Tuesday, November 28, 2023

YATIMA GEREZANI 03

 



YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 3


Nomani akiwa anaangalia madaftari na baadhi ya mitihani ya majaribio ya Samir alishagaa jina ambalo Samir kaandika kwenye zile daftari na ile mitihani.


"SAMIR FARHAN SAID" Jina kwenye madaftari ya Samir lilisomeka hivyo, kwanza Nomani alimwangalia Samir Mara mbili mbili.


"Samir haya madaftari si ni yakwako au!??" Nomani alimuuliza Samir.


"Ndiyo ya kwangu!"Samir akiwa hana hata wasiwasi alijibu.


"Hili Jina umeanza kutumia lini, wakati ulikuwa unatumia, Samir Fekon!?" 


"Nilivyo ingia Darasa la sita kipindi hiki ndo nimeanza kutumia!?"


"Heeee!! Kwa hiyo hata Mama anajua!?"


"Yeye ndo aliye niambia nitumie hilo Jina!?"


"Heeeee!! Shuleni kwa hiyo hilo jina ndo wanakuita!?" 


"Ndiyo!! Mbona unauliza hivyo kuna ubaya!?" Samir aliuliza.

Nomani hakujibu chochote aliendelea kushagaa, muda ule ule Nomani akiwa kaduwaa na madaftari mkononi Mara Mama yake akiwa kaambatana na Bwana Farhan waliingia.


"Mama mbona Samir kabadili majina kwani kuna Nini!?" Nomani alimdaka Mama na swali juu kwa juu.


"We mpuuzi nini! Swali gani Sasa hilo unaniuliza!? Sikiliza Nomani sitaki tena kuulizwa maswali ya kipuuzi la sivyo ntakuwasha makofi!" Baada ya Nomani kuuliza alijibiwa kwa ukali muno na Mama yake na hiyo ilifanya afunge mdomo wake.


Siku zilizidi kusogea, kipindi Cha kwenda shuleni kilipo fika, Nomani alishindwa kwenda kutokana na kukosa pesa,  basi Nomani alijikuta ameanza kuwa mtu wa kushinda nyumbani, huku rafiki yake mkubwa akiwa mlinzi.

Nomani alikuwa anatamani Jinsi mdogo wake Samir anavyo pelekwa shuleni na Gari na kwenda kuchukuliwa na Gari, yaani alikuwa anatamani ile hali lakini kwa upande wake hiyo fursa alikuwa kanyimwa kabisa.


Mama Samir baada ya kuona ameanza kuwa bize ilibidi atafute mdada wa kazi kwa ajili ya kumsaidia kazi pale nyumbani.

Ila baada ya mdada yule kuanza kazi, Nomani alianza kunyimwa chakula pale nyumbani, alipo uliza aliambiwa ni maagizo ya Mama yake.


Nomani alijaribu kumuuliza Mama yake lakini majibu yake yalikuwa ni makofi mazito mazito, yaani kijana alikuwa anaona Mambo yanabadilika huku akiwa haelewi chanzo nini.

Nomani aliamua kwenda Sasa kwa mwanasheria wa familia ile kwa sababu alikuwa anamjua vyema.


"Kijana kwenye listi huku huonekani kama wewe ni Mtoto wa Mr Fekon, na maelezo yaliyopo ni kwamba Mr Fekon aliacha mtoto mmoja tu, na wewe ni Mtoto wa kulelewa na Mr Fekon tu,kwa hiyo pale Nyumbani huna haki yoyote!" Hayo yalikuwa ni maneno ya mwanasheria ambayo yalifanya Nomani mdomo uwe mzito kutamka neno lolote.

Hapo ndipo alipo elewa kwamba ule wasifu wa marehemu Baba yake ulikuwa haujakosewa bali ilikuwa ni vile vile.


Nomani aliondoka kwenye ofisi ya mwanasheria huyo kichwa kikiwa chini, yaani kulia alikuwa anashindwa hata kucheka anashindwa.


"Mbona watu walikuwa wanasema nafanana na Baba Sana, inakuwaje Sasa Mimi nisiwe mwanae mbona mapicha picha haya!!" Nomani alikuwa anajiuliza maswali ambapo mtu wa kumjibu hakuonekana zaidi zaidi majibu ya swali lake alikuwa nayo Mama yake.

Nomani Siku hiyo alirudi nyumbani akiwa amevurugwa haswa, yaani moja ilikuwa haisomi wala mbili, bahati nzuri alivyo fika nyumbani tu alikuta Mama yake naye ndo kafika.


"Mama ebu naomba nambie ukweli, nimeenda kwa mwanasheria kaniambia Mimi siyo mtoto wa Mr Fekon naomba urithibitishe hilo kwa sababu wewe ndo uliye nizaa na unamjua Baba Yangu!?" Baada ya Nomani kufika Nyumbani hakutaka kupindisha maneno tena aliuliza moja kwa moja.

Kwanza baada ya swali Hilo Mama Samir alipiga makofi huku akiwa anacheka.


"Yesssss!! Kumbe Nomani una akili eeee!?? Naona Sasa ushakuwa mjanja kama umeujua ukweli basi vizuri, ni kweli wewe siyo mtoto wa Mr Fekon, kuanzia leo hilo likukae kichwani kwa hiyo kama ulikuwa na wazo lolote kuhusu hizi Mali wewe sahau kwa sababu kila kitu ni Mali ya Samir" hayo yalikuwa ni maneno mazito ya Mama Samir ambayo yalifanya kijana Nomani mwili mzima ubaki ukitetemeka.

Nomani alitoka Ndani kwa hasira na kwenda kukaa kwenye bustani huku akiwa analia Muno, alikumbuka Jinsi ambavyo walikuwa wanapendana na Baba yake aliona haiwezi kuwa kweli kwamba yule Mr Fekon siyo Baba yake.


"Yeyo!! Heiii kijana vipi mbona walia kulikoni!??" Nomani akiwa anaendela kumwaga chozi Mara mlinzi wa getini alifika pale na kumuuliza.


"Aisee Mimi hata Sielewi, yaani naambiwa eti Mimi siyo Mtoto wa Mr Fekon, mwanasheria kaniambia, hata Mama naye kathibitisha hivyo hivyo, yaani uncle Olenashi hapa Mimi sielewi kitu kabisa" Nomani alikuwa analia kama haji kulia tena hivi.


"Nomani naomba nisikilize kwa Mara ya mwisho, ili uishi kwa Amani na bila hatari yoyote acha kuchokonoa mambo wewe kubaliana na kila kitu Alafu tulia kama hujui kitu, ukianza kupeleleza sijui hiki kimekaa hivi, hiki vile nikwambie tu utakufa unajiona!!" Mlinzi yule ambaye alikuwa kadumu pale nyumbani kwa kina Nomani Zaid ya miaka 15 aliongea maneno ambayo yalifanya Nomani amwangalie Sana.


"Uncle Olenashi Mimi sikubali lazima nijue ukweli wote, naenda kumuuliza Baba yake na Victor lazima yeye atakuwa anajua kila kitu kwa sababu yeye ndo alikuwa rafiki mkubwa wa Baba!" Nomani alikuwa hataki kuelewa maneno ya mlinzi, basi bwana Olenashi hakuongeza jambo lolote alimsikitia tu kijana Nomani.

Nomani alitoka pale nyumbani mpaka Nyumbani kwa kina Victor ambapo Baba yake na Victor ndo alikuwa rafiki wa Baba yake na kweli Nomani alimkuta mheshimiwa huyo akiwa yupo pale nyumbani.


"Uuuuuu!! Nomani kijana Wangu huwenda ni kweli au siyo kweli Mimi siwezi sema lolote, unajua ukweli wa Baba halali wa Mtoto Siku zote anaye ujua ni Mama" hayo yalikuwa ni majibu ambayo Nomani alipewa na Baba victor.

Nomani baada ya kuona majibu ya Bwana huyo hayaeleweki aliamua kurudi nyumbani huku akiwa mnyonge muno.

Maisha yaliendelea huku Nomani maisha yake yakiwa magumu muno pale nyumbani, maana ilimlazimu aende mtaani akatafute chochote kitu Alafu ndo ale, ila hali hiyo ilikuwa inafanya Mama yake ampige Sana.


"Nomani nishakwambia kazi unazo enda kufanya huko mitaani unatuzaririsha sawa eeee!? Ukirudia kwenda tena basi humu ndani usirudi na kama unataka hela ya kula basi kuanzia leo usafi wote wa mazingira ya nje utakuwa unafanya wewe na wale wafanya usafi ambao huwaga wanakuja kila jumatano na jmamosi wasije tena!" Hayo yalikuwa ni maneno ya Mama Samir baada ya kuona Nomani haachi kwenda mtaani kufanya vibarua.

Kuanzia Siku hiyo Nomani aligeuka kuwa mfanyakazi wa pale Nyumbani, yaani kazi zote zinazo husu mazingira ya nje kama kumwagilia maua, kupalilia na kuyatunza zilikuwa za kwake.

Nomani pale Nyumbani hakuishi kama mwanafamilia tena bali aliishi kama mfanyakazi, yaani maisha yaligeuka miguu juu ndani ya muda mfupi.


Rafiki mkubwa wa Nomani alibaki ni Bwana Olenashi ambaye yeye kazi yake ilikuwa ni getini.

Maisha yalizidi kusogea hatimaye mwaka mzima ulikatika Nomani akiwa kazoea mazingira ya kuwa kama mfanyakazi.


Siku hiyo ilikuwa ni sherehe ya kuzaliwa kwa Mtoto Samir pale nyumbani, kwa hiyo Mama Samir alikuwa kaalika watu na wageni mbali mbali ambapo wengine walikuwa ni marafiki zake, wengine marafiki wa marehemu mume wake.

Baadhi ya watu walio fika pale Nyumbani walishangaa Sana hali waliyo muona nayo kijana Nomani pale nyumbani, yaani alikuwa kachakaa haswa.


Basi kuna Mama ambaye alikuwa rafiki mkubwa na mtu wa karibu wa Mr Fekon ilibidi amuite na kumuuliza Nomani kuhusu hali yake, hapo kijana Nomani hakutaka kuvunga alitoboa kila kitu mpaka maisha anayo ishi pale nyumbani.

Mama yule alikuwa ni wale wamama wasio ona haya wala kusubiri, na walikuwa ni wale wamama wa michambo haswa, baada ya kusikia maelezo ya Nomani Mama yule aliyabeba kama yalivyo.


Sherehe zile zilinoga kweli pale nyumbani na watu walifurahi kweli, ila katikati ya sherehe Mama yule ambaye alikuwa anafahamiana vyema na Mr Fekon alilianzisha timbwili.


"Mama Samir ebu tunaomba tupe maelezo vizuri kuhusu Nomani, nimemuona mtoto kule nje anatumikishwa kazi, alafu nimemuuliza anasema eti ulimwambia siyo mtoto wa Mr Fekon, ebu toa maelezo wewe una ujasiri upi wa kumtenga mtoto tena ambaye ndo alikuwa kipenzi Cha Baba yake, na mtoto anafanana kopi na Mr Fekon, leo hii unataka udanganye watu yule siyo mtoto wa Mr Fekon hivi Mama zimo kweli!??" Ile sherehe Siku hiyo ni kama iliingia mdudu, yaani Mama yule alikuwa anabwatuka haswa.

Baada ya  maneno hayo basi watu wote ambao walikuwa wanamjua Mr Fekon walishituka na kuanza kushangaa.


"Aaaaaaa!! Masihara haya!! Wakati tunajua ile ndo chata ya Fekon iliyo Baki!!"

"Uuuuuu!! Wanawake hatuna aibu hivi unaanzaje kukataa Mtoto kama yule kwamba siyo wa Mr Fekon!?"

Basi maneno yalianza kuwatoka watu mule ndani, muda huo Mama yule ambaye alikuwa anaitwa Madam Helena, alienda kumuita Nomani pale nje, na alitoka kamshika mkono.


"Jamani ebu oneni wenyewe, hivi kwa mtu mzima yeyote unaweza ukamwambia huyu siyo mtoto wa Mr Fekon anaweza akakubali!??, Haaaaa Mama wewe ukikataa huyu siyo mtoto wa Mr Fekon Mimi nipo tayari hata mifupa ya rafiki yangu ikafukuliwe ili vipimo vije vifanyike, au kuna ajenda za Siri unaficha!??" Madam yule alikuwa hataki masihara, yaani maneno yake yalianza kumpatia nguvu kijana Nomani.


"Eeeeee!! aaaaa!! Hapana labda jamani kutakuwa kutoelewana kidogo, Mimi sijasema Nomani siyo mtoto wa Mr Fekon ni maneno tu ambayo kajitungia mwenyewe alafu kuhusu kazi, nimempatia tu adhabu baada ya kuona haniheshimu Mimi Mama yake" baada ya Mama Samir kubanwa Sana alijikuta anageuza maneno.

Basi baadhi ya watu walio kuja pale walimuasa Mama yule asijaribu tena dhambi kama ile, na siku hiyo sherehe iliisha kinyonge muno.


Kuanzia Siku hiyo ni Kama chuki za wazi Sasa kwa Kijana Nomani zilianza na Vita mpya ilizaliwa Kati ya Nomani na Mama yake.

Kwanza Nomani pale nyumbani alitimuliwa, yaani hakutakiwa kuonekana tena, Kijana Nomani alijikuta anaingia mtaani huku akiwa hajui anaenda kuanzia wapi.


Zilipita Siku kama mbili Nomani akiwa analala kwenye makaravati, ila tayari Nomani alihisi kuandamwa na watu.

Siku hiyo ilikuwa Jioni, Nomani alikuwa yupo njiani anatembea huku akiwa kajichokea muno na njaa kubwa inamtia adabu huku akiwa haelewi hata anako elekea, akiwa hana hili wala lile huku anatembea kinyonge, kuna pikipiki ilitokea kwa nyuma, Nomani aligongwa vibaya muno na ile pikipiki tena kwa makusudi.


Ile pikipiki baada ya kumgonga Nomani ilipitiliza kwa mwendo wa kasi muno, Nomani alidondoka chini pale pale huku damu nyingi zikiwa zinamvuja kichwani, maana alikuwa kajibamiza vibaya muno chini.


Hadith ndo kwanza inaenda kuanza Sasa, maana huku ni mwanzo mwanzo.


Tukutane sehemu ya 4


Downlo app yetu ili kujua kila simulizi mpya inapoingia

NOTE: APP haipo play store

DOWNLOAD APP

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text