YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA ðŸ˜ðŸ˜
Mtunzi: Mwaki Ze Done
Sehemu ya 12.
Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona, na hapo ilibidi waanze kunyan'ganyana ile bastola na yule mkubwa, katika ile hali ya kunyan'ganyana Nomani alishika sehemu ambayo siyo, risasi ilifyatuka na kumpitia yule mkubwa kifuani, tena upande uliko moyo.
Askari magereza walio mleta Nomani pale ofisini kwa mkubwa wakiwa nje kwenye korido walisikia mlio was risasi Ndani, kwa akili yao ya kawaida walijua mkuu kamuua dogo, ila miili yao ilibaki ya moto na jasho kuwatoka baada ya kukuta mkubwa wao kalaza kichwa juu ya meza na damu zimejaa chini, huku Nomani akiwa pembeni anatetemeka.
Askari wale walipiga filimbi kuita Askari wengine, Ndani ya dakika mbili Askari walijazana Ndani ya ofisi ile na Nomani aliwekwa chini ya ulinzi, kwanza Siku hiyo Nomani alipigwa kipigo mpaka alizimia.
Taarifa zilisambaa gereza zima kwamba dogo kaua mkuu wa gereza, yaani wafungwa wote hiyo taarifa waliipata, muda huo Nomani alikuwa kafungiwa kwenye chumba Cha pekee yake akiwa kazimia.
Nomani alikuja kuzinduka ushakuwa usiku mnene, na alikuwa yupo kwenye kachumba ka pekee yake huku kukiwa na baridi ya kutosha.
Palikucha mpaka asubuhi, Siku nzima Nomani alishinda bila chakula yaani ilikuwa ni mwendo wa kumkomoa tu.
Baada ya Siku kama tatu hivi Nomani iliamuliwa ahamishwe gereza kwa sababu alionekana kuwa na hatari kukaa na wenzake.
Ilikuwa Jioni Giza likiwa linaanza Nomani akiwa kafungwa mikono na miguu alianza kuhamishwa gereza huku akiwa anapelekwa gereza la watu watukutu, Gereza hilo lilikuwa Katikati ya pori kubwa, tena pori ambalo lilikuwa limezungukwa na wanyama wa kutosha na wakali, ilikuwa ni zaidi ya pori nene , na huko ndiko aliko pelekwa Nomani.
Safari ile ilichukua karibia Siku nzima mpaka kufika huko, na Nomani alikuwa kawekewa ulinzi haswa, ila Nomani ndani yake alikuwa anatetemeka na kuogopa muno, yaani alikuwa anajiona Kabisa maisha yake ndo baasi tena.
Baada ya kufika kwenye lile gereza baada ya Nomani kuona tu mazingira ya lile gereza alijua maisha yake ndo basi, kwanza askari walio mpokea tu walikuwa na Sura ngumu na ya ukauzu kama wameramba Sumu.
Siku ya kwanza tu pale gerezani Nomani alipokelewa na kipigo, tena kipigo Cha bila sababu, yaani alidundwa haswa na Askari wa pale, na hiyo ilikuwa kama kumuonesha Nomani kwamba pale hakuna masihara.
Nomani aliyaanza maisha ya pale gerezani kinyonge, alipokelewa na wababe wa pale, yaani Nomani aligeuzwa mtumwa alikuwa anapewa Kazi na kila mfungwa mule ndani, yaani mtu yeyote akijisikia kukunwa au kufanyiwa masaji anamuita Nomani, yaani Nomani aligeuka mfanyakazi wa wafungwa mule gerezani.
Na mbaya Zaidi katika gereza hilo askari walikuwa hawaingilii hovyo hovyo Mambo ya wafungwa labda mpaka kuwe na vagi kubwa.
Mambo yalienda mbali Zaidi baada ya Nomani kuonekana ni mtoto wa Mama, huku kila mfungwa akiwa anashangaa kwa nini dogo laini laini kama yule kaletwa kule, basi kuna kundi la wababe kama watatu ambao walikuwa wanaogopewa na gereza zima mpaka maaskari, Siku hiyo baada ya kuona dogo Nomani masaji alizo wafanyia hazijawatosha waliamua kumfanyia kijana ukatili.
Nomani aliingiliwa nyuma na wale majamaa tena kwa nguvu na wote watatu walifanya hivyo kwa dhamu, kutokana na maumivu pia kutokwa na damu nyingi kutokana na kuchanika vibaya, Nomani alizimia baada ya kufanyiwa kile kitendo
Ndani ya gereza lile kulikuwa na wafungwa asilimia kubwa wakiwa na roho mbaya, ila wale wachache wenye huruma walimuonea huruma mumo dogo Nomani kwa kile alicho fanyiwa, kwanza ilibidi wamsaidie na kumpeleka kwa askari magereza, baada ya hapo Nomani alipelekwa kwenye kitengo Cha afya ili kutibiwa.
Nomani alikuja kuzinduka baada ya masaa kama 24 kupita yaani Siku nzima, na kijana alikuwa anajisikia maumivu makali muno sehemu ya haja kubwa, yaani alikuwa kila akikumbuka majamaa walivyo mfanya basi machozi tu yanaishia kumtoka.
Nomani alitibiwa Siku kama tatu hivi, kabla hajapona hata vizuri alitolewa na kurudishwa kwa wafungwa wenzake.
"Dogo ukiwa zoba zoba na Mzembe utaendelea kuwa mboga ya wahuni, ili uishi humu inatakiwa uwe na roho ngumu, changanya roho mbaya la sivyo utakufa kabla hata huu mwaka haujakata!" Baada ya Nomani kurudishwa mule ndani alifuatwa na jamaa mmoja mbavu, hayo ndo maneno aliyo ambiwa Nomani.
Basi kijana Nomani alikuwa anamwaga tu chozi.
Zilipita Siku mbili huku Nomani akiwa bado anapelekeshwa na kutumikishwa.
Ndani ya gereza hilo ilikuwa ni kawaida kwa baadhi ya wafungwa kuchaguliwa kwenda porini kukata kuni, na magogo kwa ajili ya kazi za hapa na pale, na Mara nyingi ilikuwa kila wafungwa wakienda huko porini lazima mfungwa mmoja au wawili waliwe na wanyama wakali.
Pia ndani ya msitu huo ilisadikika kuna mizimu na majini ya kutosha,kwa hiyo hakuna mfungwa ambaye alikuwa anapenda kwenda huko porini, pamoja na kwamba wafungwa hao walikuwa wanaenda bila Askari yeyote anaye walinda, lakini hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anathubutu kutoroka.
Bahati mbaya kwa Nomani akiwa hata hajapona vizuri, Siku hiyo naye alipewa nafasi ya kwenda huko porini na wenzake, kutokana na uzembe na ulegevu wa kijana Nomani kila mtu aliamini kijana huyo hatorudi huko porini.
Wafungwa kama ishirini walichaguliwa,na kweli wafungwa wale waliingia porini kukata kuni.
Kijana Nomani kutokana na vitisho alivyo pewa kuhusu lile pori alikuwa anaogopa isivyo kawaida.
Kazi ya kukata kuni iliendelea kule porini, Siku hiyo ilikuwa kama Siku mbaya kwa wafungwa wale, wakiwa wanaendelea na ile shughuli Mara walivamiwa na kundi la mbwa mwitu kule porini, hakika Siku hiyo kila mtu alitafuta pa kukimbilia, wengine walipotelea porini Zaidi na kuliwa na wanyama wengine wakali wengine walijeruhiwa na wale mbwa mwitu! Katika wafungwa ishirini walio enda porini ni wafungwa sita tu ndo walirudi na katika hao sita wanne walikuwa wamejeruhiwa.
Wawili walirudi wakiwa hawana hata alama ya kuumia na miongoni alikuwa ni kijana Nomani.
Wafungwa wengi walishangaa Nomani kurudi mzima, kutokana na ule mshangao Nomani alijikuta anaanza kupata ujasiri na kujiona anaweza.
Zilipita Siku mbili nyingine, ila yale mawazo ya Nomani kuingiliwa nyuma na wale majamaa yalikuwa bado hayajaisha.
Ilikuwa ni majira ya jioni, Nomani akiwa kaelekea kwenye mabafu ya kuogea katika pita pita yake, alikuta kuna jamaa anaoga alafu pembeni kaweka bonge ya kisu na dispisi mbili alafu na msokoto wa bangi.
Nomani alijikuta akili ya haraka haraka inamjia Kwamba aibe kile kisu kwa ajili ya kujirinda, ni kweli kijana Nomani haraka haraka aliiba kisu na disipisi moja baada ya hapo alichomoka maeneo yale kama mshare.
Nomani kile kisu alikificha kwenye suruali yake kiasi kwamba kuonekana ingekuwa ngumu.
Siku hiyo ilipita huku Nomani akiwa kalala na kisu.
Ilikuwa Siku nyingine wafungwa wote siku hiyo walikuwa wamepelekwa kwenye mazoezi, yaani yalikuwa ni mazoezi adhabu, ukiwa lege lege na dhaifu wanakuta umekauka damu.
Mazoezi hayo yalipigwa mpaka muda wa chakula, baada ya hapo wafungwa ndo walipewa muda wa kupumzika.
Masaa yalisogea hatimaye ilifika Jioni nyingine tena.
Kijana Nomani akiwa katulia sehemu huku anawaza mambo yake, alimuona miongoni mwa jamaa walio mfanyia unyama akiwa anakatiza anaelekea maeneo ya mabafuni.
Nomani aliamua kumfuata yule jamaa kwa nyuma nyuma, yaani Nomani kifua chake kilikuwa kinazidi kupandisha hasira kila alipo mwangalia yule jamaa , alafu alikumbuka na kile walicho mfanyia.
Yule jamaa alifika bafuni, na kuanza kupata starehe zake, ilikuwa ni bangi anavavuta, basi jamaa alijisahau kama yupo Nyumbani yaani alikuwa anavuta bangi alafu anajiona kama yupo jiji la maraha.
Nomani akiwa upande wa nyuma alichomoa kile kisu na kumsogelea yule jamaa ambaye utamu wa bangi ulikuwa umemkolea haswa.
Nomani alinyanyua juu kisu tena kwa nguvu na kumkita nacho yule jamaa shingoni, yaani kisu kilikitwa nusu kitokezee upande wa pili, yule jamaa hakupiga hata kelele yaani pale pale damu zikiwa zinamtoka alidondoka chini.
Nomani akiwa na roho ya ujasiri alikivuta kile kisu na kukichomoa, hapo ndipo damu zilitoka kama maji kwenye shingo ya mhuni yule.
Nomani alipangusia nguo za yule jamaa kile kisu chake baada ya hapo alichomoka mule bafuni.
Ila bahati mbaya akiwa anatoka mlangoni alikutana na jamaa mwingne miongoni mwa wale watatu walio mfanyia unyama, na jamaa huyo alikuwa anaelekea mule bafuni kuungana na mwenzake ambaye alikuwa katangulia kupiga bangi.
Yule jamaa pasina kugundua lolote alipishana na Nomani.
Kijana Nomani naye baada ya kugutuka aliona ni muda wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, haraka haraka yule jamaa akiwa hajafika hata pale mwenzake alipo fia, Nomani alimfuata kwa nyuma na kumchoma kisu Cha mgongo, yule jamaa akiwa anashituka na kugeuka Nomani alichomoa disipisi na kumkita nayo kwenye shingo, yaani alimkita nayo kama Mara tatu hivi hapo damu tu ndo zilionekana kuruka kila sehemu, Nomani alilowana damu mwili mzima.
Kama kawaida Nomani alifuta kisu chake damu na dispisi.
"Bado mmoja!!" Hayo ni maneno ambayo Nomani alijisemea kwa hasira na ujasiri mkubwa baada ya hapo alificha kisu na ile disipisi kwenye nguo zake.
Wakati anatoka huku mwili mzima ukiwa umelowa damu kuna wahuni wawili alipishana nao mlangoni.
Hazikupita sekunde hata tatu wale majamaa walipiga kelele kuita watu waje wajionee kilicho tokea, yaani ndani ya sekunde kumi tu ni kama wafungwa wote walihamia kule mabafuni.
"Kudadeki yule dogo ndo kafanya hivi mbona anaonekana fara fara fulani hivi"
"Duuuuu!! Kumbe dogo ana Mambo eeee!!"
"Sema afadhari, maana hawa wapuuzi Walikuwa wanajiona gereza wamejengewa wao"
Hizo zilikuwa ni kauli mbali mbali za wafungwa maeneo yale ya bafuni.
Askari magereza walifika kushuhudia kile kilicho tokea kwanza hapo ilibidi Nomani afuatwe kule aliko enda.
Nomani alikutwa kakaa kwenye korido huku akiwa katapakaa damu mwili mzima, tena alikuwa anakinoa kile kisu kwenye sakafu.
Wale askari magereza walimkamata Nomani na kumpokonya kile kisu, baada ya hapo walianza kumkokota ili wakamfungie kwenye chumba Cha barafu.
Muda huo huo yule jamaa ambaye ndo rafiki wa wale wawili walio uawa na Nomani alifika pale akiwa na hasira,bila kujari maaskari walio mshika Nomani,moja kwa moja alimvaa Nomani mwilini.
Je hili ndo gereza la kutisha linalo zungumziwa au kuna jingine, usikose sehemu zijazo.
Tukutane sehemu ya 13
0 comments:
Post a Comment