Saturday, December 2, 2023

YATIMA GEREZANI 7

 



YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 7.


Maisha yalizidi kusogea hatimaye miezi Tisa ya ujauzito wa Mama yako ilifika na hapo ndipo hiii Siri ninayo kwambia leo inaanzia, ilikuwa ni jumapili Siku hiyo Baba yako alikuwa yupo mikoani kusambaza mbolea, ikiwa ni mida ya saa moja za Jioni Mama yako alipatwa na uchungu.

Mimi nikiwa getini huku nilisikia kelele za vilio ndani, hapo ilibidi niende nilipo ingia ndani kufika sebuleni nilikuta Mama yako akiwa yupo kwenye uchungu na anataka kujifungua, Zena alikuwa yupo pembeni akiwa anamsaidia Mama yako.

Nilimshauri Zena kama vipi tumkimbize Mama yako hospital, lakini Zena alinihakikishia kwamba atajifungua Salama kwa sababu maswala ya ukunga yeye kapitia.


Ni kweli Mimi nilitoka nje, kusubiri kinacho endelea, yalipita masaa kama mawili, nikiwa getini nilimuona Zena akiwa bize na Simu na alitoka mpaka nje na kwenda kwenye bustani kuongea na Simu ile.

Mimi nikiwa na wasiwasi mkubwa ilibidi niingie ndani kwanza kwenda kuona hali ilivyo, niliingia ndani bahati nzuri nilikuta Mama yako kajifungua salama kabisa na Mama yako alikuwa yupo chumbani.

Basi Mimi kujihakikishia nilifika mpaka kwenye mlango wa chumba Cha Mama yako nilichungulia, niliona Mama yako kakaa kitandani huku akionekana yupo sawa na Mtoto wake alikuwa kalala pembeni.

Baada ya kuona Mama yako yupo sawa na kajifungua salama kiukweli nilifurahi, basi ilibidi nitoke kimya kimya bila kumbuguzi na nilirudi tena getini huku nikiwa na furaha, na muda wote huo bado Zena alikuwa anaongea na Simu pale kwenye bustani, na bahati nzuri au mbaya alikuwa hajaniona Mimi kama nimeingia ndani ama laa!!.


Basi zilipita dakika kama kumi Zena nilimuona akiingia ndani, ila nikiwa pale getini dakika kumi tu kupita baada ya zena kuacha kuwasiliana na Simu, Bwana Dosomi akiwa na Farhan walifika na Gari.

Japo kuwa Dosomi nilikuwa na wasiwasi naye toka muda mrefu ila sikuona kama kuna haja ya kumzuia kuingia, kwa sababu aliniambia ni dharura, na Mimi nilikuwa nishajua dharura ni mke wa boss kujifungua.


Ikiwa ni mida ya saa nne za usiku Dosomi na Farhan waliingia Ndani, Mimi nikiwa nipo getini.

Zilipita dakika kama ishirini tu nilisikia vilio ndani, na niligundua ni sauti ya Zena, basi haraka haraka ilibidi nikimbilie eneo la tukio nikiwa naamini akina Dosomi watakuwa wanamdhuru.


"Rafiki yangu Mimi jamani, rafiki yangu jamani nafanyaje Mimi!!nani atalea Mtoto jamani!" Baada ya Mimi kuingia ndani hayo ni maneno ambayo yalikuwa yameambataba na kilio kizito ambayo Zena alikuwa anayatoa.

Kwanza ilibidi nipigwe na mshangao, niliuliza nini tatizo, majibu niliyo pewa ndo yalifanya nichoke zaidi.

Niliambiwa kwamba Mke wa boss kafariki wakati anajifungua na kaacha Mtoto mchanga.


Hakika niliishiwa nguvu na kukaa chini yaani akili ni kama iliniruka, ila nilipo mwangalia bwana Dosomi niligundua shati lake lina madoa ya damu, mpaka hapo niligundua mke wa boss atakuwa kauawa na siyo kufariki, na kingine Mimi mwenyewe kwa macho Yangu nilikuwa nimemuona amejifungua Salama na ni mzima kabisa, ila nilishangaa muno kuambiwa kwamba kafariki wakati akijifungua.

Basi usiku ule ule Zena kushirikiana na kina Dosomi walichukua mtoto mchanga ambaye ndo ulikuwa wewe na walichukua mwili wa Mama yako na kuelekea hospital kwenda kuhifadhi.


Wakiwa wamebeba mwili wa Mama yako, niliona Dosomi akiwa na bastola kiunoni, hapo ndipo uoga wangu wa kutunza Siri ulipo anzia.

Basi Siku hiyo ilipita kwa ugumu muno na hapa Nyumbani niliona pazito muno, nilikumbuka na ukarimu wa marehemu basi nilijikuta chozi tu linatiririka.


Ikiwa ni Siku mpya, Baba yako alirudi toka mikoani baada ya kupewa taarifa na kina Dosomi.

Basi Mimi baada ya kuonana na Baba yako nilijaribu kumgusia kwamba akina Dosomi huwenda kuna namna wamefanya kuhusu mkewe, ila Baba yako alikuwa mbishi kutokana na Namna alivyo kuwa anawaamini.


Baba yako alikuwa na rafiki yake wa kike ambaye walikuwa wanatoka kijiji kimoja yaani alikuwa anamchukulia kama ndugu hivi ambaye alikuwa anaitwa Pili, basi Mimi ilibidi nimwelezee yule Dada hali halisi niliyo ishuhudia, lakini kitu alicho nambia alisema nikae kimya kwa sababu nikianza kujifanya shahidi naweza bebeshwa ile kesi kwa sababu Dosomi alikuwa anajuana na Maaskari karibia wote.

Basi zilipita Siku mbili Mazishi ya Mama yako yalifanyika,ila Pili uvumilivu ulimshinda, kitu alicho fanya aliamua kumfuata Zena na kumchana makavu laivu Kwamba yeye ndo kahusika na kila kitu, na alimtishia kwamba asipo sema ukweli, basi ataenda kutangaza kila mtu ajue.


Mazungumzo kati ya Pili na Zena Mimi niliyasikia vizuri kwa sababu walikuwa wanaongelea hapo nje ya geti.

Baada ya yale mazungumzo hayakupita masaa hata ishirini taarifa za Pili kuvamiwa na majambazi na kuuawa zilitufikia, mpaka hapo uoga ndo ulizidi kunijaa zaidi, nilijikuta nabaki na Siri Yangu moyoni.

Maisha yalizidi kusogea, huku Mtoto mchanga ambaye ndo wewe akiwa analelewa na Zena hapa Nyumbani, basi baada ya miezi kama sita hivi, akina Dosomi na rafiki wengine wa Baba yako walimshawishi Baba yako amuoe Dosomi ili wasaidiane kumlea mtoto kama Baba na Mama.

Ni kweli hata mwezi haukupita ndoa ilifungwa bomani, japo kuwa ilikuwa dini mbili tofauti ila ndoa ilipita na wawili hao rasmi walikuwa mume na mke.


Hapo maisha mapya yalianza kwa familia nzima, kwanza Mimi niliacha kuchukuliwa kama mwanafamilia tena, yaani hata Ndani sikuruhusiwa kuingia tena kama mwanzo na zote zilikuwa sheria za Zena.

Siku zilizidi kusogea huku Sasa wewe ukiwa kama mtoto wa Zena na kila mtu alianza kuamini Kwamba ni mtoto wa Zena kutokana na Zena alivyo kuwa anakulea na kukujali.


Pamoja na Zena kuolewa na Baba yako ila hakuacha kutoka usiku, Siku zingine nilikuwa namuona Farhan anakuja mpaka hapo getini na bajaji baada ya hapo Zena anatoka.

Nilijaribu kumgusia Baba yako ile hali ila Baba yako alikuwa mbishi, na Baba yako alikuwa ni mtu wa kusafiri muno, kwa hiyo kipindi hicho Zena alikuwa anakitumia vizuri Sana.


Baada ya miaka kama miwili na kitu kupita, Zena alipta ujauzito ambao kila mtu aliamini ni wa baba yako.

Ila kuna Siku Zena aliletwa hapa na gari na Mimi nikiwa humu Ndani nilisikia muungurumo wa gari nje japo kuwa halikupiga honi, hapo ilibidi nifungue mlango mdogo na kuchungulia, kwa masikio Yangu niliskia Farhan na Zena wanabishana kuhusu ujauzito!! Zena alikuwa anasema ujauzito ule akabidhiwe Mr Fekon, ila Farhan alionekana kuwa na wasiwasi na alikuwa anamtaka Mama yako adai taraka wagawane baadhi ya Mali ili wao waende kuishi pamoja kulea ujauzito wao, ila Mama yako alimgomea Farhan na alisema ana mipango mizito zaidi kuhusu Mali za Mr Fekon.


Kuanzia Siku hiyo niligundua Zena pamoja na kuwa mke wa Baba yako ila hana Lengo zuri, kuna muda niliogopa kumwambia Baba yako kutokana na Jinsi alivyo kuwa anampenda Zena, na inaonekana Baba yako alikuwa karishwa tayari limbwata maana alikuwa haelewi kitu kumhusu Zena.


Maisha yalizidi kuendelea huku tabia za Zena zikiwa ni zile zile, mwishowe alijifungua mtoto ambaye ndo Samir.

Pamoja na Baba yako kutaka mtoto wake aitwe Moses, lakini Zena alikataa na kusema mwanae hawezi kuitwa Jina la kikristo, hapo ndipo alipo muita mwanae Samir.

Baba yako naye alikubali japo hakupendwa aitwe Baba Samir, maisha yaliendelea huku mukiwa munalelewa vyema, ila mipango ya Zena na kina Dosomi nilikuwa sielewi kabisa, maana kila Baba yako akisafiri Dosomi na watu wake walikuwa wanakuja hapa wanaongea na Mama yenu baada ya hapo wanaondoka.


Baada ya miaka kama sita kupita hivi, Baba yako ni kama aligundua kwamba Samir siyo mwanae wa damu, hapo ndipo upendeleo wa wazi ulianza kwa Mr Fekon, yaani alikuwa anakupenda wewe kupita kiasi kuliko Samir.

Hiyo hali ilikuwa haimfurahishi kabisa Zena, na alionekana Kabisa kuna mipango yupo nayo.


Maisha yaliendelea, Baba yako alikuwa anakoswa koswa kuuawa kwenye baadhi ya matukio japo hakugundua ni watu gani wanamfuatilia, alicho amini ni kwamba ni wafanya biashara wenzake.

Nilijaribu kumgusia Baba yako kwamba asiwaamini kina Dosomi kwani siyo watu wazuri, ila Baba yako alionekana kunipuuzia maneno yangu na Siku zingine alikuwa ananitishia kunifukuza kazi akiwa anaamini ninacho ongea ni upuuzi.


Mwisho wa Siku ndo kama kilicho kuja kutokea, Mimi nikiwa getini nililetewa taarifa tu kwamba boss kagongwa na Gari na kufariki.

Kwa hiyo, hii ndo Siri nipo nayo miaka mingi, wewe ni Kama mwanangu kwa sababu ulikuwa mtoto wa rafiki yangu ndo maana sitaki upatwe na majanga, na kwa saizi wewe huna cha kufanya kwa Sababu vyombo vyote vya haki na usalama bila kuwa na pesa utaonekana una hatia tu" Hiyo ilikuwa ni stori fupi ya olenashi ambayo alimsimulia Nomani ndani ya kibanda kile, kijana Nomani mwili mzima ulibaki umepigwa ganzi kwa stori ambayo alikuwa kapewa.

Yaani ni machozi tu ndo yalikuwa yanaonekana kwa kijana Nomani.


"Uncle Mimi naenda kuwachana ukweli siwezi kukubali, Mali za Mzee ziende hivi hivi naziona!" Nomani akiwa kama karukwa na akili alitoka ndani ya kile kibanda na kuelekea ndani, olenashi alijaribu kumkamata lakini Nomani alionekana kuwa mbishi huku akiwa na hasira haswa.

Nomani alizama ndani huku pua zikiwa zinapanda na kushuka, baada ya kuingia alikuta watu wametandaza vinywaji mezani wanaburudika.


Kwanza kila mtu aliye kuwepo mule ndani alishangaa kumuona Nomani.


"Dosomi mambo gani haya, wewe umesemaje!?" Mama Samir aliuliza kwa sauti kubwa huku akiwa na mshangao.


"Wauaji wakubwa nyie, kwa hiyo Mama unataka kuniua ili urithi Mali za baba na mwanao siyo, au unafikiri bado sijajua Siri zako!?" Nomani akiwa na hasira huku anapumuliana alianza kupayuka.

Basi kijan Nomani akiwa anapiga mikwara, Dosomi alimuonesha kijana wake ishara kwamba Nomani akamatwe, bahati nzuri ile ishara Nomani aliiona vyema.


Nomani baada ya kugundua anataka kukamatwa alichoropoka na kutoka nje kwa kasi, ila akiwa anakimbia Dosomi alichomoa bastola na kufyatua risasi, yaani ile risasi ilimkosa Nomani, ilipita kwenye sikio na kumchana kidogo sikio.


Nomani kwanza haja zote mbili zilimtoka, alipo toka nje alidondoka chini kabla hajafika hata getini, baada ya sekunde kama tatu Nomani akili ndo ilikaa vizuri na aligundua yupo mikononi mwa mtu kabebwa anarudishwa ndani.

Nomani akiwa anaona kifo kinamuita, alimng'ata kwa nguvu yule jamaa ambaye alikuwa kambeba, baada ya Nomani kuachiwa mbio alizo toka nazo pale zilikuwa siyo za Dunia hii.

Muda huo olenashi baada ya kusikia risasi ndani yeye alikuwa kwenye kibanda chake akiwa anazuga kama kalala yaani alikuwa anatetemeka haswa.


Nomani alipita pale getini kama mshare,  yaani alikuwa anaona kama sikio linawaka moto na kuna vitu vinalia ndani ya sikio, hakika Siku hiyo kimbembele kilimponza.

Basi baada ya dakika kama mbili Dosomi na vijana wake walitoka kwa ajili ya kwenda kumsaka Nomani popote anapo kimbilia, yaani walijiapiza kwamba Siku hiyo lazima wamalize kazi.




PLEASE VISIT AGAIN OUR BLOG KWAAJILI YA KUPATA SIMULIZI MPYA KILA SIKU

KARIBU TENA MGENI



Tukutane sehemu ya 8

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text