YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA ðŸ˜ðŸ˜
Sehemu ya 2
Ila kwa upande wa mlinzi wa getini ambapo naye alikuwepo pale msibani yeye alitikisa kichwa kuonesha ni kweli marehemu kaacha mtoto mmoja, na mlinzi huyo alionekana ana Siri nyingi muno anazo zijua kuhusu familia ile.
Basi msoma wasifu wa marehemu alimaliza kwa kuwashukuru watu wote walio fika pale msibani kuwafariji.
Muda wa kwenda kuzika ulifika wale wa kwenda kuzika makaburini walienda, wengine walitangulia nyumbani akiwemo Mama Samir.
Kijana Nomani yeye hakutaka kuona mwili wa Baba yake kipenzi unazikwa bila yeye kushuhudia, kwa hiyo yeye ni miongoni mwa wale walio elekea makaburini kuzika.
Nomani alikuwa analia kwa uchungu muno mpaka watu walio fika kule makaburini walijikuta wanamuonea huruma kijana huyo, na kila mtu aliye muona Nomani na pia alikuwa anamjua Mr Fekon hakuhitaji utambulisho kujua kama yule ni mtoto wa marehemu kwa sababu Nomani alikuwa anafanana na Baba yake Muno haswa macho yao, yaani wote walikuwa na macho meupe kama watu wenye ulemavu wa ngozi hivi.
Mazishi yalimalizika baada ya hapo watu walitawanyika na baadhi walielekea nyumbani kwa Mr Fekon kwenda kuendelea kuwafariji wafiwa.
Nomani baada ya kufika Nyumbani alishangaa kuona bwana Farhan yupo bize pale nyumbani na wageni, yaani kama mwenyeji hivi, mpaka hapo Nomani aliamini yule ni mjomba wake kweli.
"Mjomba shikamo!?" Nomani aliamua kumfuata Mr Farhan pale alipo kuwa kakaa huku akiwa na maswali kazaa kichwani mwake.
"Marhaba vipi uncle, nikajua upo ndani?"Bwana Farhan akiwa anajichekesha alijibu.
"Hapana Mimi nimetoka makaburini, vipi mjomba, mbona Mama hajawahi kutwambia Kama wewe ni mjomba!?" Nomani aliuliza swali ambalo lilimshitua kidogo bwana Farhan.
"Eeeeee!! Usijali Mama yenu atawaelezea vizuri sawa eeee!??" Farhan alijibu kwa kupindisha.
"Sawa uncle, Alafu muda ule unasoma wasifu pale ulikosea badala ya kusema kaacha watoto wawili wewe ulisema mmoja!!" Nomani akiwa anaamini ilikosewa kweli basi alimkosoa bwana Farhan kikawaida tu.
Uncle mtu alitikisa tu kichwa kwa kujichekesha akionesha kwamba kweli alikosea, baada ya hapo Nomani aliondoka na kuendelea na Mambo yake.
Siku zilizidi kusogea watu pale nyumbani wakiwa wanapungua, baada ya kama wiki moja watu wote walitawanyika na walibaki wanafamilia tu, huku bwana Farhan naye akiwa ni mwanafamilia aliye "Farhan naona saizi Mambo yamepoa vipi umemalizana na kina Dosomi, maana sitaki Mambo ya pelepele baadae" wakiwa kwenye meza ya chakula Cha mchana, Mama Samir alimuuliza Bwana Farhan swali ambalo lilifanya Nomani aunguzwe na tonge la ugari kwa mshituko.
Ni Mara ya tatu alikuwa analisikia Jina la Dosomi tena kwenye maada ambazo hazieleweki, na tayari jina moja la Farhan alikuwa ashajua Kwamba kumbe ni mjomba wake, ila huyo Dosomi ndo alikuwa hamjui ni mtu gani.
"Eeeeee!! Mama Samir usijali wale nishawapanga na kesho nakutana nao kumaliza swala!" Farhan alijibu huku akiendelea kukandamiza chakula, Mama Samir na Farhan walikuwa wanazungumza maada zile wakiwa wanaamini Nomani na Samir hakuna wanacho kielewa.
Kijana Nomani alikuwa ni mtu anaye penda kuchunguza Mambo muno, baada ya kuona Jina la Dosomi linamtesa kichwani kwanza aliamua kumfuata mlinzi wa getini kwa ajili ya kumuuliza kama anamjua huyo Dosomi.
"Uncle Olenashi shikamo!!?" Nomani baada ya kufika getini alimkuta mlinzi akiwa anasinzia.
"Nomani marhaba, duuu bora umekuja ebu njoo tucheze hata karata maana nimekuwa mpweke kweli aisee!!" Basi yule mlinzi alimpokea Nomani kwa maneno ya kuchangamka.
Wawili wale walienda kukaa pembezoni mwa kibanda Cha mlinzi na kuanza kucheza karata huku wakiwa wanapiga stori.
"Uncle Ole samahani, hivi unamjua mtu anaye itwa Dosomi!?" Nomani aliuliza swali ambalo lilifanya kwanza yule mlinzi asitishe kucheza karata.
"Umesema nani Dosomi!?? Wewe umemjulia wapi!?" Mlinzi yule aliuliza kwa mshangao.
"Uncle unajua Mimi nimekuwa sielewi, yaani nasikia kila mda Mama analitaja hilo jina, hata Jana alivyo kuwa anaongea na uncle Farhan nilisikia hilo Jina la Dosomi linatajwa Sasa sielewi huyo Dosomi ni nani!?" Nomani alitoa maelezo ya kujitosheleza kwa yule mlinzi, ila mlinzi yule alishituka muno kutajiwa lile jina.
"Aaaaaaa!!! eeeeee!! Dosomi kiukweli Mimi sijawahi lisikia hilo Jina, alafu Nomani kwa nini wewe unafuatilia rafiki wa mama yako, hiyo ni tabia mbaya ni bora uache Mara moja sawa uncle!?" Akiwa anaonekana anaficha Jambo mlinzi yule aliamua kumzima Nomani, ila Nomani alikuwa na akili zake timamu aligundua kwamba yule mlinzi anamjua huyo Dosomi sema ameamua kuvunga tu.
"Duuuuu!! Sijui kwa nini namshitukia Mama Yangu ila naamini kuna kitu hakipo sawa kuhusu huyo Dosomi!? Lazima nijue huyo Dosomi ni nani!?" Basi Nomani alijiwazia pale na kuondoka kimya kimya bila kusema lolote kwa yule mlinzi.
Siku zilizidi kusogea hatimaye ilipita miezi miwili tangia Mr Fekon afariki, na hicho ni kipindi ambacho Nomani alikuwa kafauru baada ya majibu ya Darasa la Saba kutoka na kijana huyo alitakiwa kwenda kidato Cha kwanza.
"Nomani vipi,umefauru vizuri eheee mwanangu unataka kuja kusomea nini na kuwa mtaalamu wa vitu gani!?" Siku hiyo Mama Samir alikuwa kakaa na kijana Nomani pale nyumbani huku wakiwa wanacheza karata.
"Mama! Mimi nataka nisomee maswala ya biashara ili nije niendeshe biashara za Baba kwa ueledi mkubwa kama alivyo kuwa anafanya Baba!" Nomani akiwa na furaha alitoa jibu ambalo lilifanya Mama yake abadilike uso muda ule ule, yaani kutoka kwenye kucheka alikuwa mtu wa makasiriko.
Kuanzia Siku hiyo chenga chenga zilianza pale nyumbani, yaani Mama Samir alikuwa hataki kabisa Nomani aende kusoma.
Nomani ilibidi amfuate bwana mmoja ambaye alikuwa mtu wa karibu kabisa na Baba yake, yaani wawili hao walikuwa wanashirikiana kama ndugu, Nomani baada ya kumfuata alimuelezea shida zake zote, na Namna ambavyo Mama yake anampiga chenga kumpeleka shuleni.
Bwana huyo ambaye naye alikuwa na vibiashara vyake vya hapa na pale aliamua kumsaidia Nomani na alimpeleka shuleni.
Nomani alianza kusoma kidato Cha kwanza pasina Mama yake kuchangia hata Mia, na Nomani alikuwa anakaa shuleni.
Maisha ya Nomani pale shuleni hayakuwa mazuri kivile kutokana na kwamba pesa ya matumizi kwake ilikuwa changamoto, yaani hata yule rafiki wa Baba yake alikuwa kamsaidia tu kulipa ada ya mhura mmoja na kutoa pesa kidogo tu ya matuSiku zilizidi kusogea huku Nomani akiwa anaamini Kwamba dunia aliyo kuwa anaishi wakati Baba yake yupo hai ni dunia ile ile.
Hatimaye miezi kama mitano hivi ya Nomani kukaa shuleni akiwa hajawahi rudi nyumbani iliisha na ilikuwa ni likizo ndefu ya kurudi nyumbani.
Nomani alirudi nyumbani kwa bashasha kubwa akiwa kamumiss Mama yake na mdogo wake Samir.
Basi Nomani alipokewa vizuri na mlinzi wa pale getini, baada ya hapo Nomani alipitililiza ndani na tena Siku hiyo alisukuma mlango bila hata kugonga.
Nomani baada ya kuingia ndani ule mkao ambao alikuta Mama yake kakaa na mjomba wake pale sebuleni ulikuwa siyo mkao mzuri kabisa kwa Dada na kaka kukaa Kama vile.
"Pumbavu zako, kwa Hiyo Nomani huko shuleni uliko enda tena bila kunipa taarifa ndo huo ujinga mnao fundishwa kuingia ndani pasina kugonga milango!?" Baada ya Nomani kuingia alifokewa muno na Mama yake, huku makofi ya kutosha yakiwa yamempitia kwenye mashavu yake.
Basi Nomani aliishia kuomba msamaha ila Mama yake alionekana kukasirishwa kupita kiasi.
Siku ya kwanza ilipita, Siku ya pili nayo ilipita huku Nomani akiwa anaona mazingira ya pae nyumbani yamebadilika, yaani alikuwa haelewi elewi mchezo unao endelea.
Basi Siku Hiyo ilikuwa usiku Nomani akiwa kwenye chumba chake ambacho alikuwa kahamishiwa baada ya kukatazwa kulala na mdogo wake Samir, usiku huo alisikia kama kuna mtu anapita kwenye korido.
Nomani akiwa ni mtu anaye penda kuchunguza chunguza ilibidi aamuke kwenda kuona ni kitu gani kinapita kwenye korido usiku ule wa manane.
Nomani alibaki macho kodo, baada ya kumuona mjomba wake Farhan akiwa kavaa kiboksa tu huku anakatiza kwenye korido, tena akiwa hana hata wasiwasi.
Nomani alifuata nyuma nyuma kwa kujificha, kwa macho yake mawili Nomani alimuona Farhan anazama kwenye chumba Cha Mama yake.
"Haaaaa!! Huyu si uncle huyu, au naota!??" Nomani alijiuliza swali ambalo lilimshawishi kusogea kwenye mlango wa Mama yake.
Nomani alikaa pale mlangoni kama dakika kumi, Maneno na vitu alivyo sikia kule ndani hakika vilikuwa vya kushitua kwa kijana Nomani. we
Nomani alirudi chumbani kwake na kujilaza, ila mpaka inafika asubuhi kijana huyo hakupata usingizi tena.
Siku hiyo Nomani alichelewa muno kuamka kutokana na mawazo ambayo alikuwa nayo kutokana na kile alicho shuhudia usiku.
Maisha yalikuwa ni tofauti kabisa kwa Nomani kwa sababu awamu hii hata akichelewa kuamka alikuwa haamushwi kuja kunywa chai kama mwanzo, yaani awamu hii akiamka alikuwa anakuta kila kitu kishaisha kama ni chai basi ishapigwa yote.
Nomani baada ya kuona sehemu ya kutua mzigo ule wa kile alicho kiona usiku haipo, aliona ni Bora akapunguze mawazo kwa kwenda kumsimulia mlinzi wa pale getini ambaye walau alikuwa anampa kampani kidogo.
"Duuuuu!! Uncle Ole, wee acha tu, jana usiku nakwambia nimemuona ucle Farhan akiingia chumbani kwa Mama, huwezi Amini walicho kuwa wanakifanya na kukizungumza" Nomani aliongea maneno ambayo yalifanya mlinzi yule apate wasiwasi na kuangaza huku na kule.
"Eeeeee!! Hiyo kawaida tu Nomani vipi lakini shuleni nani alikupeleka, wewe si ulisema Mama yako hataki!?" Bwana Olenashi baada ya kuona Nomani analeta maada za uchonganishi ilibidi abadili maada kiujanja.
"Shuleni alinipeleka Baba yake Victor, yule rafiki yake na Baba, Japo naye kasema awamu ijayo hatanilipia tena ada!" Nomani alijibu majibu ambayo yalionesha kumshitua yule mlinzi kwa Mara nyingine.
"Heeeee!! Unataka unambie yule bwana mweusi anaye kujaga na kigari Cha blue hapa ndo alikupeleka wewe shuleni!?" Mlinzi yue jicho likiwa limemtoka ilibidi aulize kwa mshangao.
"Ndiyo ndo yeye!!" Nomani alijibu.
"Duuuuu!! Sasa Nomani sikiliza nikwambie kitu,ukitaka uishi kwa amani hapa Nyumbani wewe acha mumfuatilia Mama yako na kila unacho kiona ibaki Siri yako, pia maswala ya shule achana nayo kabisa" hayo yalikuwa ni maneno ya mlinzi yule ambayo yalifanya Nomani aamini kwamba mlinzi yule na Mama yake basi wote lao ni moja kutaka yeye asisome.
Nomani aliondoka bila kumjibu yule mlinzi neno lolote .Kadri Siku zilivyo zidi kusogea Nomani alijikuta anaona utofauti wa pale nyumbani, yaani Mama yake alikuwa anampuuzia na kutomjali tena.
Ilikuwa ni weekend tulivu kabisa huku pale nyumbani akiwepo Samir na Nomani tu, Siku Hiyo Nomani alikuwa anapitia madaftari ya mdogo wake ambaye alikuwa kaingia Darasa la sita.
Nomani akiwa anaangalia madaftari na baadhi ya mitihani ya majaribio ya Samir alishagaa jina ambalo Samir kaandika kwenye zile daftari na ile mitihani.
Ndo kwanza tupo mwanzo, kwa nini Hadith inaitwa Yatima na gereza la kutisha usijali utajua yote kuhusu huyo Yatima.
Tukutane sehemu ya 3
Mwendelezo
0692663502
Download app yetu ili kupata simulizi mpya
NOTE: App haiko play store
0 comments:
Post a Comment