Tuesday, November 28, 2023

KICHAA MPELELEZI 34$35

 SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 34&35




Ndani


ya lile handaki nilibaki  mimi na Clara pekee wengine wote nilishawaua kwa sindano📌 yenye sumu kali sana,  nilisimama mbele ya Clara huku nikiwa bado nimeshika ile sindano ambayo bado ilibakiza sumu kwenye bomba lake, Clara alitoa macho ya mshangao 😳 mithili ya songombinyo baada ya kuona nimewaua wale wanajeshi waliokuwa wakimuunga mkono na sasa nimesimama mbele yake nikiwa na hasira☹️ isiyo kifani, wakati huo nje ya handaki lile ilikuwa ikisikika milio ya mabomu ikirindima kila kona "Unadhani ukiniua ndio na wewe utakuwa umesalimia, hebu sikiliza huko nje milio ya mabomu inavyorindima kama milio ya radi kipindi cha masika😃 ukiniua utatokea wapi, maana upande wa pili wa hili handaki linatokea Mexico tena msituni ambapo wanajeshi wa hapa wakizidiwa wanaenda kujificha huko kwenye msitu wa nchi ya Mexico na kutoka hapo msituni mpaka ufike Mexico city ambapo ndio mji mkuu wa Mexico unaweza kutumia takribani siku thelathini, kwahiyo mimi nachokushauri hakuna haja ya kununua maana na wewe utakufa😃 cha msingi ungana na mimi ili tuone namna ya kujikomboa sisi kama sisi, maana wewe unatafutwa na watu wangu wakuue na mimi natafutwa na wanajeshi wa kambi ya hapa Marekani ili waniue,  sasa cha kufanya wewe achana na kundi lako la wanajeshi na mimi niachane na kundi langu la majambazi tujenge maisha Mr. Brighton maana hata hivyo nimeyachoka haya maisha ya ujambazi" alisema Clara🤔 nikawaza na kuona hizi ni porojo,  maana tabia ni kama ngozi ya mwili hata ujichubue vipi ipo siku uchumi wa kununua vipodozi utayumba na hapo ndipo ngozi itakapokumbua, vivyo hivyo na kwenye ujambazi ipo siku ataishiwa na atatamani tena akavunje ili apate maokoto kama yale aliyokuwa anapata kipindi akiwa jambazi, nikawa nimuue au nifanye nini🤔 wakati huo milio ya mabomu ilikuwa inasikika kabisa karibu na mdomo wa handaki.


Huku zikisikika sauti zikiita kwa karibu karibu kabisa "Clara.... Clara" nadhani walianza kumtafuta Clara kwenye mahandaki😳 "Hapa nikiendelea kumsikiliza huyu mpuuzi mwishowe nitakutwa na watu wake hapa" Nikajisemea kimoyo moyo kisha nikamuweka Clara mabegani kwangu na kukimbia🏃‍♂️ ndani ya lile handaki ili nikatokee upande wa pili wa handaki lile ambapo ni msitu wa nchi ya Mexico, moyoni nishaamua moja kwamba huko msituni nitajitahidi kujificha nikiwa na Clara mpaka hali ya hivi vita ipoe ndipo nijitokeze naye nimlete kwenye kambi ya jeshi kusudi nipate maokoto yangu" Niliwaza huku nikikimbia ndani ya lile handaki nikiwa nikiwa nimembeba Clara. Nilikimbia umbali mrefu sana nikafika sehemu nikawa natembea maana nilikuwa nimechoka balaa😟 huku nikihema kama hata aliyetoka kukmbizwa ili achinjwe afanywe kitoweo,  giza likaingia nikiwa ndani ya handaki lile, sikutaka kulala nililembea ndani ya handaki lile usiku mzima kwa kutumia mwanga wa tochi wa simu yangu. Na kweli palikua mbali kwasababu nilitumia siku tatu mpaka nikafanikiwa kutoka ndani ya handaki lile na kuingia kwenye msitu wa Mexco. Nikiwa napita mule msituni kwa mbali sana nilisikia sauti za watu wakielekezana 😳 "Nyie piteni na njia hiii na sisi tupite na njia hii" nilisikia sauti hizo huku milio ya mbwa ikisikika kila kona. Nikawaza watakuwa labda ni wanajeshi na mbwa wao lakini hapana hawa ni majambazi wenzie na Clara kwasababu Clara asishawahi kuniambia kwamba endapo mwenzao wa muhimu atapotea basi mara nyingi huwa natumia mbwa wao wanaowafuga na kuwapa mafunzo ya kumtafuta mtu kwa kunusa aidha apatikane akiwa hai ama mfu.


Hapo nikaamua nisitembee na njia bali mikate njia yangu pekee yangu katika vichaka, nikatoa bastola kibindoni mwangu ambayo nilichukua kwa wale wanajeshi niliowaua  ndani ya handaki, nikawa  natembea kwenye vichaka huku nikiwa nimeishikilia mkononi na Clara nikiwa nimembeba mabegani, mabuti yangu ya kijeshi yalinisaidia dhidi ya miiba mikali katika pori lile, Nilitembea umbali mrefu  sana ambapo nilifika sehemu ambayo kulikuwa na jiwe kubwa sana na chini yake kulikuwa na pango kubwa, nikaamua kujificha hapo na Clara, kwa bahati nzuri mbele ya pango hilo kulikuwa na kichaka ambacho kilikuwa na miti yenye matunda ya porini ambayo yanaliwa na chini kulikuwa na maji, tuliyatumia matunda na maji kama chakula, kwa kweli tulikaa mule kwa takribani siku saba, mapenzi yangu na Clara yakarejea tena😍 kiasi kwamba tukawa tunafanya michezo ya kikubwa kaka baba na mama, mguu wa Clara ukaanza kupata nafuu japo sio kivile, basi mchana mmoja nikiwa nimekaa na Clara kimahaba 😍 nje ya pango lile ghafla nikashtukia😳 tumezungukwa na mbwa wakubwa kama saba hivi, walianza kubweka, sijakaa sawa wakatokea watu waliovaa kininja yani walifunika nyuso zao  na kuacha sehemu ya macho tu🥷 moja kwa moja nikatambua ni wenzake na Clara lakini moyoni nikasema kwa jinsi nilivyokuwa namkoleza Clara na mapenzi😃🥰 mpaka anatoa matusi akijitukania mwenyewe mama yake basi anaweza kunitetea. Niliwaza🥱hivyo....


Je itakuaje? Narudi🏃‍♂️


Pakua app ili kujuzwa endapo simulizi imetolew

NOTE:APP haiko play store INA bidi ufuate maelekezo yote ili kuipata

DOWNLOAD APP



Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text