Monday, November 27, 2023

KICHAA MPELELEZI 31

 SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 31





Tulikaa pale kwenye ile mbuga kwa takribani masaa mawili, huku jua kali likitukaanga vilivyo😔 kwani eneo lile lilikuwa ni eneo la uwanda wa tambarare hakukuwa na mti hata mmoja wa kujinga na kivuli.  Tulikaa kwa takribani masaa mawili mara ghafla😳 tukashangaa kuona helcopter 🚁 tatu zikizunguka angani kama vile zinataka kutua katika eneo lile, mwanajeshi mmoja akatoa darubini yake🎥 kwenye begi lake na kuzichunguza zile ndege angani, "Jamani ni ndege za kijeshi za Marekani, nao wanazunguka angani wakitutafuta kwa darubini oneni," alisema yule mwanajeshi, nikaichukua ile darubini kisha na mimi nikachunguza angani ili nijionee mwenyewe😄 laaaa haulaaa kweli zilikuwa ni ndege za kijeshi za jeshi la Marekani, wote tulianza kushangilia mithili ya mashabiki ambao timu yao imesawazisha goli dakika ya 80 na kuongeza goli katika dakika za nyongeza😃. Wakati huo Clara alikuwa amenuna, uso wake ulipoteza nuru na furaha kabisa, ile haiba ya uzuri wa sura yake ulipotea kabisa, alikuwa amenuna😔 mithili ya mtu aliyesikia jirani yake aliyemzidi maendeleo yupo hoi kitandani kama sio wa leo wa kesho, basi mtu huyo akawa anazunguka kutangaza mitaani kwamba mwaka huu jiranj yake hatoboi lakini ajabu baada ya wiki kadhaa anashangaa😳 kumuona  jirani yake anadunda  barabarani ndio mfano wa Clara, aliombea tufie  wote msituni baada ya kuona eneo tulipo hamna mtandao, na hata tulipomgeukia Mungu na kumuomba atuokoe yeye alikuwa anacheka, Mungu akaamua kumuonyesha kwamba yeye ni muweza wa kila kitu akaamua kumuaibisha waziwazi. Basi bwana hatimaye helcopter🚁 zile zikafanikiwa kutua, makomando🧑‍🎨wale wa jeshi la Marekani walituletea chakula🍵 pamoja na maji, hapo tukaanza kula wakati huo wao wakiendelea kuipakia kwenye helcopter ile miili ya wanajeshi watatu waliokufa tukiwa njiani.


Clara alikuwa anakula  huku akiwa na mawazo, hata kumeza chakula  kwake ilikuwa tabu na chakula chenyewe alipewa tu kusudi asije akafa njiani kabla hajafikisha kwenye kambi ya jeshi la Marekani, alikula huku machozi yakimtiririka😭 nadhani alikuwa anajutia madhambi yake aliyoyafanya hakutegemea kwamba arobaini yake ingefika angali bado ni msichana mdogo kabisa tena mrembo kupindukia,  basi tulipomaliza kula Clara akachukuliwa  na kurushwa ndani ya helcopter kisha na sisi tukapanda na hapo rubani akaianza safari, tulichana mawimbi angali kwa takribani masaa mawili na nusu, hatimaye tukafanikiwa kufika kwenye uwanja wa mazoezi wa kambi ya jeshi la Marekani, vikosi vya majeshi vilikuwa vimejaa uwanjani kwa ajili ya mapokezi yetu,yani kitendo cha helcopter niliyopanda kutua chini pale mlangoni kulitetwa redi capet ambayo ilikuwa inaenda moja kwa moja mpaka kwenye jukwaa kuu walipo viongozi wakubwa wa vikosi vya jeshi. Nikashuka kwenye helcopter🚁 na kuanza kutembea kwenye red capet kuelekea kwenye jukwaa kuu huku kulia kwangu na kushoto kwangu wakiwa wamejipanga wanajeshi wananipigia saluti🧑‍🎨 nilipokuwa napita kuelekea jukwaa kuu. Nilisalimiana na viongozi wakubwa wa kijeshi jukwaani kisha nikakaa kwenye kiti nilichoandaliwa. Mkuu wa vikosi vya jeshi alipewa maiki na Mc atoe tamko lake baada ya sisi kufika salama kwenye kambi ya jeshi.


Mkuu wa vikosi vya jeshi alishika maiki kisha akawasalimia wanajeshi wote waliokuwepo pale akaniita mbele, "huyu ndiye shujaa wetu aliyehakikisha anapambana kwa akili mpaka tukafanikisha kumnasa gaidi mkuu wa kiitaliano aliyetesa taifa letu Clara Agustino, pongezi kwake🧑‍🎨" alisema mkuu vya vikosi vya jeshi kisha wanajeshi wote wakanipigia saluti kwa pamoja kisha nikapewa maiki nijitambulishe mbele ya vikosi vya jeshi na niseme chochote angalau kwa uchache. Nikaichukua maiki na kuanza kuongea huku mkuu wa vikosi vya jeshi akiwa amesimama pembeni yangu. "Mimi naitwa Brighton Lymo ni mtanzania ambaye nilijitolea kumsaidia kichaa aliyekuwa ameweka kambi nje ya nyumba yangu jua lake mvua yake lakini kwa ubinadamu nikaona si vizuri nimuache aendelee kuteseka nnje kwangu  na jua pamoja na mvua hali ya kuwa nina nyumba kubwa hapo nikaamua kumsaidia kibinadamu kwani pesa na mali ni vitu vya kupita tu lakini badae nikagundua kichaa huyo ni askari mpelelezi na pale nje kwangu alikuja kwa ajili ya kufanya upelelezi dhidi ya Mwanamke jambazi niliyekutana naye kwa muda mfupi nikaanza kuishi naye bila hata kumchunguza kumbe ni gaidi la kimataifa mimi siju...." Kabla sijamalizia kuongea ghafla😳 mkuu wa vikosi vya jeshi akatandikwa risasi ya kichwa, ubongo pamoja na damu vikanirukia, kabla sijakaa sawa nikakoswa koswa na risasi ya shingo, weeee wanajeshi wote walikimbilia ndani ya mahandaki kujificha maana hakuna aliyegundua huyo sniper aliyekuwa alisimama kwa wapi, nikakimbia🏃‍♂️ na kuingia ndani ya handaki aliloingizwa Clara na wanajeshi wanne, ile naingia nikapigwa na butwaa na kushangaa sana baada ya kuona😳.........


Je kipi tena kimetokea cha kumshangaza Brighton, 🤔 usikose sehemu ijayo maana moto🔥🔥🔥🔥 ndio kwanza unaanza🧑‍🎨



Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text