Tuesday, December 5, 2023

YATIMA GEREZANI 9

 



YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭


Mtunzi: Mwaki Ze Done


Sehemu ya 9.


"Oya fanyeni haraka mvua inakuja hii jamani!" Basi kuna jamaa mwingne aliongea kuharakisha Mambo, Nomani alijikuta anajikatia tamaa picha ya Baba yake ikiwa inamjia kichwani, kijana alijikuta anafumba macho huku akiwa tayari kwa kile kinacho enda kutokea.

Nomani alifungwa jiwe mgongoni bila hata kuonewa huruma, baada ya hapo kijana alitupwa kwenye ule mto.

Sekunde ile ile anatupwa kwenye maji kuna dogo alifika pale akiwa anahema akionekana ni mtu aliye kuwa anakimbia.


"Jamani wale mbuzi wa Mzee Makanja wamekamatwa kijiji Cha pili, na wezi wametaja kwamba Lumi ndo aliye wauzia usiku ila kwa bei ya hasara!" Hayo yalikuwa ni maelezo ambayo yalifanya kila Mmoja aliyepo pale ashike kichwa na kutazama mtoni, maana iligundulika mwizi siyo Nomani bali ni yule mjukuu wa Mzee makanja.


"Duuuuu!! Ila siyo mbaya! Kwasababu hata hivyo huyu dogo naye alikuwa mwizi!" Basi kuna jamaa na roho zake mbaya baada ya kuona watu wameshika vichwa aliamua kuwatoa wasiwasi na kuonekana kama walicho kifanya siyo kosa.

Mvua kubwa ilianza kunyesha, kila mtu aliondoka kimya kimya pale mtoni huku wengine roho zao zikiwa zinauma, wengine wakiwa wanaona poa tu.


Kuna jamaa alijikuta tu huruma inamuingia na imani fulani inamjia, wakati mvua kubwa inapiga, watu wote wakiwa wanakimbia yeye badala yake alidumbukia ndani ya ule mto na kuzama kwa ajili ya kumtafuta kijana Nomani kama bado yupo hai.

Bahati nzuri ule mto maji yalikuwa hayatembei kwa kasi hivyo,kwa hiyo alipo Zama alikuta mwili wa kijana Nomani ukiwa ndo unapambania pumuzi ya mwisho.


Kijana yule alipambana kufungua lile jiwe haraka haraka, kwa kuwa alikuwa anajua kuogelea baada ya kufungua jiwe aliibuka na Nomani juu ya maji na kumtoa mpaka nje.

Nomani tumbo lilikuwa limejaa kama linataka kupasuka, yaani alikuwa kameza maji ya kutosha.


Yule kijana alifanya kila jitihada kumsaidia Nomani na yale maji yote aliyo meza Nomani yalifanikiwa kutoka, ila Nomani bado alikuwa hajazinduka wala kuonesha dalili za kuzinduka.


Kijana yule akiwa anazidi kuparangana pale kwa ajili ya kuokoa uhai wa Nomani, aliona kuna bonge la nyoka anakatiza yale maeneo, yaani alikuwa ni nyoka mkubwa hajawahi ona.

Kutokana na uoga ambao alikuwa nao yule kijana pindi linapo kuja swala na wadudu haswa nyoka, yaani alikimbia kama haji kukimbia tena, alimsahau Nomani pale pale.


Mvua kubwa ilizidi kunyesha huku kigiza kikiwa kinaanza, basi yule nyoka alipita eneo lile na kupotelea zake kwenye maji.

Mvua ile ilipiga mpaka saa mbili usiku, Nomani ndo muda alio zinduka huku mwili wake ukiwa na baridi haswa.


Kwanza Nomani baada ya kuzinduka alikuwa hajielewi kabisa, yaani akili ni kama zilikuwa zimeruka alikuwa haelewi kipi ni kipi.

Nomani alijitahidi kusimama, huku akiwa anatetemeka, baada ya hapo alianza kutembea kuelekea hata asiko kujua


Nomani alikuwa anatembea huku akiwa anapepesuka, baridi kali ilikuwa inamtwanga haswa, kukiwa na giza Nomani akiwa haelewi hata anako elekea alizidi kusonga mbele.

Noman alitembea umbali mrefu muno bila kuona msaada wowote, Zaid zaidi Nomani alikuwaa anasikia sauti za bundi na wanyama wa ajabu kule porini.


Baada ya Nomani kuona haelewi hata ataishia wapi aliamua kukaa chini ya mti usiku ule, yaani akili ya kijana Nomani bado ilikuwa haijakaa vyema na kukumbuka kipi kimetokea.

Homa na baridi kali vikiwa vinatalii kwenye mwili wa Nomani, ila Nomani alikaa pale chini ya mti kwa kuvumilia mpaka kulikucha.


Walau kijua kilipo anza kuwaka hapo Nomani ndipo alipo pata nguvu na akili zilianza kumrejea taratibu taratibu.


"Heeee!! Kwamba ndo nishakufa ama!? Huku nipo wapi Sasa!!" Baada ya Nomani kukumbuka kilicho mtokea Mara ya mwisho alianza kujishangaa na kujiuliza bila kupata majibu, yaani alikuwa anaona kama maajabu.

Nomani alikuwa yupo Katikati ya pori zito muno, yaani katika harakati zake za kuchunga mbuzi pale kijijini alikuwa hajawahi fika maeneo hayo ya porini.


Nomani alipiga Mahesabu na kuangalia upande upi kunaweza kuwa na msaada, basi aliona aelekee kule jua linako elekea.

Nomani alianza safari akiwa mdogo mdogo, ila kadri anavyo zidi kusonga mbele aligundua ndo anazidi kuzama ndani ya msitu kabisa, ila kijana Nomani aliona ni Bora asonge mbele kuliko kurudi nyuma.

Nomani alitembea tokea asubuhi mpaka jioni kigiza kikiwa kinaanza lakini bado alikuwa hajatoboa ule msitu, ila bado hakukata tamaa ya kutembea.

Mpaka inafika saa sita za usiku Nomani akiwa hoi alikuwa bado hajatoboa, hapo ilibidi atulizane na kukaa sehemu.


Kulikucha tena, Nomani aliendelea na safari huku mwili wake ukiwa umenyong'onyea muno kutokana na njaa kali ambayo ilikuwa inamchapa.


Nomani baada ya kutembea muno hatimaye alianza kuona matumaini, baada ya kuona mbuga kubwa huku mashamba ya mpunga yakiwa yameongozana na mwisho wake hauonekani.

Nomani alianza kukatiza mashamba yale ya mpunga akiwa na imani kwamba ataona watu maeneo yale.


Kama tujuavyo maeneo ya mbugani yanakuwa na maji maji kila sehemu, basi Nomani alijikuta anatembea huku akiwa anadondoka na kuinuka, yaani alikuwa anakatiza majaruba ya mpunga  mpaka anatamani kupaa, maana mashamba yale yalikuwa makubwa muno.

Hatimaye Nomani alianza kuona vimoshi vikiwa vinaonekana kwa mbali huku akiwa anaona mahema kwa mbali, hapo Nomani alipata nguvu na kuamini anaenda kukutana na watu, japo kuwa Nomani bado alikuwa haamini kama yupo kwenye dunia ya kawaida.


Nomani alipata ngvu ya kutembea zaidi baada ya kuona dalili ya kupata msaada, Nomani alifika kwenye yale mahema na alisikia watu wakiwa wanacheka ndani ya mahema yale.

Nomani alijikohoresha kwa nje na kubisha hodi huku akiwa na presha maana alikuwa bado anahisi yupo dunia ya tofauti kabisa.


Basi alitoa jamaa mmoja akiwa kavua shati huku ana kitambi cha pombe


"Oya dogo vipi, umetokea wapi mbona sijawahi kukuona hapa kambini!?" Yule mwanaume akiwa na Sura ya ukauzu aliuliza.

Basi Nomani alitoa maelezo kwa ufupi Kwamba kapotea anaomba msaada.


"Oya Athumani hawa ndo madogo ambao watakuwa wanatuibia vitu vyetu kila Siku hapa kambini!" Nomani akiwa anajitetea kuna jamaa mwingne alikuja huku akiwa na Sura ya ukauza zaidi.

Nomani kwanza ilibidi akarishwe chini na kuanza kuulizwa huku akiwa anakula makofi.

Nomani alijitahidi kutoa maelezo, ila kutokana na maelezo yake na sehemu ambayo alikuwa anaonesha kwamba katokea hakuna ambaye aliona ni ukweli.


"Dogo wewe mwizi, unawezaje kutokea kwenye ule msitu wakati tunajua kwenye ule msitu hakuna watu wanao ishi, wewe umetokea kule kama nani!?" Nomani alikuwa kabanwa na maswali ambayo alishindwa kujibu mwishowe aliamua akae tu kimya.

Basi wale jamaa walimtandika Nomani sitiki za kutosha wakiwa wanaamini ni mwizi, maana eneo hilo vijana kutokea kijiji Cha jirani walikuwa wanakuja kuiba muno, hasa pindi wale majamaa wanapo kuwa mashambani, maana kipindi hicho kilikuwa Cha palizi ya mpunga.


Nomani baada ya kutimuliwa pale kambini alianza kujisogeza taratibu taratibu kwenye kijiji ambacho kilikuwa karibu na eneo hilo na tayari ilikuwa jioni.

Nomani alienda kuishia kwenye nyumba ya Bibi mmoja hivi, na Nomani alikuwa hoi huku mwili ukiwa umelegea, na Nomani alizimia pale pale upenuni.


Bahati nzuri yule Bibi mwenye mji wake naye ndo alikuwa anarudi tokea kwenye pombe, baada ya kukuta mtu pale nje alianza kumumwagia maji.

Nomani alizinduka lakini mwili ulikuwa hauna nguvu yaani alikuwa kalegea anashindwa hata kuongea.

Yule Bibi alikoroga uji wa bila hata sukari na kuanza kumnywesha Nomani.


Hakika chakula ni mhimu kwa binadamu, yaani baada ya Nomani kupiga bakuri zima la uji baada ya lisaa kupita hata sauti ilianza kusikika.

Nomani alimuelezea yule Bibi stori kwa ufupi kumhsu na aliomba msaada akae pale walau kwa muda.


Wakati Nomani anatoa maelezo yote hayo kujieleza yule Bibi naye alionekana ana jambo lake, maana ujio wa Nomani pale ulifanya Sura yake kuwa ya furaha zaidi.

Hakika Nomani aliamini yule Bibi ni mkarimu maana alikuwa kachangamkiwa haswa yaani alikarimiwa muno jioni ile, alipikiwa magimbi, akapewa na maziwa ya mgando, yaani Nomani alijiona kama anakula Pizza ndani ya paradiso.

Masaa yalisogea, muda wa kulala Nomani alioneshwa sehemu ya kulala na alipewa shuka zito kabisa kwa ajili ya kustili baridi, hakika Nomani alijisikia vyema.

Usiku wa manane yule Bibi aliamuka na  kuvaa kaniki nyeusi huku akionekana kabisa ana jambo lake, kwa muonekano na ishara tu ambazo Bibi yule alikuwa anazifanya alionekana ni mwanga na mchawi.


Yule Bibi alielekea kwenye chumba ambacho Nomani alikuwa kalala kwa usiku huo, Bibi yule alifanya anacho fanya ishara za hapa na pale, alimsogelea Nomani huku akiwa kamgusa kichwa, yule Bibi alitamka maneno anayo yajua baada ya hapo alipotea ndani ya chumba kile akiwa na Nomani.

Bibi yule alienda kutua chini ya mti mkubwa ambao ulikuwepo hapo Kijijini, na eneo hilo walionekana wachawi wengi kukusanyika huku wakiwa wanaimba nyimbo zao.


"Jamani ile dhamu Yangu ya kutoa nyama naitizimiza leo, nimewaletea nyama hii hapa!" Yule Bibi akiwa anamuonesha Nomani mbele ya wachawi wenzake aliongea, ila mkubwa wa lile kundi la wachawi alionekana kukasirika muno Mara baada ya maneno ya yule Bibi.


"Bi Mwantumu nadhani umeanza kukizoea chama, yaani unatuletea nyama iliyo chacha, nyama isiyo na radha, sisi tulikwambia tunamtaka mjukuu wako aliyepo mjini hatutaki nyama zilizo chacha!" Hayo yalikuwa ni maneno ya mkubwa wa kile chama, na maneno hayo yalifanya Nomani aponee chupu chupu kuliwa.

Yule Bibi alimrudisha Nomani akiwa mnyonge muno, yaani hakufurahishwa kabisa, na Bibi yule alionekana hayupo tayari kumtoa huyo ambaye alisadikika ni mjuu wake ambaye alikuwa anaishi mjini.


Masaa yalisogea hatimaye palikucha, Nomani aliamuka akiwa na uchovu kama wote, ila asubuhi ile yule Bibi alionekana kuwa tofauti na jana yake usiku, yaani ule ukarimu ulikuwa haupo tena.

Nomani alishangaa yule Bibi kakunja Sura kama anataka kuitia kwenye mfuko, yaani alikuwa hamchangamkii Nomani kama jana yake.


"Kijana ebu kula hayo magimbi uondoke, msaada wangu unaishia hapa!" hayo yalikuwa maneno ya Bibi yule ambayo yalifanya Nomani ashangae, maana Bibi yule alikuwa kabadilika mudi yake gafla.

Kwakuwa hata hivyo Nomani alikuwa kapata pata nguvu kidogo alishukuru kwa ule msaada kidogo alio upata, alikula yale magimbi baada ya hapo alimuaga yule Bibi kwa kushukuru.


Awamu hii akili yote ya Nomani Sasa ilikuwa inawaza kurudi mjini, maana aliona kukaa vijijini ni changamoto kubwa muno, yaani aliona ni bora arudi kupambana mjini.

Pale kijijini kuna magari mengi tu yalikuwa yanafika kwa ajili ya shughuli mbali mbali, kwa sababu eneo hilo lilikuwa linasifika kwa kilimo, haswa Cha mpunga.


Nomani akiwa anahaha Namna ya kurudi mjini, bahati nzuri alikutana na gari aina ya fuso ikiwa imetoka kushusha mifuko ya mbolea pale kijiji, na Nomani aliigundua ile fuso kwamba inatokea kwenye kiwanda Chao, maana marehemu Baba yake Mr Fekon alikuwa anamiliki kiwanda Cha kutengeneza na kusambaza mbolea.


Basi lile fuso likiwa linaondoka kurudi mjini, Nomani alidandia kwa nyuma na kutulia.

Safari ile ilikuwa ndefu muno, yaani ilikuwa ni Zaid ya masaa 15 mpaka kufika mjini.


Kwa Mara nyingine baada ya miaka kama miwili kupita Nomani alirudi mjini, na gari iliingia pale mjini mida ya saa saba za usiku.

Nomani usiku huo alilala chini ya kibanda Cha mbao ambacho kilikuwa kimejengwa pembezoni mwa Barabara kwa ajili ya kuuzia matunda.


Kutokana baridi kali na manyunyu ya mvua ambayo yalikuwa yanadondoka usiku huo Nomani hakupata hata lepe la usingizi, Zaid Zaid alihisi kichwa kinamuuma.

Hatimaye palikucha mpaka asubuhi, watu wakiwa wanapishana kuwahi makazini kutafutia familia zao chochote kitu, Nomani yeye alikuwa anatembea huku mikono ikiwa kichwani, yaani alikuwa kajikatia tamaa kabisa na maisha, na alikuwa tayari kwa lolote lile.


Bahati mbaya kwa Nomani wakati anaranda randa mtaani akiwa haelewi anaelekea wapi, mtu wake na bwana Dosomi alimuona.

Muda huo Nomani kichwani mwake alikuwa anajisemea kwamba liwalo na liwe kitu alicho kifanya alielekea pale pale nyumbani kwao akiwa anataka kwenda kudai haki yake.


Bahati nzuri kama kawaida Kabla hajaingia kule ndani alimkuta olenashi pale getini.

"Nomani mwaka na miezi kadhaa ulikuwa umetoka Mimi nikajua umekubaliana na yote inakuwaje Sasa unarudi? unataka kufa ama!?" Olenashi kama kawaida alimkataza Nomani kwenda kule ndani ila Nomani yeye alikuwa hataki kuelewa.

Basi olenashi aliamua kumvutia Nomani kwenye kibanda chake ili asije akaonwa, maana ilikuwa ni asubuhi na Mama Samir na Farhan bado walikuwa wapo Nyumbani.


Bahati mbaya wakati Olenashi anamvutia Nomani ndani, Mr Farhan ndo alikuwa anatoka ndani, kwa hiyo aliona tu mtu akiingizwa ndani ila hakugundua kama ni Nomani.

Farhan kwanza ilibidi asogee kwenye kibanda kile Cha mlinzi kujua ni mtu gani kaingia na mlinzi mule ndani.


"Nomani sikiliza, hasira hazisaidii ni kweli Mali ni zako, na umedhurumiwa ila huna Cha kufanya, Labda Mimi nikushauri unamjua yule Mama bonge bonge ambaye alikuwa rafiki wa Baba yako?, kwake ni pale bondeni, Sasa nenda kwa huyo atakusaidia kupata haki yako, maana hata hivyo yeye anajuana na wanasheria wengi wakubwa" olenashi alimpa Nomani mawazo, na olenashi alikuwa anafunguka bila kutambua kama nje pana mtu anasikiliza.


"Sasa uncle Ole, vipi kuhusu vifo vya wazazi wangu wewe ulisema Mama na Uncle Farhan na Baba yake na Victor ndo wahusika, itakuwaje nao si naweza kuwafungulia kesi!?" Noman alikuwa anazidi kupekenyua mambo bila kugundua kama kuna mtu anasikiliza nje.


Hapa ndo tunaenda kuanza Sasa mkasa wenyewe unao Sadifu kichwa Cha hii Hadithi,je ni gereza gani linatajwa,usikose sehemu zijazo.


Tukutane sehemu ya 10

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text