwa donge nono kama zawaidi. " nilisoma taarifa hizo huku moyo ukinidunda balaa😳 "Mungu wangu tayari nishabambikiziwa kesi ya mauwaji, hivi wakinipata si nimekwisha mimi🤔" niliwaza, basi usiku uleule nilienda benki za marekani kwasababu zilikuwa zinafanya kazi masaa 24 nikatoa kama milioni saba ambazo nilibakiza kwenye account yangu, baada ya kutoa haraka nikaondoka bila kupoteza muda maana kuna watu walianza kunitizama usoni nahisi walianza kunifananisha na picha zangu zilizopostiwa, baada ya kuondoka pale nikaenda kwenye duka la nguo nikanunua baibui na nikabu ya kuficha uso, nikaenda hotelini na kuchukua chumba , kwenye daflari la kujiandikisha wageni nikaandia jina tofauti lakini la kiume, ila nilipoingia chumbani nikabadilisha mavazi haraka na kuvaa yale ya baibui na nikabu, wakati nipo ndani ya chumba changu mara nikasikia nje polisi wakiongea na muhudumu wa vyumba " Sisi ni jeshi la polisi samahani hapa hotelini kwako una CCTV camera" polisi aliuliza . "hapana ilishaharibika" alijibu  muhudumu. "Basi sawa kuna muhalifu tunamtafuta kama kungekuwa na CCTV camera ingekuwa rahisi kumpata ila kwasababu hamna waamshe wateja wako wote tufanye ukaguzi chumba hadi chumba" alisema polisi. Macho yalinitoka😳moyoni nikasema sasa kimenuka..   .


JE ITAKUWAJE SASA ? BRIGHTON ATAKAMATWA AU? Hakika mambo ni moto si kitoto🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥😁 hakikisha unalike na kucoment ili nije chaaaap


PLEASE VISIT AGAIN OUR BLOG KWAAJILI YA KUPATA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

KARIBU TENA MGENI



Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text