YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭
Mtunzi: Mwaki Ze Done
Sehemu ya 10.
"Sasa uncle Ole, vipi kuhus vifo vya wazazi wangu wewe ulisema Mama na Uncle Farhan na Baba yake na Victor ndo wahusika, itakuwaje nao si naweza kuwafungulia kesi!?" Noman alikuwa anazidi kupekenyua mambo bila kugundua kama kuna mtu anasikiliza nje.
"Nomani sikiliza nishakwambia hiyo iache ibaki kuwa Siri kama Siri zingine, lasivyo utaishia pabaya, Mimi kukaa kimya siyo Kwamba mjinga, wewe ukifika kwa huyo Mama usimwelezee kuhusu Namna vifo vilivyo tokea, bali zungumzia kuhusu haki yako tu, ya kupata Mali" olenashi alizidi kufunguka.
"Sasa uncle olenashi maana yake ipi Sasa, yaani watu wameua wazazi Wangu wapo wanatumia Mali za wazazi Wangu alafu unasema nisilizungumzie hilo swala, Mimi siwezi uncle lazima hii kesi ifike mahakamani!"
"Nomani mbona kichwa kigumu hivyo wewe, huko mahakamani wewe unao ushahidi wa kupeleka!?"
"Uncle Nomani si Shahid utakuwa wewe, maana wewe una ushahidi kuhusu kifo Cha Mama yangu namna alivyo kufa!" Nomani alizidi kubwatuka, ila olenashi alimwambia ile maada iishie pale pale na asije akarudia tena.
Muda huo bwana Farhan kijasho kilikuwa kinamtoka, alikuwa kasikia mazungumzo yote na kugundua Mambo yote.
"Duuuuu!! Huyu mpuuzi tunaishi naye hapa miaka yote kumbe anajua Siri zetu, alafu ushahidi gani ambao anao huyu mpuuzi, hapa bila kufanya Jambo mambo yanaweza kuwa magumu" Farhan hayo yalikuwa ni mawazo ambayo alikuwa anajiwazia huku akiwa anarudi ndani haraka haraka kwenda kumsimulia, Mama Samir.
Baada ya Mama Samir kusimuliwa kila kitu kilicho kuwa kinazungumzwa mwanamke alichanganyikiwa haswa, yaani alikuwa anaona anaenda kuumbuka.
"Heeee!! Farhan kama Nomani kaambiwa aende kwa yule kidudu mtu Mambo yanaweza kuwa magumu, yaani yule mwanamke ana gubu hatari mtaa mzima utajua, hapa inabidi tufanye kitu" Mama Samir alikuwa anakuna kichwa huku akiwa anaongea.
"Sasa kipenzi hapa tunafanyaje, maana inaonekana naye huyu olenashi kuna ushahidi anao kuhusu kifo Cha Mama Nomani, na hatuwezi jua ni ushahidi gani huwenda hata ni video" Farhan naye alikuwa na wasiwasi wake, yaani matumbo yalikuwa joto haswa.
"Dear! Sikiliza kwanza inabidi tufanye Jambo, Mali zote tunahamishia kwa Jina la Samir, alafu baada ya hapo tutajua kipi kinafuata, alafu mpigie Simu Dosomi aje na vijana wake tutengeneze mpango kazi wa kukabiliana na hili" hayo yalikuwa ni maneno ya Mama Samir, ambayo yalifanya Farhan atabasamu tu.
Upande wa huku kwa Nomani alikuwa hataki kupoteza hata nukta, baada ya kupewa maelezo na olenashi moja kwa moja alielekea kwa Mama ambaye alikuwa ni rafiki wa Baba yake enzi hizo.
Mama huyo alikuwa ni Mmiliki wa restaurant moja maarafu pale mjini, na wengi walikuwa wanamuita Mama chibonge, na hiyo ilikuwa inatokana na unene wake ila Jina lake kamili alikuwa anaitwa Helena.
Mama huyo bahati mbaya alikuwa hajabahatika kupata Mtoto maisha yake yote na pia alikuwa hana ndugu yeyote pale mjini zaidi ya marafiki na majamaa, na Mama huyo alikuwa kakulia huko vijijini maisha yake yote akiwa kalelewa na Bibi yake tu.
Nomani alifika kwa Mama huyo, alimkuta ndo anataka kuondoka.
"Fekon mwenyewe! Eheee vipi kijana mbona umepauka hivyo kulikoni!?" Basi Mama yule chibonge baada ya kumuona Nomani aliongea kwa kuchangamka.
Noman alijikuta machozi yanaanza kumlenga lenga baada ya kutajiwa Jina la Baba yake.
Basi ilibidi waingie ndani kwanza ili Nomani asimulie kitu kilicho mleta.
Noman alisimulia kila nukta, yaani hakuacha hata neno, mpaka kuhusu vifo vya wazazi wake kama alivyo simuliwa na olenashi napo alisimulia.
"Heeeee huyu mwanamke kumbe shetani hivi, Sasa sikiliza hapa umefika mbona watataja yote, yaani wanataka wadhurumu Mali za mshikaji Wangu, aaaaaaa!!! hiyo haipo" Mama yule baada ya kupewa ile stori kwanza alibaki anatikisa tu kichwa, pale pale alichukua Simu na kumutwangia rafiki yake ambaye alikuwa mwanasheria.
"Sasa kijana wewe bakia hapa hapa Nyumbani, kuna mdada wa kazi kaenda sokoni Mara moja akikukuta mwambie Mimi ni shangazi sawa ngoja kuna maswala naenda kufuatilia" Mama chibonge aliongea na kuondoka kwa mizuka.
Baada ya kutoka pale kwake safari ya Mama huyo ilikuwa ni kwa Mama Samir, yaani Mama huyo alikuwa siyo mtu wa kupepesa mambo, wala kusubiri kesho.
Alienda kumchana makavu Mama Samir laivu pale kwake.
"Sikiliza we mwanamke kama unataka haya mambo yasifike mbali, basi mkabidhi yule kijana haki yake, na kama unaona kazi basi mgawie hata nusu ya Mali za baba yake! Lasivyo utakosa kila kitu Maana hii kesi itafika mpaka mahakama za kimataifa" Mama chibonge baada ya kufika pale nyumbani na kumkuta Mama Samir akiwa na Farhan alitia mkwara wa maana.
Muda huo huo bwana Dosomi na vijana wake walifika pale, maana walikuwa wameitwa ili wajadili kwamba inakuwaje.
Mama chibonge baada ya kumuona Dosomi hapo ndo vitisho vilizidi, yaani mwanamke alikuwa anapayuka kupita kiasi.
"Nawapatia Siku mbili, mumrudishie yule kijana Mali zake au kesi hii iende mahakamani na ulimwengu mzima ujue madhambi mliyo fanya, na niwaambie tu ushahidi wote upo mkononi, kwa hiyo machaguo ni yenu!" Mama chibonge alitia mkwara na kuondoka pale Nyumbani kwa mbwembwe.
"Dosomi tumalizane naye kabla hajafika mbali! Maana hili lishakuwa balaaa!!" Baada ya Mama bonge kuondoka, Mama Samir alitoa maamuzi ya haraka haraka.
"Duuuuu sikilizeni, Mimi Helena namjua vizuri kuliko nyie, hata kijijini aliko tokea napajua vyema kwa sababu nimefika Mara nyingi tu enzi za uhai wa Mr Fekon, huyu mwanamke siyo mwepesi kama unavyo dhani, Bibi yake huyu ni mchawi wa wachawi,tukifanya upuuzi wowote kwa mjukuu wake!! Haaaaa hatumalizi hata wiki, hilo nina uhakika nalo na ushahidi kumhusu yule Bibi ninao anaitwa Bi Mwantumu maana kuna kazi amewahi kutusaidia, kikubwa hapa Cha kufanya inabidi tuongee na huyu Mama kiungwana na ikiwezekana kumpooza tumpooze!" Bwana Dosomi baada ya maamuzi ya kukurupuka ya Mama Samir aliamua kuelezea kiufupi kumhusu Mama chibonge.
Basi kwa umoja wao walijadili Jambo la kufanya.
Siku hiyo ilipita huku kwa upande wa Nomani akiwa kalala kwa Mama bonge tena kwa kujiachia na raha mstarehe.
Ikiwa ni Siku mpya majira ya saa nne Mama bonge alipigiwa Simu na bwana Dosomi kwamba wakutane.
Na kweli Mama bonge alienda sehemu husika, alipo fika alikutana na sura ya Mama Samir, Farhan na Dosomi mwenyewe.
Siku zote pesa hubadili wema wa mtu, pesa huondoa utu, pesa inaweza fanya mlima ukawa bahari, Mama bonge baada ya kufika pale alikutana na pesa zimejaa brifikesi, kwa maisha yake ndo ilikuwa Mara ya kwanza kuona pesa nyingi kwa pamoja vile.
Kwanza alibaki akitabasamu na kucheka cheka tu baada ya kuona zile pesa.
Mama Samir alitoa maelezo na msaada ambao wanahitaji, basi Mama bonge bila hiyana huku udenda ukiwa unamtoka alikubali kuungana na wabaya wale.
"Sasa Mama bonge umesema Nomani yupo kwako, fanya mpango utuletee nyumbani kwa Namna yoyote, maana tunataka tuwaunganishe na mlinzi wetu pale nyumbani" hayo yalikuwa ni maombi mingine ya Mama Samir.
"Kuhusu hilo msijali, ila kitu ninacho waomba tumia plani yoyote ile ila Nomani msimuue" Mama bonge aliongea,basi walikubaliana wote kwa pamoja.
Dosomi na wenzake waliondoka pale huku vichwa vikiwa vinawasha, maana wao lengo lao lilikuwa ni kumuua Nomani, ila Mama bonge alikuwa kaomba kwamba wasimuue.
Basi Dosomi ilibidi awapatie mpango mwingine kina Farhan, na wote walikubaliana na huo mpango.
Ilifika jioni, pale nyumbani kwa Mama Samir, olenashi akiwa getini aliitwa na Boss wake ndani.
Mlinzi yule akiwa hana wasiwasi alizama mpaka ndani, basi baada ya kuingia alikutana na sura zimenuna kuliko kawaida.
"Olenashi ebu naomba unipe ushahidi wote ulio nao kuhusu mauaji ya Mama Nomani, na kama huna uniambie umeficha wapi, ukifanya hivyo pesa hizo hapo tunakupatia uondoke nazo uende nazo mbali kabisa" Mama Samir akiwa na Sura ya ukauzu aliongea maneno ambayo yalifanya Olenashi atumbue macho, yaani alikuwa haamini kama Siri zake zishagundulika.
Olenashi alikosea stepu, na tamaa yake na pesa ilimponza, yaani alijikuta kaelezea ukweli wote, na pia alielezea kwamba yeye hana ushahidi wowote.
"Ahaaaa vizuri, kwa hiyo olenashi unamanisha huna ushahidi ila wewe ndo shahidi, kwa mantiki hiyo tukikuua wewe tunakuwa tumepoteza ushahidi!?"Mama Samir akiwa anatabasamu aliuliza swali ambalo lilifanya olenashi apate kigugumizi.
Na kweli hata hazikupita sekunde nyingi Dosomi alichukua bastola na kumfyatulia Olenashi risasi ya kichwa, yaani pale pale mlinzi yule alidondoka chini na kufariki pale pale.
Pale nyumbani alikuwepo mdada wa kazi ambaye alikuwa anamsaidia Mama Samir, kwa kuwa yule mdada kuna Siri kadhaa alikuwa naye kazisikia, ilibidi naye aunganishwe na Olenashi, naye alipigwa risasi ya kichwa.
"Sasa ni muda wa kukamilisha ule mpango wetu, Dosomi mpigie Mama bonge atuletee mtu wetu ili tutimize mpango wetu!, Alafu Farhan na wewe hakikisha ile dawa inakuwa tayari, haitakiwa kukosea stepu hata moja, maana zaidi ya hapo tutaingia kwenye matatizo." Mama Samir akiwa anatabasamu aliongea.
Je ni mpango gani hawa watu wanataka kuufanya!? Hadithi ndo imeanza Sasa kunoga usikose sehemu zijazo.
Tukutane sehemu ya 11
0 comments:
Post a Comment