Tuesday, December 5, 2023

YATIMA GEREZANI 8


YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 8.


Basi baada ya dakika kama mbili Dosomi na vijana wake walitoka kwa ajili ya kwenda kumsaka Nomani popote anapo kimbilia, yaani walijiapiza kwamba Siku hiyo lazima wamalize kazi.


Nomani mbio zake zilienda kuishia kwenye varanda la watu, yaani alikaa pale kwenye varanda huku akiwa anahema muno.

Bahati mbaya kwa Nomani ile sehemu ambayo alikuwa kakaa, mtu mwenye ile nyumba alikuwa katoka kuibiwa siku chache zilizo pita.


Nomani akiwa anahema pale varandani huku anakumbuka Jinsi alivyo koswa na risasi alishangaa kumuona mtu anatoka ndani kupitia mlango wa nyuma wa nyumba ile, mtu huyo alikuwa kashika bonge la panga.

Nomani baada ya kugundua anafwata ni yeye alianza kutimua tena mbio upya.


"Jamani mwizi!! Mwizi!! Kamata mwizi huyo!!" Awamu hii Nomani alianza kufukuzwa na nduru za wizi nyuma, Nomani alijikuta anajikojolea kwa Mara ya pili, huku nguo zake zikiwa zinaendelea kunuka, maana kijana alikuwa ashajichafulia.

Watu kibao walijitokeza kumkimbiza Nomani huku neno mwizi ndo likiwa linasikika.


Nomani alikuwa anakimbia kama hana akili nzuri, katika kukimbia Nomani aliona mbele kuna watu wamesimama wanamurika na tochi, muda huo nyuma kundi la watu lilikuwa linakuja.

Nomani akiwa anasema liwalo na liwe huku anasonga mbele, lahaula uso kwa macho alimuona Baba victor akiwa na vijana wake kule mbele huku wakiwa wanaangaza na tochi zao.


Nomani alitamani kurudi nyuma ila nako tayari watu walikuwa wanamfukuza, maeneo hayo palikuwa karibu na kambi ya jeshi na ndo sehemu pekee ambayo Nomani aliona anaweza kimbilia, maana mbele kulikuwa na wabaya wake, pia nyuma kundi la watu wakiwa wameshika kila aina ya siraha walikuwa wanakuja.


Nomani akiwa haelewi litakalo mtokea, aliruka ukuta na kuingia ndani ya kambi la jeshi, baada ya hapo alienda kujificha nyuma ya kibanda ndani ya kambi hiyo.

Nomani alitulia maeneo yale huku akiwa anahema haswa na harufu kali ikiwa inamtoka.

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, Nomani akiwa kakaa pale, Mara mbwa wa pale kambini walimuona na walianza kubweka huku wakiwa wanamsogelea, yaani walikuwa mbwa kweli kweli, na walikuwa wanatisha haswa.


Kutokana na uoga wa Nomani alianza kukimbia, hapo ndipo alipo haribu, maana wale mbwa walianza kumfukuza.

Nomani akiwa ndani ya kambi ile huku haelewi hata anako kimbilia alianza kupiga makelele, baada ya kuona mbwa wanakaribia kumnasa.


Nomani akiwa tayari ashadakwa mguu na wale mbwa, gafla wanajeshi kama wawili walifika na kuwafukuza wale mbwa.


"Dogo umetoka wapi mpaka unakuja kubwatuka humu ndani!?" Wale wanajeshi walimchukua Nomani na kuanza kumuuliza maswali.

Nomani alikuwa anatetemeka anashindwa hata kuzungumza, yaani mdomo ulikuwa mzito haswa, ni harufu tu za kinyesi na mkojo zilikuwa zinamtoka Nomani.


Nomani baada ya kukaa kimya alirambwa makofi mazito matatu, alijikuta anaona dunia nzima inazunguka.


"Mimi!!!!..eeeee!!.. naniiii!!.. nime...nime.....!!" Nomani akiwa kachanganyikiwa huku anababaika kujibu, alibebwa juu kwa juu na mjeda mpaka nje ya kambi.


"Dogo usije fanya makosa kama uliyo fanya leo utakuja kuolewa sawa eeee!?"hayo yalikuwa maneno ya mjeda yule baada ya hapo alimuacha Nomani pale pale.

Siku hiyo Nomani aliona kama haiishi hivi yaani alikuwa anatetemeka haswa, kijana Nomani alienda kutulia kwenye mtaro, yaani alikaa ndani ya mtaro mpaka kulipo anza kupambazuka.


Kulipo kucha tu Nomani alitembea Mpaka kwenye kimto ambacho kilikuwa kimekatiza ndani ya mji huo, basi kijana alioga vizuri na kufua nguo zake, bila hata sabuni.

Noman alizivaa nguo zake zikiwa mbichi vile vile na kuingia mtaani, ila tayari mtaani watu walikuwa wametegwa kila kona kwa ajili ya kumsaka.


Kitendo Cha Nomani kuingia tu mtaaani alianza kuandamwa.


Nomani akiwa anatembea hana hili wala lile alishagaa kuna mtu anamuita.


"Dogo vipi unaweza kazi ya kufagia fagia, kuna Banda la kuku hivi nataka ukanisaidie kufagia ntakupatia pesa!" Baada ya mtu yule kumuita hayo ndo maneno ambayo Nomani aliambiwa, basi kijana Nomani Meno yote yalimtoka baada ya kupata dili.


Basi Nomani alibebwa kwenye pikipiki ambayo yule jamaa alikuwa nayo.

Mungu Siku zote ana namna nyingi za kuokoa watu wake,  Nomani akiwa kabebwa kwenye pikipiki Mara kuna jamaa alimuita yule jamaa ambaye alikuwa kampa Nomani dili.

Baada ya yule bwana kuitwa alipunguza mwendo wa pikipiki ili kusikiliza kaitiwa nini.


"Oya dogo Mau, Boss Dosomi yuko wapi mbona hakamatiki kwenye Simu Sasa!?" Hayo yalikuwa maneno ya yule jamaa aliye simamisha pikipiki, na maneno hayo yalifanya Nomani ashituke pale pale na machale kumcheza, yaani alipo gundua tu jina la Dosomi limetajwa aligundua hakuna cha dili wala Bibi yake dili.


Nomani aliruka kwenye ile pikipiki ikiwa inatembea taratibu taratibu, baada ya hapo aliingia uchochoroni na kupotea kabisa eneo lile.

Nomani aligundua anasakamwa pale mjini kila kona, maana kila sehemu anayo pita alihisi kuna watu wanamfuatilia.


Masaa yalisogea hatimaye ulifika usiku, Nomani alijikuta anenda kulala stendi, sehemu ya abilia kujipimzisha, maana alikuwa hana pa kwenda.

Nomani akiwa pale stendi katulia, alisikia pembeni kuna majamaa wanazungumza maswala ya kwenda kwenye vibarua kunako mashamba ya mpunga huko vijijini.


"Kwa hiyo mwanangu huyo boss anatafuta watu wangapi!?" 


"Watu kama kumi hivi anatafuta, tayari washapatikana kama Saba, hao watatu ndo kazi kuwapata!"


"Daaa!! Mwanangu uhakika lakini pesa ipo isije ikawa miyeyusho!?"


"Pesa ipo babu mchawi wewe tu!!" 


"Basi mwanangu mwambie boss kaongezeka mwingine, si umesema maswala ya nauli juu yake!"

Hayo ni mazungumzo ambayo Nomani akiwa pale alishawishika kusogea kuyasikiliza, baada ya kugundua kuna dili la kibarua, Nomani bila kujari ni kazi za aina gani aliamua kuomba naye awe miongoni.

Japo kuwa alikuwa mdogo kiumri ila kutokana na watu wa kwenda huko kuwa haba yule jamaa alimkubalia.

Basi Nomani alitulia pale stendi mpaka asubuhi huku akiwa anajihisi homa kali,   asubuhi ile yule jamaa alikuja kumchukua Nomani kumpeleka kwa boss.

Baada ya hapo vijana wote walio patikana na kukubali kwenda kijijini kwenye mashamba ya mpunga walitafutiwa usafiri na kuanza safari ya kwenda huko.


Nomani aliogopa kusema kwamba anaumwa kwa sababu aliogopa kwamba ataambiwa yeye asiende, na ukichukulia tayari pale mjini alikuwa anaona dalili za kufa kufa.

Safari ile ilikuwa ndefu muno, na kijana Nomani homa ilikuwa inazidi kuwa kali, hatimaye alianza kutetemeka ndani ya Gari huku akiwa anatoa jasho jingi Muno.


"Oya mkubwa mbona kama huyu dogo anaumwa!!" Basi kuna jamaa alikuwa anaitwa Ommary baada ya kuona Nomani anatoa jasho aliamua kumwambia yule jamaa ambaye alikuwa kawatafuta, ambaye ndo alikuwa kama wakala wa boss.

Nomani aliulizwa lakini aligoma kwamba haumwi.


Ila vijana wengi ambao walikuwa kwenye msafara ule walikuwa washagundua kwamba dogo anaumwa ila anaficha.

Safari iliendelea hatimaye ilifika mida ya jioni huku wakiwa bado hawajafika huko waliko kuwa wanaenda, wakiwa bado wanaendelea na safari Nomani alizidiwa na homa hatimaye alizimia ndani ya Gari.


Ule msafara baada ya kufika kwenye moja ya kijiji ambacho kilikuwa kimechangamka kidogo waliuliza zahanati ambayo ipo hapo kijijini, na kweli walielekezwa.


"Huyu kijana ni mgonjwa muno, alafu kaishiwa damu hapa sisi tutampatia huduma ya kwanza tu, itabidi mfanye mpango mumpeleke hospital kubwa" hayo yalikuwa ni maneno ambayo akina Ommary walipewa na mtabibu wa ile zahanati.

Yule jamaa ambaye ndo alikuwa boss was msafara aliona Sasa ule ni msara anaubeba, na pia aliona atatukanwa na boss kumchukua mtu mgonjwa.


Wale vijana waliamua kumtelekeza Nomani pale pale zahanati akiwa anapata huduma ya kwanza.

Nomani alisaidiwa baadhi ya huduma za kwanza, ila mtu wa kumpeleka hospital hakuwepo tena ilibidi kijana akae pale pale zahanati.


Usiku wa manane Nomani ndo alizinduka, na hakuelewa yupo Sehemu gani, kijana huyo kichwa kilikuwa kinauma muno.

Noman ilibidi kwanza atulie pale kitandani mpaka palikucha, hapo ndipo alipo muona Mama mtu mzima akiwa anaingia mule ndani.


"Afadhari umezinduka, vipi mbona ndugu zako wamekukimbia kwani nyumbani wapi!?" Baada ya Mama yule ambaye alikuwa mtabibu kuingia mule ndani alimuuliza Nomani Maswali ambayo Nomani hakujua ajibu vipi.


"Kwa hiyo kijana nakuuliza wewe umekaa kimya siyo!? Basi naomba uondoke Mimi Sina msaada zaidi, mtu mwenyewe hujalipia hata shilingi kumi" Mama yule baada ya kuona Nomani yupo kimya aliamua kuanza kutukana, na alimtimua Nomani pale zahanati.


Noman akiwa na njaa kali,huku hali yake ikiwa siyo nzuri aliondoka pale zahanati na kuanza kudhurura huku na kule.

Nomani alijaribu kuuliza sehemu wanayo lima mpunga maeneo hayo akiamini kwamba akienda ataenda kuwakuta kina Ommary, ila aliambiwa mpunga unako limwa ni mbali muno kutokea pale, yaani unatembea karibia masaa kumi.


Nomani Katika tembea tembea alijikuta anaenda kuomba msaada kwa Mzee mmoja ambaye alikuwa anaitwa Mzee Makanja, na Mzee huyo hapo kijijini alisifika kwa ufugaji wa mifugo kama mbuzi na kondoo, yaani alikuwa na mbuzi Zaid ya 200 na kondoo wa kutosha.

Nomani baada ya kufika pale kwa hari ambayo alikuwa nayo alishindwa hata kujielezea vizuri, ila ni neno tu naomba msaada ndo lililo sikika kutoka kwa Nomani.


Mzee huyo alikuwa anaishi na mke wake pamoja na mjukuu wao, basi Nomani alikaribishwa na alipewa chakula, ambapo ulikuwa ugari wa mhogo.

Nomani alikula kama haji kula tena, baada ya Nomani kupata chakula angalau hata nguvu zilimjia na alikuwa ananyosha maelezo vizuri.


Basi Nomani alitoa maelezo ambayo aliona yatamsaidia kupata msaada, na kweli maelezo yake yalifanya Nomani akaribishwe katika familia ile.


Maisha mapya ya Nomani yalianza katika kijiji kile, Nomani akiwa kama mchungaji wa mbuzi na kondoo kwa yule Mzee.

Mwanzo Nomani aliona maisha magumu kutokana na mazingira ya pale Kijijini, ila kadri siku zilivyo zidi kusogea Nomani alikuwa anazoea mazingira taratibu.

Ilipita miezi kama Saba Nomani akiwa ashazoea mazingira, na Nomani alikuwa anaitwa jina la utani mchunga mbuzi, na hiyo ilitokana na watu kuamini kwamba Nomani alikuja pale kijijini kwa ajili ya kibarua Cha kuchunga mbuzi.

Nomani wala hakujali aliona ni sawa tu, Nomani alikuwa anafanya kazi ya kuchunga mbuzi na kondoo huku mshahara wake ukiwa ni chakula na kulala tu.


Maisha ya Nomani yalizidi kuwa ya papatupapatu kutokana na kwamba alianza kupakaziwa kesi za wizi pale kijijini, yaani kila tukio la wizi linalo tokea pale kijijini Nomani alijikuta anahusishwa.

Yaani kesi kumhusu Nomani zilikuwa haziishi kwenye ofisi ya Kijiji yaani kila Siku Nomani alikuwa anaitwa kwenye ofisi za kijiji anapigwa fimbo za kutosha kama onyo.

Nomani pamoja na yote aliona ni poa tu, yeye aliendelea na kazi yake ya kuchunga mbuzi na kondoo pale kwa Mzee Makanja.


Baada ya miezi kama Sita hivi kupita huku misuko suko kwa kijana Nomani ikiwa haiishi, kuna mkasa wa wizi ulijitokeza, Mzee Makanja aliibiwa mbuzi wake kama kumi na kondoo wawili na ailiibiwa usiku.

Kwakuwa Nomani ndo alikuwa mchungaji wa ile mifugo pale nyumbani basi kesi yote ilimdondokea Nomani kwamba ndo kaiba.


"Nasemaje Awamu hii sikuachi kijana, Mimi miaka yote sijawahi ibiwa yaani Mara baada ya wewe kuwepo hapa kwangu ndo nimeibiwa, yaani nina uhakika ni wewe umeiba, hata kama siyo wewe basi umeshirikiana na wezi" Mzee Makanja alikuwa anaongea kwa ukali mpaka mate yalikuwa yanamtoka.

Nomani alikamatwa na kupelekwa kwenye ofisi za kijiji huku watu wakiwa wamejazana.


"Achomwe moto huyo!!"

"Tumpeleke mto wa adhabu huyo"

"Haiwezekani huyo dogo mwizi, kwanini yeye Mara baada ya kuja wizi ndo umeongezeka hapa Kijijini"

"Apelekwe mtoni, hatutaki maelezo" 


Hizo zilikuwa ni kauli mbali mbali kutoka kwa watu ambao Walikuwa wamejazana pale kwenye ofisi za kijiji, na kila mtu alikuwa anaamini kijana Nomani ni mwizi, au kama siyo yeye basi anakula madili na wezi.


Kwakuwa ofisi ya kijiji ilikuwa imeyachoka matatizo na kesi za Nomani pale ofisini, Awamu hii maamuzi waliyo yafanya waliamua kwamba Nomani apelekwe mtoni, yaani mto huo ulikuwa unaitwa mto wa adhabu.

Na waharifu wote walio shindikana Walikuwa wanapelekwa huko, ukisha fikishwa huko unafungwa jiwe kubwa na zito mgongoni, baada ya hapo unadumbukizwa kwenye huo mto ambao ulikuwa unatisha kweli kweli, na ulikuwa na kina kirefu haswa.


Yaani ndani ya mto huo hakuna mtu ambaye alikuwa kadumbukizwa na akapona, na ndo huo mto iliamuliwa Nomani apelekwe baada ya kuona matukio ya wizi yamezidi, na mhusika akionekana ni kijana Nomani.

Wanakijiji wakiwa wamechafukwa, huku wameandamana walimbeba Nomani juu kwa juu na kuanza kushuka mabondeni ambapo ndo huo mto ulikuwepo.

Nomani alikuwa analia tu huku akiwa haelewi hata anako pelekwa.


Safari ile ilienda kuishia kwenye mto mkubwa ambao ulikuwa una kina kirefu haswa.

Nomani baada ya kuona mto ule kwanza kwa uoga tu alijikojolea pale pale, maana hata kuogelea tu mtoto wa watu alikuwa hajui.


"Oya fanyeni haraka tafuteni jiwe kubwa tumfunge tumalize kazi, maana mvua hii inakuja" jamaa Mmoja ambaye alionekana kuwa na roho mbaya kweli kweli aliongea kwa mizuka, hapo ndipo uoga ulizidi kuwa mkubwa kwa kijana Nomani baada ya kugundua kwamba anafungwa jiwe zito ndo anatupiwa kwenye maji.

Basi jiwe kubwa lilitafutwa na pia kamba maarumu kwa ajili ya kufungia zililetwa,muda huo kimvua kilikuwa kimeanza kupiga kwa mbali.


"Oya fanyeni haraka mvua inakuja hii jamani!" Basi kuna jamaa mwingne aliongea kuharakisha Mambo, Nomani alijikuta anajikatia tamaa picha ya Baba yake ikiwa inamjia kichwani, kijana alijikuta anafumba macho huku akiwa tayari kwa kile kinacho enda kutokea.


Je ndo mwisho wa Nomani!? Au kuna muujiza utajitokeza??


Tukutane sehemu 9


 

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text