Tuesday, November 28, 2023

YATIMA GEREZANI 05

 



YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 5.


"Nomani sikiliza, huyu mwanamke humu ndani siyo Mama yako mzazi, pia yule Samir siyo mdogo wako wala siyo mtoto wa Baba yako Mr Fekon " Hizo, zilikuwa ni taarifa za kushitua kidogo kwa kijana Nomani ambazo zilifanya kwanza agune ikiwa ni ishara ya kuto kuziamini zile taarifa.


"Uncle Olenashi kwani we unazungumzia nini mbona sikuelewi!?? Kama yule siyo Mama Yangu, eheee Mama yangu nani Sasa!?" Nomani akiwa kwenye sintofahamu na mshangao aliuliza.

"Nomani kwa leo tuishie tu hapa na hicho ndo kitu Cha wewe kukijua, hata huyo unaye mwamini na kupeleka shida zako Mara kwa Mara siyo mtu mzuri usiende tena!!" Mlinzi yule alizidi kuongea maneno yaliyo zidi kumuacha Nomani njia panda Zaidi.


"Mtu yupi ambaye namuamini ambaye unamzungumzia wewe!?"

Nomani aliuliza.


"Huyo unaye endaga kupeleka shida zako, baba yake na Victor!!" Nomani alizidi kumshangaza Olenashi kwa kusema yule rafiki wa marehemu Baba yake eti naye siyo mtu mzuri.


"Aaaaaaa!! Sasa uncle hapo umeanza kuniongopea, Baba yake na Victor angekuwa siyo mtu mzuri angenitolea ada shuleni kipindi kile na kunisaidia Mambo mengine!?" Nomani bado alikuwa haamini.

"Sikiliza kuna Siku wewe uliniuliza Dosomi ni nani si unakumbuka!?? Sasa kama ulikuwa humjui Jina lake yule ndo anaitwa Mr Dosomi Jina la utani tajiri asiye na kazi, Sasa wewe endelea kumpapatikia kama hayajakutokea puani, Awamu hii umekoswa koswa, ila Awamu inayo fuata sijui itakuwaje!" Olenashi alikuwa anatoa taarifa ambazo zilibaki kuwa mshangao kwa kijana Nomani.


Nomani alijikuta anaanza kuunganisha baadhi ya matukio, hapo picha ilianza kumjia kichwani, alikumbuka maneno ambayo alikuwa kayasikia Siku ile ambayo Farhan alikuwa kaingia kwenye chumba Cha Mama yake usiku hapo aligundua kuna kitu kipo nyuma ya pazia.


"Lakini Farhan Mimi Samir tangia mdogo nimemlea na Baba wa kambo tena kwa Siri, leo hii upo hutaki kufanya kazi kwa ufanisi, nimekwambia hakikisha yule mwanasheria unaelewana naye" hayo Ni miongoni mwa maneno ambayo Nomani aliyakumbuka na alikuwa kayasikia kutoka kwa Mama yake akiwa anamwambia Farhan siku Hiyo.

Baada ya Nomani kukumbuka mazungumzo yale aliyo yasikia siku ile hapo alijikuta kaanza kuamini maneno ya mlinzi olenashi na pia kuunganisha maneno ya doctor Devi kuhusu kifo Cha Baba yake.


"Uuuuuu!! Au huyu Farhan ndo Baba yake na Samir ndo maana Samir kabadili mpaka majina!!?" Nomani alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi, mpaka olenashi aliamua kumshitua.


"Nomani sikiliza! Farhan bado hajarudi na muda wowote anaweza akarudi kwa hiyo akikukuta hapa hilo tatizo, zingatia niliyo kwambia, kama unaweza toroka kabisa hapa mjini nenda sehemu nyingine!" Olenashi alitoa ushauri ambao Nomani aliona haufai.


"Hapana Mimi lazima nijue ukweli, naenda kituoni kufungua kesi kwamba Mama kanifukuza Kwenye Mali za marehemu Baba Yangu!" Nomani akiwa na akili ya kufikiria karibu alifanya maamuzi ambayo yule mlinzi alikata asifanye hivyo, ila kijana aliamua kuwa mbishi.

Nomani usiku huo alilala kwenye kibanda Cha mlinzi, ila kulipo karibia kukucha tu aliondoka bila kumuaga olenashi, maana aligundua akiaga basi ataanza kupewa ushauri wa hapa na pale ambao kwa upande wake aliona ni wa kipuuzi.


Kukiwa kumeanza kupambazuka Nomani akiwa bado hajapona vizuri, aliwahi kituo Cha polisi, na alipokelewa vizuri kabisa.


"Mimi nimefukuzwa nyumbani kwenye nyumba ya marehemu Baba Yangu, wakati Mimi ndo mwenye haki zote" hayo ni baadhi ya maelezo machache ambayo Nomani aliyatoa pale kituoni, basi aliulizwa baadhi ya maswali na alimtaja mpaka marehemu Baba yake, pia huyo Mama yake.

Askari waliahidi kumsaidia kijana huyo, na kweli mida ya mchana ulipo fika walimpigia Simu Mama samir alikuja pale kituoni kutoa maelezo.


Siku zote pesa Ina maelezo mazuri  zaidi ya maelezo yenyewe, Mama Samir aliongea na wakubwa wa kituo kile, kitu alicho zungumza na wale wakubwa kilikuwa Siri yao, ila Nomani aliambiwa akae pale kituoni basi ikifika jioni atakuja kuchukuliwa na mtu anaye muamini ili akakae sehemu Salama wakati Jambo lake linafanyiwa kazi.

Nomani alikuwa hana wasiwasi kwa sababu aliamini yupo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.


Jioni ilifika Nomani akiwa bado yupo pale kituoni alishangaa kumuona Baba yake na Victor anakuja pale kituoni kumchukua.


"Nomani vipi mwanangu shida gani tena ambayo umeipata mpaka unakuja kituoni bila kunipa taarifa, si unakumbuka nilikwambia kukiwa na shida yoyote nambie!!?" Basi baada ya Baba victor kufika pale aliongea kistaarabu huku akiwa anamshika shika nywele kijana Nomani.

Basi Nomani alijisikia faraja na kuhisi kama yupo na Baba yake, yaani alisahau yale maneno yote ya olenashi kwamba Baba yake na Victor siyo mtu mzuri.


Basi Nomani alichukuliwa na baba yake na Victor kwa ajili ya kwenda kukaa kwa mheshimiwa huyo.


"Aaaaaaa!! Tajiri asiye na kazi nambie ndugu yangu upo kweli wewe!?? Mbona adimu hivyo!?" Nomani na Baba victor wakiwa wanaondoka basi kuna askari alimtania Baba victor huku akiwa anaongea kwa kucheka, na Baba victor alionekana ni mtu anaye Juana muno na Maaskari wa pale kituoni.

Baada ya Nomani kusikia jina Hilo hapo ndo yale maneno ya olenashi kumhusu bwana huyo yalimjia.


Nomani alitaka amwambie Baba victor kwamba yeye haendi naye ila alijikuta tu kwa muonekano wa Bwana yule anapuuzia, pia alikumbuka jinsi mtu huyo alivyo kuwa mtu wa karibu kwa Baba yake, aliamua kupuuzia.

Nomani na Baba victor walipanda kwenye gari binafsi ya mheshimiwa huyo na kuondoka maeneo ya pale kituoni.


Safari yao ilikuwa siyo nyumbani kwa kina Victor, bali walienda kuishia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ipo katikati ya mji kabisa,mule Ndani mlikuwa kimya kweli kweli mpaka Nomani alijikuta kaanza kuogopa Sasa.


"Nomani karibu, jisikie upo huru, haya ni makazi yangu mengine kwa hiyo wewe utakaa hapa sawa eeee!?" Baba victor aliongea akiwa hana wasiwasi huku anajichekesha.


"Eeeeee!! aaaaaaa kwani hapa ntakaa pekee Yangu!?" Nomani ilibidi aulize.


"Nomani hapana kuna Mama anakaa hapa, huyo ndo utaishi naye, muda huu nadhani atakuwa yupo jikoni kupika kwa sababu nilimwambia nakuja na mgeni!" Baba victor alizidi kuonesha wema mbele ya Nomani na kumfanya Nomani kutoa mashaka yote dhidi ya Mtu huyo.

Muda ule ule kuna Mama Mtu mzima alifika pale na kuwakaribisha kwa kuwachangamkia.


"Vipi chakula tayari mgeni ale!?, maana Mimi nina haraka ya kuondoka!" Baba victor alimuuliza yule mwanamke.


"Chakula tayari, ngoja nikalete vipi na wewe unakula!?" Yule mwanamke alimuuliza Baba victor, basi Baba victor alijibu huku akiwa anasimama kuonesha ana haraka muno.


"Aisee Mimi nina haraka kunawatu wananisubiri, Nomani naona una njaa wewe kula alafu pumzika baadae ntakuja kukuona!" Baba victor aliongea maneno ambayo yalimfurahisha Nomani, maana kweli Kijana alikuwa na njaa ya ukweli ukweli.

Basi yule Mama mtu mzima aliandaa vizuri chakula, alikipakua na kukitenga mezani.


"Kijana Karibu chakula wewe kuwa huru tu!!" Yule Mama baada ya kutenga chakula aliondoka na kutoka nje.

Nomani alisogea pale mezani huku akiwa anakimezea mate kile chakula haswa maana ilikuwa siyo kwa kunukia kule.

Nomani katika malezi yake alikuwa kafundishwa kwamba asile chakula kabla aliye kiandaa hajamnawisha na kumruhusu aendelee kula, kwa hiyo Nomani alipo sogea pale mezani alitulia na kumsubiri yule Mama muandaaji ili aje aruhusu shoo iendelee.


Nomani japo kuwa alikuwa anatamani kuanza kula chakula kile, ila aliona siyo ustaarabu kabisa kuanza kula kabla mkubwa na muaandaaji wa  kile chakula hajakaa pale mezani.


(kuna muda tunafundishwa na wazazi vitu vidogo vidogo tunaona havina maana nakupuuzia, ila amini kwamba kila kitu mzazi anacho kufundisha basi ujue kina maana kubwa, maana hakuna mzazi anaweza mfunza mwanae ujinga, na hicho kitu kilimsaidia Nomani Siku hiyo)


Nomani baada ya kukaa dakika kama tatu pale mezani huku akiwa anameza mate tu, aliamua kutoka nje kwenda kumchungulia yule Mama kama yupo karibu au katoka ili yeye afanye maamuzi ya kujinawisha na  kuendelea kula ama laaa.

Nomani aliangaza pale nje hakuona mtu yeyote, wala dalili ya mtu kuwepo.


"Aaaaa!! Mimi naenda kutwanga aisee, nisije kufa njaa bure maana huyu Mama haeleweki!" Nomani baada ya kutoona mtu alijisemea mwenyewe, baada ya hapo aliamua kurudi Ndani.

Ila bahati mbaya mule Ndani mlikuwa na paka, na paka huyo alikuwa mwizi mwizi, baada ya Nomani kutoka nje tu yule pakaa alianza kujigongea chakula pale mezani.

Nomani wakati anaingia Ndani alikuta pakaa kajibweda juu ya meza anakula, basi ilibidi amfukuze kwa hasira huku akiwa anaamini yule pakaa anapunguza chakula.


Nomani alikaa mezani na kunawa vyema, kisha alijiwekea chakula chake kwenye sahani, ilikuwa ni pilau kwa samaki.

Nomani akiwa na midadi kweli na kile chakula haswa, alikula kijiko Cha kwanza, akiwa anataka kula kijiko Cha pili alisikia jikoni kuna vitu ni kama vinapiga makelele na kugombana.

Nomani ilibidi aache chakula na kwenda kuangalia ni kitu gani, Nomani baada ya kufika jikoni alishangaa kuona yule paka aliye kula chakula akiwa anajipiga piga kwenye mavyombo huku damu zikiwa zinamtoka mdomoni na puani.

Nomani akiwa anazidi kushangaa alishuhudia yule pakaa anakata moto na kufa pale pale, mpaka hapo Nomani hakuelewa imekuwaje paka yule afe kwa taabu vile Mara tu baada ya kula kile chakula.


Aisee nasema yajayo ndo mazuri Zaidi hapa ni mwanzo tu, tukutane sehemu inayo fuata.




Tukutane sehemu ya 6


Download app yute kwa  simulizi zaidi

DOWNLOAD APP

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text