Monday, November 27, 2023

SIMULIZI| KICHAA 01

  SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳🔥





Sehemu... 01 & 02.

Page   Bahari ya simulizi


Ilikuwa takribani siku nne zimekatika tangu nianze kumuona mwanaume kichaa nje ya jumba langu akiwa ameketi na makorokoro yake, siku ya kwanza niliogopa kidogo kwani alilala hapo na makorokoro yake mpaka kukakucha, siku ya pili pia alifanya hivyo lakini siku ya tatu nilianza kumuhisi vibaya maana vichaa wengi wamekuwa wakitumiwa na majambazi katika kazi zao atakuja karibu na nyumba yako atapiga kambi wewe utajua ni kichaa kumbe ni msoma ramani. Basi nikataka kwenda kunfukuza lakini roho yangu ilisita kwa woga kwani sura yake ilikuwa inatisha vibaya mno, rundo la nywele chafu lilijikusanya kichwani mwake na isitoshe alikuwa anavuta mamisokoto sijui ni bangi au ni gonzo mwenzenu nikajihami hata kumsogelea. Basi bwana usiku wa siku hiyo kulinyesha mvua kubwa sana, mvua ilipokatika nikatoka nje na tochi kuzunguka nyumba yangu niangalie usalama maana sikuwa na mlinzi bali nilikuwa naishi mimi tu na mke wangu Clara ambaye ni mzungu, naye tulikutana tu hotelini miezi miwili iliyopita nikiwa kwenye safari zangu za kikazi nikamtongoza akaubali basi nikamkaribisha kwangu na mabegi yake  niishi naye wakati tukiendelea kufanya mchakato wa kwenda kutambulishana kwa wazazi. Sikukagua mabegi yake kwani sisi waafrika mila zetu ni mwiko kukagua mabegi ya mgeni japo yalikuwa chumbani kwangu.


Basi bwana wakati nazunguka nyumba yangu huku nikitembeza mwanga wa tochi huku na kule ghafla nikamuona yule kichaa akiwa amekaa palepale anapopenda kukaa na alikuwa amenyeshewa na mvua vibaya mno, nikasema potelea mbali hata awe jambazi siwezi kuruhusu binadamu mwenzangu ateseke vile mimi nimelala ndani, kama anaiba aibe tu, mali hizi ni za kutafuta na tutaziacha duniani. Kwanza angekuwa jambazi asingekubali anyeshewe vile yule ni mwendawazimu" Nilijisemea nafsini mwangu na kwa huruma nikaenda kumchukua, lakini kuna kibegi chake chakavu na kilikuwa kimeloana sana aliking'ang'ania licha ya kumtaka akitupe lakini alikataa katakata, nikaona kubishana na chizi ni kujipa kazi nikamchukua vile vile na kibegi chake, nilienda kumuogesha vizuri bila kujali kwani wote ni wanaume, nilimpa nguo zangu safi avae usiku ule kisha nikamuonyesha chumba alale, aliingia chumbani na hakutaka kuachia kibegi chake nilijiuliza "Kwani hicho kibegi kina nini mbona huyu kichaa hataki kukiachia" nilijiuliza sana lakini mwisho niliona ni tabia ya vichaa kung'ang'ania vitu wanavyovipenda.


Basi nilipohakikisha yule kichaa Kalala na mimi nikarudi chumbani kwangu alipo Clara mke wangu ambapo alikuwa amelala tangu mchana, nilipoingia chumbani nikamkuta anajiandaa maana kuna baadhi ya siku alikuwa akitoka usiku kwa madai ya kwamba anaenda kumpa kampani rafiki yake wa kike kule hotelini asibaki mpweke nami sikuwa namkatalia maana huyo rafiki yake ambaye walikuwa wanakaa naye hotelini ndiye aliyeniruhusu niishi naye na hata siku nilipotoka safarini na Clara tulikuja na rafiki yake lakini yeye alifikia hoteli ya mtaa wapili na kwangu. Alidai ana mtu wake mara kwa mara anamtembelea hivyo anataka amkute hotelini na si kwa mtu. Basi Clara alipoondoka usiku ule nikabaki na maswali kichwani mwangu." Huyu mwanamke licha ya mvua yote hii kunyesha lakini hajaona haja ya kulala hivi ni kweli huwa anaenda kwa rafiki yake? Na begi lake dogo kabeba mbona hili kubwa limetiwa kufuli kuna nini ndani yake? Mh🤔 huku kukaribisha watu usiowafahamu vizuri ndani na mabegi huku hapana?" Niliwaza kisha nikaenda kuchukua plaizi ili nivunje lile kufuli nione ndani ya begi kuna nini halafu nirudishie kufuli kitaalam maana kazi hizo niliziweza.


Basi nikahangaika na kufuli mpaka likachomoka. Nikaanza kufungua nzipu taratibu huku mikono ikinitetemeka, ile natupia macho ndani ya begi😳 ghafla moyo wangu ulipasuka paaa mithili ya ukuni mkavu baada ya kuona slaha kali za kivita ambazo toka nizaliwe sijawahi kuziona. Macho yalinitoka 😳 kama dudumizi lilikabwa na kiazi cha moto kooni, ghafla uso wote ukaloa jasho licha ya chumba changu kuwa na kiyoyozi.. haraka nika.....


ACHENI NIFUTE JASHO KWANZA kisha niendelee maana Mika mimi mtanionea huruma kwa kilichoendelea. 

Follow our website for next  part

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text