Tuesday, November 28, 2023

YATIMA GEREZANI 04

 



YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 4.


Ile pikipiki baada ya kumgonga Nomani ilipitiliza kwa mwendo wa kasi muno, Nomani alidondoka chini pale pale huku damu nyingi zikiwa zinamvuja kichwani, maana alikuwa kajibamiza vibaya muno chini.


Baada ya dakika Kama tano wasamalia wema ndo walimuona Nomani, baada ya hapo ilibidi wamkimbize hospital kwa ajili ya matibabu.

Taarifa zile za kugongwa kwa Nomani zilimfikia Mama Samir, baada ya kupigiwa Simu na watu ambao walimtambua mtoto huyo.


Siku hiyo ilipita ilipo fika asubuhi na mapema Kabisa, Mama Samir akiwa na Bwana Farhan walifika pale hospital kuja kumuona kijana Nomani.

Mama Samir na Bwana Farhan hawakufurahia kabisa hali ya Nomani ambayo walimkuta nayo, walikuta kijana Nomani tayari kazinduka na alikuwa anaendelea vizuri huku bandeji zikiwa ziemjaa kichwani.


"Eeeeee Mtoto wenu hajaumia Sana, Zaid Zaid alichanika kichwa kidogo na ndo tumemshona kwa hiyo anaendelea vizuri baada ya Siku mbili nadhani anaweza kuruhusiwa kuondoka" hayo yalikuwa ni maelezo ya daktari ambayo yalifanya Mama Samir na Farhan wajichekeshe kinafiki ila walionekana kutofurahia kabisa.


"Daaaa!! Farhan ebu ongea na Dosomi basi awaambie vijana wake uzembe umezidi, ujue kuna Siku tutakuja kuingia kwenye matatizo kisa uzembe wa watu wachache!!" Baada ya kutoka mule ndani Mama Samir alionekana kumfokea muno bwana Farhan.


"Darling usijali! Nakuhakikishia kesho haifiki" Farhan akiwa anajichekesha alimjibu Mama Samir, na kwa Namna walivyo kuwa wanaongea ilikuwa ni uthibitisho tosha kwamba wawili wale wapo kwenye mahusiano.

Masaa yalizidi kusogea matibabu yakiwa yanaendelea kwa kijana Nomani, pia Mama yake alikuwa anakuja pale hospital na kuondoka huku akionekana ni mtu mwenye mipango yake.


Hatimaye ulifika usiku mida ya saa tano,  Nomani akiwa kwenye wodi yake, Mara alishangaa kumuona mtu anaingia mule ndani akiwa kavaa koti refu jeusi na barakoa ambayo ilikuwa imeziba uso wake wote.


"Aaaaa!! eeee wewe nani!!?" Nomani aliuliza kwa taabu huku sauti ikiwa haimtoki vizuri.

Ila mtu yule hakujibu kitu alicho kifanya alichukua sindano mfukoni mwake na kumchoma nayo Nomani, baada ya hapo alitoka nje, baada ya dakika kama mbili mtu yule asiye julikana alikuja na box kubwa, alimchukua Nomani na kumtia ndani ya box lile na kuondoka naye.


Masaa yalizidi kusogea hatimaye palikucha nakuwa asubuhi, kama kawaida Mama Samir na Farhan waliwahi asubuhi pale hospital huku wakiwa na matumaini ya kupata taarifa njema kumhusu kijana Nomani.

Baada ya Mama Samir na Farhan kufika pale hospital taarifa ambayo walikutana nayo ilifanya wampigie bwana Dosomi muda ule ule kuuliza.


"Dosomi ebu toa maelezo vipi nyie ndo mmemchukua Nomani siyo!??" Hilo lilikuwa swali la Farhan baada ya kumpigia huyo mtu anaye itwa Dosomi.


"Aaaaa!! Samahani bwana Farhan, aisee huyo mtu wenu tulikuwa tumechelewa, tulivyo fika tulikuta kashahamishwa!" Hilo lilikuwa jibu la bwana Dosomi ambalo lilifanya Mama Samir na Farhan waanze kukuna vichwa.

Upelelezi ulifanyika pale hospital lakini haikujulikana kijana Nomani kachukuliwa na nani au katorokaje, kwa sababu walinzi wa getini walikiri kutomuona akipita pale getini.


Masaa yalizidi kusogea hatimaye ilifika jioni nyingine tena Kijana Nomani alikuja kushituka akiwa ndani ya nyumba ambayo hakuelewa ni nyumba ya nani, kwanza alikuwa kafunikwa vizuri alafu katundikiwa na dripu.

Nomani alitaka aamini kwamba yupo hospital lakini kutokana na mazingira ya pale chumbani aligundua ile siyo hospital.


"Jamani kuna mtu!!? Msaada!!??" Nomani ilibidi aanze kuita baada ya kuhisi anaweza akawa yupo kwenye hatari.

Hazikupita dakika hata mbili alikuja Kijana ambaye Nomani alipo mwangalia vizuri alimkumbuka, alikuwa ni daktari ambaye alikuwa anafanyia kazi katika hospital ya rufaa, na Nomani alimkumbuka vizuri kutokana na kwamba kuna Siku daktari huyo alimuuliza Nomani maswali ambayo mpaka muda ule alikuwa hajawahi pata jibu lake.


"Naitwa doctor Devi, hapa ni Nyumbani kwangu kwa hiyo upo sehemu Salama usiwe na wasiwasi." Yule daktari alijitambulisha.


"Heeeee!! Sasa uncle kwa nini nipo hapa mbona sielewi na Mama yangu yuko wapi!?" Nomani akiwa haelewi kinacho endelea aliuliza.

"Labda samahani una uhakika kabisa yule ni Mama yako mzazi!?" 

"Ndiyo ni Mama yangu kwani kuna Nini uncle maana hili swali siyo Mara ya kwanza kuniuliza!?"


"Sasa kama ni Mama yako kwa nini anataka kukuuwa wewe,!?" Daktari aliuliza swali ambalo lilifanya Nomani ajilazimishe kuamka pale kitandani.


"Unasemaje!!?? Mama yangu anataka kuniua!??"Nomani aliuliza huku jicho likiwa limemtoka

"Ujue kijana kuna vitu sielewi, unakumbuka mwaka ulio pita, Mr Fekon alivyo pata ajari, yule Mama yako baada ya kuona Mr Fekon anaendelea vizuri alinifuata Mimi na kunipa dili la kumumalizia Mr Fekon kwa kutumia dawa ambayo ni sumu, ila Mimi ile kazi niliikata, lakini Cha kushangaza ilipo fika kesho yake Mr Fekon alifariki,na Mimi nilipo pima damu yake niligundua kafariki kwa Sumu, nilijaribu kupeleka ile inshu kwa mkubwa Wangu wa kazi pale hospital nilipewa onyo na niliambiwa ibaki Siri Yangu milele, ndo maana kama unakumbuka ile Siku Baba yako kafariki, nilikuuliza yule ni Mama yako mzazi, na ni mke wa Mr Fekon!" Hayo yalikuwa ni maelezo ambayo yule daktari alikuwa anayatoa kwa kijana Nomani.


"Inamaa..maa.maaaana!! Unataka useme Mama alimuua Baba, anataka kuniua na Mimi!?"Nomani mwili mzima ukiwa unatetemeka aliuliza.


"Huo ndo ukweli wenyewe, nasema hivyo kwa sababu Jioni ya jana pale hospital dalili nilizo ziona na pirika pirika za Mama yako, niligundua wewe hautakuwa Salama, na kweli Mimi ninavyo toka na wewe jana kuna watu nilipishana nao getini hata sikuwaelewa! Kwa hiyo litambue hilo na inabidi upeleleze vizuri je yule ni Mama yako kweli!?" Yule daktari alizidi kuongea kwa msisitizo, basi Nomani ilibidi akae kimya tu huku chozi likiwa linamtoka kama maji, yaani alikuwa haamini kama Mama yake ndo alimuondolea Baba yake.


Siku hiyo ilipita huku Nomani akiwa na mawazo kweli, kulipo kucha asubuhi Nomani akiwa anaendelea vizuri huku yupo kule chumbani, Mara alianza kusikia mabishano ya yule daktari na mkewe sebuleni.


"Devi nasemaje huyo mgonjwa wako simtaki humu ndani, Mimi sitaki matatizo jamani!"


"Lakini mke Wangu huyu mtoto anahitaji msaada kama nilivyo kuelekeza mwanzo, akipona ataondoka tu!"

"Devi Mimi sitaki tena sitaki kabisa kumuona humu ndani, kama unataka aendelee kukaa humu ndani basi Mimi narudi kwetu, akiondoka ndo utakuja kunichukua!"

Hayo yalikuwa ni mabishano ya doctor Devi na mkewe ambayo Nomani aliyasikia vyema Kabisa akiwa kule chumbani kwake.


Kijana Nomani alijikuta anajisikia vibaya muno kuona anakuwa chanzo Cha watu kugombana.


"Hapa sehemu ya kukimbilia ni kwa kina Victor sina Namna!" Hayo yalikuwa ni mawazo ya Nomani aliyo jiwazia baada ya kusikia wanandoa wanabishana kwa ajili yake.

Masaa yalisogea, ilipo fika mchana pale nyumbani akiwa kabaki mke wa Devi, huku Devi akiwa kazini, Nomani aliamua kujikaza na kuchomoka kule chumbani.


Bahati nzuri, mke wa doctor alikuwa yupo jikoni anapika, Nomani alitumia fursa hiyo kutoroka huku safari ikiwa ni kuelekea Nyumbani kwa kina Victor, yaani kwa rafiki wa marehemu Baba yake.

Wakati Nomani anafika pale nyumbani kwa kina Victor aliwashudia Mama yake na Farhan wakiwa wanatoka pale getini na Gari yao, baada ya hapo Baba yake na Victor alitoka nje na kuwapungia mkono ishara ya kuwaaga.

Nomani alijikuta ile hamu ya kwenda kuomba msaada kwa Baba victor inakata kabisa baada ya kuona yupo na Mama yake


Nomani kwa Siku hiyo aligairi kwenda nyumbani kwa kina Victor, kwanza ilibidi Kijana atafute sehemu ya kupumzika maana alikuwa kachoka muno, alafu kichwa kilikuwa kinauma kupita maelezo.

Giza likiwa limeanza kutanda uso wa dunia Nomani alichekecha kichwa aliona mtu wa kwenda kumsaidia ni bwana Olenashi, yaani walau amsaidie hata chakula.


Bila kuhofia wala kuogopa Nomani alienda mpaka kule nyumbani kwao, aligonga geti huku mwili mzima ukiwa unatetemeka.


"Heeeee!! Nomani ni wewe!?? Upo hai kumbe!?" Olenashi baada ya kumuona Nomani aliuliza kwa mshangao.


"Mimi nipo, ila usimwambie Mama kwamba nipo hapa maana nasikia yeye ndo alitaka kuniua, na pia yeye ndo aliye muua Baba!" Nomani mambo ya kukaa na Siri yalikuwa yanamshinda, alijikuta sasa anamwambia Olenashi zile taarifa.

"Shiiii!! Nomani ibaki Siri yako usije ukasikika au ukamwambia mtu hizo taarifa ni mwiko, Nomani Mimi najua Siri nyingi ambazo nikikwambia wewe najua ntakuwa nimekwisha ndo maana unaona nakuwa kimya, na naomba hata wewe uwe kimya  na ikiwezekana hapa mjini uhame kabisa" yule mlinzi aliongea kwa sauti ya chini ikionesha hataki mtu yeyote asikie.


"Uncle Siri gani Sasa hizo, si niambie hata mbili Mimi sitamwambia Mtu" Nomani aliuliza huku akiwa kamkazia macho yule mlinzi.


"Nomani sikiliza, huyu mwanamke humu ndani siyo Mama yako mzazi, pia yule Samir siyo mdogo wako wala siyo mtoto wa Baba yako Mr Fekon " Hizo, zilikuwa ni taarifa za kushitua kidogo kwa kijana Nomani ambazo zilifanya kwanza agune ikiwa ni ishara ya kuto kuziamini zile taarif



Tukutane sehemu ya 5


Download app yetu ili update simulizi mpya mapema


DOWNLOAD APP APP

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text