YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA ðŸ˜ðŸ˜
Sehemu ya 1
Kabla hujaanza kuisoma Hadithi hii nakushauri ukae na kitambaa Cha kujifutia machozi pembeni, maana naamini itakusisimua na kukutoa machozi, ni Hadithi inayo husu maisha ya kijana Nomani,ni Zaidi ya mikasa ambayo utakutana nayo kwenye Hadithi hii, hakika Nina imani utaipenda.
Mwanzo.
Ni Ndani ya Jumba la kifahari alionekana Mama akiwa na furaha huku akiwa anacheza na kucheka na watoto wake wawili ambao kwa muonekano tu kwa namna walivyo kuwa wanacheka Ni ishara tosha Kwamba Mama huyo alikuwa anawapenda muno Sana watoto hao na pia hivyo hivyo kwa watoto nao wakionekana kumpenda Sana Mama yao.
Furaha ile gafla ilikatishwa na taarifa zilizo letwa pale nyumbani kupitia Mlinzi wa getini.
"Olenashi tabia gani unaingia Ndani bila kugonga mlango, umeanza kuizoea kazi eee, Alafu vipi mbona unahemeana kulikoni!??" Mama wa familia ambaye alikuwa anaitwa Zena au Mama Samir aliuliza kwa ukali baada ya kuona Mlinzi wa getini kaingia mule Ndani kwa kasi tena bila kugonga mlango.
"Eeeeee!! Boss!!mkubwa eti!! eti!! Nanilihii!! Nasikia! Kananiii.!!" Mlinzi yule alionekana anababaika kutoa zile taarifa kwa sababu zilionekana ni taarifa za kutisha na kusikitisha.
"Kama huna Cha kuzungumza tafadhari toka nje" Mama Samir alifoka.
"Eti bosi kagongwa na gari, kafariki!!" Yule Mlinzi akiwa kakaza macho aliongea, kwanza Mama Samir pamoja na watoto wake walishituka.
"Olenashi ebu rudia, au hatujasikia vizuri!!"
"Mama muuza maandazi kaniletea taarifa pale getini, eti bosi mkubwa kagongwa na Gari kafariki, maeneo ya Ukumbi wa Mirenia" Mlinzi yule alirudia, na maneno hayo yalifanya Mama Samir aamuke haraka na kuchukua ufunguo wa gari, bila hata kujiandaa Mama huyo alitoka haraka na watoto wake kuelekea eneo la tukio ambako ndo aliambiwa tukio limetokea.
Walifika maeneo ya Ukumbi wa Mirenia sehemu ambako ndo ilisadikika ajari ile imetokea, baada ya kufika pale na kuuliza, ni kweli walithibitishiwa kwamba ajari imetokea ila mhusika wa ajari bado hajafariki na kakimbizwa hospital ya rufaa.
Taarifa za kutofariki kwa bosi mkubwa zilionekana kutomfurahisha Mama Samir, yaani kutoka kuwa na Sura ya wasi wasi baada ya kupata taarifa za ajari ya mumewe Sasa Sura ilikuwa siyo ya wasiwasi tena bali ilikuwa ya kukasirika na chuki.
Mtoto wa kwanza wa Mama huyo ambaye alikuwa anaitwa Nomani akiwa ni mtoto wa miaka 13 alishangaa kuona Mama yake anakasirika Zaidi baada ya kusikia ajari ile haijamfanya Baba yao afariki.
Pia Nomani akiwa ni kijana ambaye alikuwa anajua kunyumbua baadhi ya mambo japo kuwa alikuwa mdogo, alishangaa lile eneo ambalo ilidaiwa Baba yake kapata ajari, yaani lilikuwa ni eneo ambalo ni gumu kwa Mtu kupata ajari.
Kwanza lilikuwa eneo la parking ya magari, eneo ambalo watu wanao fika kwenye Ukumbi ule maarafu walikuwa wanapaki magari.
"Mama twende basi hospital tukamuangalie Baba!!" Nomani akiwa na wasiwasi na hali ya Baba yake aliongea.
Basi ni kweli Mama Samir aliingia kwenye Gari tena bila kujibu, baada ya hapo walielekea hospital yeye na watoto wake,ni kweli walipo fika huko walikuta Hali ya Baba Nomani siyo mbaya Sana japo kuwa alikuwa kagongwa vibaya Muno maeneo ya kiuno kushuka chini.
Nomani na mdogo wake Samir walikuwa wanamwaga tu machozi kwa hali waliyo muona nayo Baba yao.
Basi ilibidi watolewe nje ya wodi baada ya kuangalia hali ya mgonjwa, na madaktari walithibitisha kabisa kwamba mgonjwa wao atapona, japo kuwa hataweza kutembea tena katika maisha yake.
Mama Samir na watoto wake walitoka nje na kwenda kukaa kwenye korido huku wakiwa wanasubiri maelezo mengine ya madaktari, ila muda wote huo Mama Samir alionekana anajisemesha mwenyewe kwa makasiriko, yaani kama Mtu anaye nung'unika na kulalamika.
Baada ya hapo Mama huyo alitoa Simu kwenye mkoba wake, na alienda pembeni kabisa, nyuma ya wodi kuipiga Simu ile.Nyie vijana ebu muiteni Mama yenu aingie humu Ndani!??" Wakati Mama Samir ametoka na kwenda kupiga Simu, daktari alikuja na kutoa maelezo ya kumhitaji Mama Samir Ndani.
Nomani akiwa kama mkubwa ilibidi achukue jukumu la kwenda kumuita Mama yake ili aje asikilize wito wa daktari kule Ndani.
Lakini Nomani wakati anasogea kule nyuma ya wodi alianza kumsikia Mama yake akiwa anaongea sauti ya chini tena kwa kufoka.
"Dosomi!! Mnazingua tena siyo kidogo, mnafanyaje uzembe kiasi hicho, wapuuzi nyie mnaacha kukanyaga kichwa mnakanyaga kiuno, kwa hiyo ndo maelekezo mliyo pewa na Farhan!??" hayo ni maneno ya ukali ambayo kijana Nomani kwa masikio yake mawili alimsikia Mama yake akiyazungumza kwa mdomo wake, huku akiwa anaongea na Mtu kwenye Simu.
Maneno hayo yalifanya kijana Nomani arudishe mguu nyuma, na kugeuza kule aliko toka huku mapigo ya Moyo yakiwa yananenda kasi Sana.
Nomani akiwa kama mtoto alijiuliza maswali mengi kuhusu kauli ya Mama yake aliyo isikia ila hakupata maana ya haraka haraka, japo aligundua Mtu aliye kuwa anazungumzwa ni Baba yake, maana huyo ndo alikuwa kakanyagwa kiuno.
Basi baada ya dakika kama nne Mama Samir alikuja na kuwakuta wanae wakisubiri.
"Mama unaitwa na Daktari" Nomani alitoa maelezo huku akiwa kamkazia macho muno Mama yake, yaani alikuwa anamwangalia hamumalizi kabisa.
Dakika zilidi kusogea, baada ya dakika kama kumi Mama Samir alitoka kwenye chumba cha daktari na kuwaambia watoto wake waondoke.
Mama Samir na vijana wake alirudi nyumbani huku akionekana yupo bize kuchati na simu japo kuwa alikuwa anaendesha Gari.
Safari ya kurudi nyumbani ikiwa inaendelea Mara Simu ya Mama Samir iliita na Mama huyo aliwaangalia kwanza watoto wake baada ya kuona wapo bize na mambo yao alipokea.
"Dosomi sikiliza, maelezo yote anayo Farhan nimeongea naye, hakikisha haipiti leo, uzembe mwingine hautakiwi sawa eeee!" Hayo ni maneno ambayo Mama Samir aliyoongea huku Nomani akiwa anayasikia vizuri.
tayari kichwani mwa Nomani majina mawili yalikuwa yamekaa, yaani Dosomi na Farhan kwa sababu majina hayo Nomani alikuwa kayasikia kwa Mara ya pili yanatajwa na Mama yake.
Nomani alitamani amuulize Mama kuhusu kitu gani anakiongea na hao watu, ila kuna nafsi ilimwambia avunge na atulie, na kweli kijana Nomani alitulia.
Basi walifika Salama nyumbani ila bado Mama Samir hakuacha ubize wa kuongea na Simu tena inshu za ualakini ambazo kila Nomani alipo zisikiliza zilimtia mashaka.
Masaa yalisogea hatimaye ilifika usiku Nomani na mdogo wake walienda kulala katika chumba chao, na pia naye Mama Samir alielekea kulala chumbani kwake.
Masaa hayagandi, hatimaye palikucha huku Mama Samir akiwaamusha wanae, ili waelekee hospital kwenda kumjulia Baba yao hali.
Siku hiyo hata kifungua kinywa hawakunywa, maana ilionekana Mama Samir ana shauku muno ya kwenda kumuona mumewe hospital.
Baada ya kufika pale hospital walikutana na taarifa ya tofauti kidogo na matarajio, Baba Nomani au Mr Fekon kwa Jina maarufu la kibiashara tayari alikuwa kaaga dunia.
Nomani kwanza mapigo ya Moyo yaliongezeka baada ya kusikia taarifa zile, kwanza kijana alipiga Kelele kwa uchungu na alizimia pale pale.
Mama Samir naye alionekana analia kwa uchungu japo ilikuwa ni kwa unafiki ila alikuwa analia.
Samir naye alikuwa analia kivyake huku manesi wakiwa wamemshika, na kijana Samir yeye alikuwa na miaka kama 10.
Masaa yalizidi kusogea taarifa za kifo Cha Mr Fekon zilizidi kusambaa kwa wafanyakazi wa makampuni ya bwana huyo, pia kwa wafanyabiashara wenzake na Mr Fekon.
Mida ya saa Saba za mchana pale hospitali watu mbali mbali walikuwa wanakuja kuthibitisha kama kweli Mr Fekon ambaye alikuwa mfanya biashara mkubwa na tajiri kafariki.
Waandishi wa habari nao walikuwa wamekuja kwa wingi kuchukua taarifa za kile kilicho tokea mpaka Mr Fekon anaaga dunia.
Masaa yalizidi kusogea, Kijana Nomani alikuja kuzinduka baada ya kufika Jioni huku akiwa chini ya uangalizi wa daktari,na muda huo daktari alikuwa yupo mule chumbani.Baba!! Baba!! Baba Yangu Mimi!!" Nomani baada ya kuzinduka na kukumbuka tukio la Baba yake kufariki alianza kulia kwa uchungu kule kule chumbani.
"Samahani kijana, hivi huyo Mama hapo nje ni Mama yako mzazi!? Na ni mke wa Mr Fekon!?" Daktari yule ambaye alikuwa kijana kijana tu aliuliza swali ambalo Kijana Nomani aliishia kutikisa kichwa akionesha kukubali, japo kuwa hakuelewa kwa nini yule daktari kauliza vile.
Basi Daktari yule baada ya kujiridhisha na majibu yake alitoka nje kuwapatia taarifa wahusika kwamba mtu wao kazinduka, na kweli baada ya dakika tatu Mama Samir aliingia mule Ndani akiwa kaongozana na mwanaume ambaye Nomani alikuwa hamjui kivile japo kuwa alikuwa anamuona Mara kwa Mara anakuja nyumbani.
Siku hiyo ilipita huku Nomani na mdogo wake wakiwa wamerudishwa Nyumbani na kuambiwa watulie Ndani, ila Mama Samir yeye alionekana kuwa bize muda wote.
Kijana Nomani bado alikuwa na maswali mengi muno kichwani yasiyo na majibu na alikuwa haoni mtu wa kumuuliza.
Basi sekunde, dakika na masaa vilizidi kukimbizana hatimaye ilifika siku nyingine, pale nyumbani kwa kina Nomani Siku hiyo unaweza sema paligeuka kama kiwanda Cha kutengeneza magari, yaani idadi ya magari yaliyofika pale yalikuwa hayahesabiki, na hiyo ni kutokana na kwamba Mr fekon alikuwa mtu maarafu na tajiri.
Yaani watu wazito wazito walikuwa wanakuja kutoa pole na Salam za rambirambi pale nyumbani kwa kina Nomani.
Nomani akiwa katoka kuoga huku anavaa nguo nyeusi za maombolezo ili aende akakae walipo wanafamilia wenzake kwa ajili ya kupokea pole na Salam Mara Mama yake alifika kule kule chumbani.
"Nomani sikiliza, wewe bakia huku huku chumbani haina haja ya kutoka nje, na ukitoka ishia sebuleni, usije ukatoka kule nje kwenye maturubai Sawa eee!!?" Hiyo ni kauli ya Mama Samir ambayo ilifanya Nomani aache mdomo wazi.
"Mama mbona sikuelewi, naachaje kwenda kupokea pole kwenye kifo Cha Baba Yangu!?"
"Nomani Mimi nina sababu zangu na akili kuliko wewe, kama ni hizo Salam unazitaka basi Samir anakuwakilisha, maana wewe na Samir ni kitu kimoja, kwa hiyo wewe usitoke sawa mwanangu!" Mama Samir alizidi kujenga hoja ambazo bado kijana Nomani aliona haiingia akilini.
"Mama kwani Mimi nikienda kuna nini, Mimi siwezi kukaa humu Ndani aisee badala ya kwenda kupokea wageni huko nje, na unajua Mimi ndo mtoto mkubwa" Nomani aliendelea kuleta ubishi tena kwa hoja.
"Nomani mwanangu Mimi ni Mama yako, nayajua mengi kuliko wewe, unajua kabisa wewe ndo mrithi wa pekee wa Baba yako, na huko nje kuna watu wabaya na wazuri, na wote wanaiwinda hii familia, wewe ukiwa kama mboni ya hii familia sipendi likukute lolote baya ndo maana nataka ukae huku huku Ndani kwa usalama Zaid."Mama Samir alizidi kutoa vishawishi, awamu hii maneno hayo walau yalimkolea Nomani na alijikuta anapoa na kukubaliana na Mama yake.
Basi Siku hiyo wageni wengi muno walikuja pale nyumbani, huku Mama Samir na mwanae Samir ndo wakiwa ndugu wa pekee wa marehemu, wengine Walikuwa ni wale jamaa wa karibu na marafiki wa marehemu.
Siku hiyo ilipita, ilikuwa ni Siku nyingine ambayo mwili wa Mr Fekon ulikuwa unaenda kufanyiwa ibada kanisani Kabla ya kwenda kuzikwa.
Mr Fekon alikuwa ni mkristo mzuri kabisa, ila mke wake alikuwa ni muislamu mzuri kabisa, na ndo maana hata baada ya kupata watoto wawili waliamua kugawana majina, yaani Nomani na Samir.
Na mke wa Fekon ambaye ni Zena alikuwa hapendi Kabisa kuitwa Mama Nomani, vivyo hivyo naye Mr Fekon alikuwa hapendi kabisa kuitwa Baba Samir.
Kwa hiyo hata Siku hiyo ya ibada kuuaga mwili wa marehemu mume wake kanisani, Mama Samir yeye hakwenda.
Siku hiyo ilipita huku kanisani kukiwa na mafuriko ya watu na kipindi hicho chote Nomani aliambiwa akae tu Ndani na Mama yake.
Ilikuwa ni Siku nyingine ambapo Sasa ndo ilikuwa Siku ya mazishi, ila kabla ya kwenda kuzika ilitakiwa mwili wa Mr Fekon uagwe na wapendwa wake na familia yake iseme Jambo na wasifu wa marehemu usomwe.
Ilikuwa ni sehemu ya wazi ambapo karibia mji mzima ulikuwa umehamia pale kumuaga Mr Fekon, na hiyo Siku Nomani alikataa kabisa kubaki Ndani aliamua kulazimisha na kuelekea sehemu ya tukio.Basi taratibu za hapa na pale ziliendelea na ulipo fika muda wa mwanafamilia kutia neno lolote, Nomani alishangaa kumuona yule jaman ambaye kwa Mara ya mwisho alimuona hospital akiwa na Mama yake anasimama na kwenda mbele.
Bwana yule alijitambulisha Kama Farhan huku akijitambulisha Kama ni mdogo wake na mke wa marehemu, yaani Mama Samir.
"Heeeee!! Inamaana huyu ni mjomba!? Mbona Mama hajawahi kututambulisha!??" Baada ya utambulisho ule Nomani alikuwa anajiuliza maswali ambayo hayana hata majibu.
Basi bwana Farhan alizidi kutoa maelezo kuhusu Namna kifo Cha marehemu kilivyo tokea na Namna familia yake ilivyo pigwa na butwa na kupata pengo kubwa kuondokewa na mtu huyo.
Ulifika Sasa muda wa kusoma wasifu wa marehemu, na huo wasifu ndio ulio fanya maisha ya kijana Nomani yaanze kubadilika.
"Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 42, marehemu ameacha Mke mmoja na Mtoto mmoja" hayo ni maneno ya bwana Farhan ambayo yaliwashitua watu wengi ambao walikuwa wanamjua vyema Mr Fekon.
Kijana Nomani baada ya kusikia maneno yale aliamini msomaji atakuwa kakosea kutamka, pia baadhi ya watu nao waliamini msomaji kateleza ulimi.
Ila kwa upande wa mlinzi wa getini ambapo naye alikuwepo pale msibani yeye alitikisa kichwa kuonesha ni kweli marehemu kaacha mtoto mmoja, na mlinzi huyo alionekana ana Siri nyingi muno anazo zijua kuhusu familia ile.
Ni mengi yapo ndani ya pazia hatuyajui, ili kujua drama zote Ndani ya simulizi hii usikose sehemu zijazo!? Je ni yupi ni mtoto wa Mr Fekon na yupi siyo na kwa nini!?? hii ni stori ambayo naamini hutojutia kuifuatilia.
Tukutane sehemu ya 2
Download app ili kupata simulizi mpya
NOTE: App haiko play store
0 comments:
Post a Comment