SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 32&33
Wakat
i naendelea kjiambulisha pale kwenyek jukwaa kuu kabla sijamalizia kujieleza na kukabidhi maiki🎤kwa Mc, ghafla😳 nikashtukia mkuu wa vikosi vya jeshi ametwangwa risasi, ubongo pamoja na damu vikanirukia kwani alikuwa amesimama pembeni yangu, wanajeshi🧑🎨 walijaribu kuangalia huku na kule kuangalia kwamba ile risasi imetokea wapi, lakini wakati tukiwa bado kwenye mshangao, ghafla😳 nikakoswa koswa na risasi ya shingo ambayo ilinipita na kwenda kumtoboa jicho kiongozi wa mwingine wa jeshi aliyekuwa pale jukwaani, hapo sasa kila mmoja akaanza kukimbilia ndani mahandaki yaliyokuwa pale kwenye uwanja wa mazoezi wa kambi ya jeshi, nililimbia na kuingia kwenye handaki ambalo wanajeshi wanne walimuingiza Clara ili wamfiche, ajabu nilipoingia kwenye handaki lile nikashangaa😳 kuona wale wanajeshi wanne ambao walimzunguka Clara wakipambana kumfungua pingu kwa vifaa maalumu, "Haiwezekani mtu mweusi aje aheshimishwe kwenye taifa letu hali ya kuwa sisi wazawa tupo" niliwakuta wakiongea lakini bado walikuwa hawajanionaa maana walikuwa bize kuifungua ile pingu mikononi mwa Clara. Rohoni nikajisemea, hapa nimeingia choo cha kike acha nirudi nje kabla hawajanionaa" nilisema kimomoyo lakini ile nageuka ili nitokee nje ya handaki lile ghafla😳 nikasikia milio ya mabomu nje ya handaki lile, hali ambayo ilinijaza woga nikabaki nimesimama, nimeduwaaa nisiamini kabisa mambo yalivyobadilika kwa sekunde chache tu hali ya kuwa nilijua tayari nishamaliza kazi.
Nikiwa bado nimesimama nimeduwaa 😳 mara wale wanajeshi wakageuka na kuniona kwani tayari walikuwa wamekwishamaliza kumfungua Clara pingu. " Enhee mtu mwenyewe si huyu hapa, kwanza huyu tunamuulia humuhumu ndani haiwezekani mtu mweusi aje atunukiwe tunzo ya heshima kwenye taifa letu tena kwenye kambi ya jeshi isitoshe hata jeshini hajapitia, hii ni kudhalilisha jeshi letu hali ya kuwa jeshi la America ndio tunasifika ulimwenguni kwa kutengeneza mabomu ya nyuklia na silaha nyinginezo za kivita, leo hii mtu kutokea kataifa kadogo kama Tanzania anakuja kupewa tunzo nchini kwetu eti kwa kufanikisha kumkamata gaidi ambaye sisi wanajeshi tumehangaika kumtafuta kwa muda mrefu, habari hii hata muheshimiwa raisi Joe biden akisikia wanajeshi wote tutaachishwa kazi kwani ataona hana jeshi imara kwahiyo ili yote hayo yasitokee huyu afie humu humu" alisema yule mwanajeshi kisha akachomoa bastola kibindoni kwake😳 wakati anataka kunipiga risasi Clara akamzuia. "Hapana usimuue haiwezekani huyu fala afe kifo kirahisi namna hii, kwanza huyu ni msaliti na ndiye alisababisha nikavunjika goti sasa inatakiwa tuondoke naye akapate adhabu yake inayomstaili kwanza mlegezeni mwili ili tuondoke naye" Clara aliwaambia wale wanajeshi akimaanisha wanipige mpaka nilegee ili iwe raisi wao kuondoka na mimi. Clara alipotoa kauli hiyo ghafla😳 mwanajeshi mmoja aliruka teke la hewani hewa, buti lake zito🥾 likatua kifuani kwangu, chini nilianguka kabla sijasomama alinipiga mabuti ya mbavu nikatapika chakula chote nilichokula, yule mwanajeshi akaninyanyua kutoa pale chini, nikiwa tayari nimesimama, alinisukumia ngumi nzito ya mdomo iliyoning'oa meno mawili ya mbele ambapo nilitema damu zilizoambatana na yale meno mawili, hapo hasira zikazidi kunipanda☹️ kwani kabla sijapata hasira nilikuwa naogopa kupigana nao maana walikuwa wanne lakini nilivyong'olewa meno nikasema kimoyomoyo "hapa nikiwa mzembe wananiharibu sura hawa kama ni kufa acha nife kishujaa lakini siwezi kuruhusu nipigwe kiasi hiki kama ngoma"
Nilitema haraka damu iliyoambatana meno mawili, kisha kwa hasira nikafurumusha ngumi nzito ambayo iliishia kwenye mikono ya mwanajeshi yule baada ya kuweka hadi, yani kukinga kwa mikono yake naye bila kuchelewa akarusha ngumi akiielekezea usoni kwangu haraka nikainamaa na kumshona ngumi 🤜 nzito maeneo ya juu kidogo ya tumbo lake yani kwenye chembe cha moyo, maeneo ambayo ni hatari na isitoshe ile ngumi 💪 yenye uzito wa kilo moja ilimuingia vilivyo, alianza kuyumba yumba mithili ya mlevi wa mataputapu, bila kuchelewa nilimparamia na mateke kama vile napanda ngazi, nilikaanyaga tumbo lake na mguu wa kushoto kisha nikamalizia na mguu wa kulia kifuani kwake alianguka chini kama gunia la mahindi. Wenzake walipoona vile wakaona waingilie ligi😃 maana mwanzo walimuacha kwanza apigane na mimi ili waupime uwezo wangu.
Ile wanajileta wazima wazima niliruka mateke ya angani angani, mmoja nikamzibua teke nzito la sikio, na mwingine nikamkanyaga teke la pua, isitoshe nilikuwa nimevaa mabuti ya jeshi, walianguka chini, yule niliyempiga teke la sikio sijui nilimlimpiga karibu na mshipa wa fahamu maana hakuchukua muda akapoteza fahamu, huyu mwingine alikuwa amelala chini huku akiwa ameshikilia pua nahisi ilikuwa imevunjika, na yule niliyemshindilia ngumi ya chembe cha moyo akashindwa kabisa kunyanyuka chini akawa anagaragara tu chini, akabaki mmoja ambaye alikuwa amekunja ngumi, na mimi nikakunja🤜
"Aaaaaaaaaaaaaa" alipiga kelele kwa hasira huku akiruka juu na kujileta mzima mzima akiwa ametanguliza teke na ngumi zake kakunja, nilimkwepa kiaina😀 akadondoka chini haraka kama kicheche anavyomrukia kuku nami nikamrukia juu yake nilimtwangwa ngumi nyingi za macho mpaka macho yake yakafunga😵, huku yakitoa damu , mikono yake nikaikanyaga kwa mabuti yangu mpaka ikapoteza nguvu nikamsachi mfukoni alikuwa na sindano📌 yenye sumu, nikaanza kumdunga yeye kisha nikamalizia kwa wenzake, baada ya hapo nikasimama na kumwangalia Clara huku nikiwa bado nimeshika ile sindano yenye sumu mkononi☹️, Clara aliniangalia kwa woga huku akiwa ametoa macho😳 kwani licha ya kufunguliwa pingu alikuwa hana uwezo wa kusimama kwasababu goti lake lilivunjika, wakati huo nje ya handaki lile ilisikika milio ya mabomu, majangili walikuwa wanaharibu miundo mbinu ya kambi ya jeshi, basi nikiwa nimebaki na Clara wawili tu ndani ya handaki nikawaza na yeye nifamfanyaje maana wenzake tayari nilishawaua kwa sindano yenye sumu🤔 bila kuchelewa nikaamua ku..................
Je kama wewe ndio ungekuwa Brighton ungefanyaje? Hakika mambo ni moto
Namuuwa pia Kwa maana ni msaliti mkubwa mno
ReplyDelete