Wednesday, November 29, 2023

KICHAA MPELELEZI 39 TO 40

 


SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 39&40


"Mr Brighton🤔 hivi unadhani kama Clara ana mimba yangu nitakubali akahukumiwe, yani nikubali tu kirahisi mtu ahukumie hali ya kuwa ana kichanga changu tumboni😁 haiwezekani kabisa" alisema Mr. Michael. "Kwa maana hiyo unataka kusemaje🤔?" Nilimuuliza. "Ah mimi naona tu uachane na hizi habari za kumpeleka Clara kwenye kambi ya jeshi la marekani kwasababu kwa sasa Clara ni mama mtoto wangu mtarajiwa" alisema Mr. Michael "Wewe una uhakika gani kwamba mimba ya Clara ni ya kwako?" Nilimuuliza, wakati huo Clara alikuwa anacheka tu 😂 kwa jinsi tunavyobishana. "Sasa unataka tufanyaje?" Aliniuliza Michael. "Mi naona katika zile bilioni 20 ambazo ilitakiwa tugawane unipatie bilioni 10 nirudi zangu Tanzania kuhusu mimba mtajuana wenyewe iwe yako mama isiwe yako mimi sitaki kujua" Nilimwambia Mr. Michael. "Sasa kwani hizo bilioni 20 unazotaka tugawane ni zakwako ama ni za Clara alitoa kwenye account yake na kunipatia nifanye biashara kipindi nipo Oman?" Aliniuliza Michael na kuzidi kunipandisha hasira☹️ "Sililiza Mr. Michael izo bilioni 20 tulizipata kwa kuuza meli ya mizigo ambayo tuliiteka, tena katika hizo bilioni 20 ilitakiwa tugawane watu watano, mimi Clara pamoia na watu wake watatu sasa inakuaje leo hii unaingilia suala ambalo hulijui kiundani?" Nilimuuliza Mr. Michael. "Wewe kwanza unazitaka hizi pesa za wizi ili zikusaidie nini, jipange urudi Tanzania laa sivyo nitakupa kesi kwanza upo kwenye nchi yangu huna pasport ya kusafiria halafu unataka kukoroma kwenye nchi za watu, tafuta kazi upate pesa za kurudi nchini kwako , mambo ya nchi yangu yaache kama yalivyo" alisema Michael, moyoni nikasema huyu hanijui, nilimpiga ngumi👊 ya jicho la kushoto, kabla hajakaa sawa nilimrukia teke la tumbo alibamiza ukutani na kudondoka chini☹️ nilimfuata palepale chini na kuanza kumshindilia ngumi za uso, damu zilianza kumtoa puani na masikioni, kwa hasira☹️ alinisukuma kwa nguvu sana nikaanguka pembeni yeye akasimama, ile nataka kunyanyuka pale chini alinishindilia teke nzito la mbavu mpaka nikahisi bandama zimeoka, nilirudi tena chini, wakati najizoazoa pale chini ili nisimame tena alinirukia teke la uso kwa bahati nzuri kabla teke lile halijatua usoni kwangu nilifanikiwa kulidaka, alidondoka chini kama mzigo wa kuni.


Haraka nikamrukia juu yake, na kumkaba shingo yake kwa nguvu sana💪 huku nikiichomoa pingu yake aliokuja nayo kwenye Luksi ya suruali yake nikafanikisha kunfunga mikono yake na ile pingu aliokuja nayo kisha funguo ya pingu nikaweka mfukoni kwangu, wakati huo Clara alokuwa amenitolea macho ya mshangao😳 baada ya kuona nimefanikisha kumdhibiti Michael.  "Nisikilize Michael haijalishi Clara ana mimba yako ama sio yako, Clara ni muhalifu na ni lazima ahukumiwe kwa mujibu wa sheria, lakini sasa naona na wewe unataka kumtetea muhalifu mtu aliyeua mamia ya watu kisa eti unahisi ana mimba yako, hapa brother umeyakanyaga lazima wewe na Clara wote wawili muhukumiwe" Nilimwambia Mr. Michael. "Ni sawa lakini unadhani ukitupeleka kwenye kambi ya marekani ndio utapata sifa kwa viongozi wa nchi, sasa kwa taarifa yako nchi ya marekani, mwafrika ama black amerika yoyote hata afanye vipi hawezi kuthaminiwa, wewe unadhani viongozi wa jeshi ni wapumbavu kiasi hicho wakubali wewe muafrica utangazwe shujaa kwa kumkamata jambazi aliyetesa nchi ile hali wao wapo?, kwanza watadharaulika na hata kuachishwa kazi kwa kigezo kwamba wanajeshi wa taifa kubwa kama la marekani wanashindwaje mbinu na mtu ambaye ni mtu mweusi isitoshe sio hata mwanajeshi brother kwa taarifa yako hutatangazwa popote zaidi ya kusifkusifiwa tu palepale kambini na kupewa kifuta jasho chako kisha watakuaga halafu wao ndio watajimwambafai kwa viongozi wa nchi kwamba wao ndio wamefanikisha kumkamata Clara, mimi naona uachane tu na hizi habari , nitakupa bilioni moja urudi nchini kwako hizo ni pesa nyingi pia" alisema Michael. "Acha janja janja wewe  kwasababu nimeshakufunga pingu ndio unasema utanipa bilioni moja, lengo lako nishalijua unataka nikufungue pingu ili upate namna nyingine ya kunigeuka hilo haliwezekani acha nifanye mpango niwafikishe wewe na Clara marekani mengine tutajulia huko mbele🤔" Nilimwambia Mr. Michael.


Nilifanya mpango wa kuwatafuta polisi wa palepale station ya treni na kuwaelezea kila kitu, lakini wao wakadai hawawezi kufanya lolote kwasababu Michael ni usalama wa Taifa na cheo chake kipo juu yao wenye mamlaka ya kumkamata Michael ni mahakama ya kijeshi pekee endapo Michael anahatia, hivyo labda kwa kunisaidia wapige simu makao makuu ya kambi ya jeshi la marekani niongee nao wao ndio watajua wapi waanzie, "Sawa hata kwa msaada huo nitashukuru" niliwaambia, basi wakapiga simu📱 niliongea na viongozi wa kambi ya jeshi la marekani na kuwaeleza kwamba nimemkamata gaidi Clara na nipo station ya treni mjini Mexico hivyo nilihitaji msaada wao, sikuwaambia chochote kuhusu Michael maana ningewaambia kwamba nipo na Michael wangesema Michael atumie pesa ambazo alipewa kama adivansi ya kufanya upelelezi ili jambazi Clara apatikane, jambo ambalo Michael asingekubali sasa nikatumia mbinu huzo ili wakija wakute na Michael ninemfunga pingu, endapo wataniuliza sababu nitawajibu kwamba Michael alitaka kunigeuka ili ashirikiane na Clara kisa anahisi mimba aliyonayo Clara ni ya kwake. Basi waliahidi ndani ya masaa mawili watakuwa wamefika, nikakaa kusubiri. "Mr Brighton hii ni vita umeanzisha dhidi yangu na wewe, nitaachishwa kazi lakini na wewe sitakuacha salama" alisema Mr. Michael kwa kunipa maneno ya vitisho, sikumjibu kitu zaidi ya kumkalia kimya, hatimaye baada ya masaa mawili na dakika kadhaa kupita  helicopter🚁 ya jeshi la marekani iliwasili, kwanza wanajeshi walishangaa sana baada ya kushuka kwenye helicopter na kukuta nimemfunga pingu mr Michael, walipouliza kulikoni niliwapa sababu kwamba Michael alitaka kunigeuka ili ashirikiane na Clara baada ya kuhisi Clara ana mimba yake hivyo nikamdhibiti Michael kwa kufanya vile ili Clara afikishwe kwanza kwenye vyombo vya dola maana ni muhalyeye  "Hongera sana kijana wewe ni shujaa, Mr Michael kwanza umeenda kinyume na sheria za kuwa askari wa usalama wa Taifa, kwanz hutakiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muhalifu, nafikiri suala hili litashughulikiwa na mahakama ya kijeshi tuondokeni" alisema mkuu wa kikosi kile cha jeshi kilichokuja kutoa msaada, tulipakia kwenye helcoper na safari ya kuelekea marekani ilianza, siku hiyohiyo, maamuzi juu ya Clara na Michael yalitolewa baaada ya kufika marekani. Ilitakiwa Clara ateswe kwa siku saba ndipo auwawe kwa kunyongwa lakini ilipobainika kwamba anamimba aliswekwa gerezani kwa miezi tisa mpaka ajifungue ndipo atasomewa tena mashtaka yake na atahukumiwa tena kwa mujibu wa vifungu vya sheria, Michael aliachishwa kazi kabisa kwa kujihusisha kimahusiano na muhalifu, hivyo mimi nilibaki kwenye kambi ya jeshi nikila bata tu😁 huku nikisubiri Clara ajifungue ahukumiwe nipewe mavumba yangu  nirudi TZD, Miezi tisa si haba Clara alishikwa na uchungu na kujifungua, ajabu Michael alituma barua za maombi kwenye ofisi kuu ya kambi ya jeshi akidai kwamba anataka tufanye vipimo vya DNA kati yangu na yeye ili ijulikane ni nani baba wa mtoto kati yangu na yeye, "🤔 Mh mara pap vipimo vya DNA vinaonyesha mtoto wa Clara ni wangu itakuwaje?" Niliwaza sana wakati huo tulikuwa tunasubiri majibu kutoka kwa daktari, baada ya  lisaa daktari alituita wote ndani😨


Nyieeee! Nyieee acheni tu itakuwaje ? Like coment nije chaaaaap

SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 40.


Baada ya daktari kukamilisha kufanya vipimo vyake ndani ya ofisi yake, alitoka nje na kutuita tuingie ndani kwa ajili ya kupokea majibu ya vipimo vya DNA, tuliingia ndani wote wanne, mimi, Clara, mr Michael pamoja na mtoto ambaye bado alikuwa hajapewa jina mpaka ajulikane baba yake😔 tuliingia ndani na kukaa kwenye viti vilivyokuwa mbele ya meza ya doctor wakati huo mapigo ya moyo wangu yalikuwa yanapiga kite kuliko kawaida yake, nilisali kimoyomoyo matokeo ya DNA yaonekane mtoto sio wangu, Doctor yule mwenye asili ya kiafrika aliniangalia machoni na kuniuliza "Mbona wewe kama unatetemeka sana shida nini" nilimwangalia sura yake nikagundua doctor yule ni mpare nikamjibu kwa kipare "Henaicho ivyo vipimo vitidhe😂" Nilimuuliza kwa kipare nikimaanisha kwahiyo vipimo vinasemaje?. "Avae mwana ni wako😁" Doctor alinijibu kilugha kwamba mtoto ni wa kwangu "😨Weeee mvwire uu mndu iti mwana ni wake, ambu wekimvira iti ni wangu henevuka vita ambu uu jamaa emanje iti mwana ni wake nivonia huruma ili ni isanga la vandu😭" Nilimwambia doctor amwambie Mr. Michael kwamba mtoto ni wake, maana Mr Michael anajua mtoto ni wake ili tu niepushe shari na nipokee maokoto yangu mengine yatafuata baada ya kushika maokoto yangu. "Daktari mbona siwaelewi mnaongea kilugha halafu nasikia maneno kama  huruma mnamaanisha nini sasa☹️" aliuliza Michael kwa ukali sana kwasababu kiswahili alikijua na isitoshe kuna maneno ya kilugha ambayo niliyatamka kiswahi kwa kutojua yanatamkwaje kilugha. "Ahhh unajua huyu jamaa kule kwetu Tz kimakabila ni mtani wangu sasa nimemwambia mtoto sio wake anasema eti nimuonee huruma maana anampenda sana Clara hivyo nikisema mtoto ni wake wewe utamuacha Clara hivyo atafanikiwa kuwa na Clara, na mimi siwezi kumwambia mtoto ni wake kamwe maana kwenye kazi hii nilikula kiapo" Doctor alimlaghai Mr. Michael kwa maneno ili mr. Michael asigundue chochote lakini ukweli ni kwamba mtoto alikuwa ni wangu ila nilicheza mchezo na Doctor na kumuahidi atapata malipo yake baada ya mimi kulipwa fungu langu.


Basi bwana Mr. Michael alifurahi sana 😁 baada ya kuambiwa mtoto ni wake, walikumbatiana na Clara kisha askari jela wa kike akamchukua Clara na kuondoka naye, akampeleka kizuizini ambapo alipewa muda wa kumlea mtito kwa miaka minne ili akuekue ndipo akabidhiwe baba yake Mr. Michael na ndiposa Clara ahukumiwe kwa mujibu wa sheria. Basi ilikuwa ni siku ya jumamosi kambi ya jeshi iliamuamua kunifanyia sherehe kubwa sana 🥰 kunipongeza kufanikisha kupatikana kwa Clara, na pia licha ya Mr. Michael kuachishwa kazi lakini alialikwa kwenye sherehe hiyo kusudi apewe pesa za mishahara yake ya huko nyuma ili aache kazi rasmi, hata hivyo kwa furaha ya moyo wangu nilimwalika Doctor shedy ambaye tulikula naye njama aseme mtoto ni wa Mr. Michael. Sherehe ilienda vizuri makomando wa kimarekani walionyesha uwezo wao wa kimazoezi mbele yangu mithili ya makomando wa kitandania wanavyoonyesha mbwembwe zao mbele ya muheshimiwa raisi😁 wapo walioruka sarakasi, wapo waliolalia ncha za misumari kwa migongo yao, hakika walikomaa migongo kama ngozi ya mamba maana misumari ilikuwa mikali sana, hata hivyo wapo waliotua chini kwa kamba helcopter ikiwa angani juu sana, kiufupi bwana 😁 nilienjoy, tulikula na kusaza kwani sherehe ile ilihusishwa wanajeshi tu na hapakuwa na kiongozi wa serikalini na sijui  kwanini walifanya vile hata hivyo sikutaka kuuliza nilichotaka ni kupata maokoto💸💵 yangu kwanza na sio vinginevyo, basi mkuu mpya wa vikosi vya jeshi akasimama kuhutubia kisha mbele ya halaiki ya watu niliwekewa bilioni 50 kwenye account yangu pesa ambayo ningekula mpaka kifo changu na bado ikabaki😁, si hiyo tu pia kuna wanajeshi waliungana na kuchanga bilioni ishirini nayo ikawekwa kwenye account yangu, yani kiufupi wengi walifurahishwa na ushujaa wangu kutokana na kwamba sikupitia mazoezi yoyote yale ya jeshi hivyo waliona kama ni kipaji ambacho ninacho na ilistahili kupongezwa


Basi, baada ya kukabidhiwa pesa zangu, mr Michael naye alilipwa pesa zake na kuachishwa kazi paleple, alipewa siku tano awe amerudisha sare ya jeshi pamoja na maganbuti ya jeshi kwani kutoka wasaa ule yeye ni raia kama raia wengine, pia mkuu wa jeshi alinieleza kwamba iwapo kesho yake nitasafiri kurudi Tanzania basi nisisahau kuacha mawasiliano yangu maana mimi kwao ni kama ndugu na iwapo baada ya miaka minne kupita kama watanihitaji kwa ushahidi zaidi juu ta hukumu ya Clara basi nitatakiwa nirudi tena marekani nitoe ushahidi. Nilikubaliana naye na kumueleza kwamba nitatoa ushirikiano kadri ya uwezo wangu endapo watanihitaji, basi mchana tulikula na kusaza hatimaye usiku tukakusanyika kwenye bwalo kubwa la kijeshi ambapo wanajeshi walitakiwa kunywa na mimi vinywaji ili waniage kwa mara ya mwisho kwani kesho yake nilipanga kurudi TzD, Ndani ya bwalo pia Mr, Michael alikuwepo, hata Doctor shedy naye alikuwepo , watu walikunywa pombe balaa ila mimi nilikuwa soda, kwa kawaida wanajeshi vichwa ngumu sana hawalewi walikunywa mpaka saa sita usiku lakini bado walikuwa fiti, mimi nilikunywa tu maji kwa siku hiyo sikutaka kulewa lakini doctor Shedy alilewa mithili ya mlevi wa mataputapu, mara akaanza kuropoka mbele ya Mr. Michael na wanajeshi wengine 😳...........


Kiruuuuuuuuuu je itakuwaje sasa hili nalo ni Tatizo😂 acheni kwanza nimeze funda la soda niliyokuwa nakunywa maana imekwama kooni baada ya doctor Sheddy kuanza kubwabwaja.Nyieeee nyieeee acheni nirudi🏃🏿‍♂️📌


Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text