Tuesday, December 5, 2023

KICHAA MPELELEZI FINAL

 SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 





Sehemu ya 43,44&45  MWISHO✍️


Nikiwa tayari nimekwishavalia baibui langu na nikabu ambayo iliyonifunika uso wote na kuacha sehemu ya macho🥷 nikajilaza kitandani huku nikiwaza ni kwa namna gani nitachomoka marekani nirejee tanzania bila jeshi la polisi la marekani kunitia nguvuni, wakati naendelea kujadiliana na serikali pamoja na bunge la kichwa changu mara ghafla😳 nikasikia huko nje polisi wakiongea na muhudumu wa vyumba, walimueleza kwamba kuna muhalifu wanamtafuta hivyo wakamuomba CCTV camera 🎥 ambayo ingenasa picha za watu wote waliowasili hotelini hapo, kwa bahati nzuri muhudumu aliwaeleza kwamba CCTV camera iliyokuwa inatumika hotelini hapo imeharibika, basi wakamwambia "basi sawa sio tabu hebu waamshe wateja wako wote tukague chumba hadi chumba" niliposikia kauli hiyo mwili wote ulianza kunitetemeka mpaka utumbo, kwani niljua ni lazima tu nitiwe nguvuni.


Basi nikakaa kimya nikingoja kitakachojiri, niliwasikia wakikagua chumba hadi chumba huku wakiwauliza wateja majina yao na sehemu walipotoka pamoja na kazi zao, waliuliza chumba hadi chumba walipofika kwenye chumba changu wakagonga mlango 😳 hapo nikajidai nimelala na ninakoroma kama paka aliye usingizini😀 wakapiga mpaka simu ya mezani📞 iliyokuwa mule chumbani, simu iliita mda mrefu lakini bado nilizidi kujikausha. "Mh huyu mtu vipi ni usingizi gani huo yani pamoja na kubamiza kote mlango kiasi hichi manusura uvunjike lakini bado yupo usingizini hapana huenda ndiye muhalifu mwenyewe kwani kwenye daftari na mteja wa chumba hichi ameandika jina gani" Askari alimuuloza muhudumu wa vyumba. "Ameandika George Nicholus" muhudumu alijibu. "Na ameandika ametoka wapi? Askari alimuuliza tena muhudumu. " Washngton Dc " muhudumu alimjibu askari kwamba natokea jiji la washton Dc lililopo hapohapo marekani, "Ni sawa lakini  kama ni mwema kwanini ajikaushe asifungue mlango, je alikuwa ni mzungu au ni mwafrica" askari alizidi kumdodosa muhudumu. Swali hilo likawa mwiba kwangu kwani wakati naingia mpaka napewa chumba nilikuwa bado sijavalia yale mavazi tangu ya kujificha yani baiubui na nikabu🥷. "Ni mwafrica na anadai yeye ni mfanyabiashara wa madini" alijibu muhudumu. "Je ni huyu hapa kwenye picha" askari aliendelea kumuuliza muhudumu huku akimuonyeshea picha yangu. "Sina uhakika maana hapa nahudumia watu wengi na kuna vyumba zaidi ya mia mbili ishirini hivyo ni vigumu kukariri kila sura ya mteja anayeingia na kutoka" alisema muhudumu. 


"Sawa kama ni mwafrica tunaomba tuvunje mlango, tutalipa gharama za mlango na ikiwa sio yeye tunayemtafuta pia tutamlipa gharama za usumbufu" alisema askari. Basi sawa" muhudumu alikubaliana nao. Moyoni nikasema "Kishanuka sasa hapa natembeza mkong'oto 👊bila kujali ni nani atapita mbele ya macho yangu" niliongea kimoyomoyo huku nikiwa bado nimejilaza pale kitandani wakati huo mlango wakiendelea kuvunja mlango, mlango ulipofunguka nikajifanya nimekurupuka kitandani mfano wa mtu aliyekuwa anaota ndoto mbaya akashtuka na kupiga kelele. Tena nilipiga kelele kwa kuigiza sauti ya kike😨 "Heee mbona sasa ni mwanamke yupo na kwenye daftari amejiandikisha mwanaume. Aliuliza askari na nilikuwa hodari wa kuigiza sauti ya kike haswa yani Joti wa kutokea Tanzania akasome. "Wewe dada kulikoni umejiandikisha jina la kiume ile hali wewe ni mwanamke" askari alianza na swali hilo.

Mimi nilikuwa na mume wangu tulikuja hapa kuenjoy kama wapenzi ila ameitwa kazini maana yeye ni mfanyabiashara wa madini na yeye ndiye aliyejiandikisha kwenye kitabu" Nilijibu. "Hebu kwanza toa hiyo nikabu yako sisi tunataka tuongee na mtu ambaye tunaona sura yake" alisema askari. "Kaka dini yangu hairuhusu" nilijibu kwa kulegeza sauti. "Dada acha kuleta mambo ya udini kwenye serikali toa nikabu yako haraka sana😔 usituletee udini wako hapa kila mtu ana imani yake lakini tuwapo kwenye mambo ya kiserikali wote tuwamoja na pia wewe unaonekana ni muhalifu tu kwasababu utalalaje na hizo nguo 🤔"


Alisema askari. Kabla hajakaa sawa nilimchopu ngumi👊 ya kidevu, alianguka pembeni haraka nikashika kiti kilichokuwa mule chumbani, nikaanza kuwatembezea wenzanzake kwa kuwatwanga nacho vichwani, yani kila aliyejileta aliambulia kiti cha kichwa, nilipopata tu kaupenyo sikutaka kung'oja nnzi wajae😜 nilichomoka mbio na kuanza kukimbia, baadhi walinikimbiza lakini walishindwa kunipata, asubuhi yake nilienda uwanja wa ndege nilikata pasport ya kusafiria ambayo ilikuwa na jina la kike, nilisafiri mpaka uturuki na huko nilobadili sura yangu na kuwa ni ya mwanaume ambaye ni chatara mwenye asili ya kizungu na africa kisha nikakata pasport tena ya kusafiria na kurudi Tanzania, iliniwia vigumu ndugu za kunielewa lakini sauti pamoja na kuwatambua ndugu wote wa ukoo pamoja na kuwatajia majina yao hadi waliokufa viliwafanya waniamini, hata hivyo nilihama nilipokuwa naishi  kuhamia kijijini kabisa ambapo kwa sasa nimejiwekeza katika biashara mbalimbali ila kiuhalisia natumia sura ambayo sio yangu. Yote yote pia nimejifunza kutokuwakaribisha watu nisiowafahamu vizuri nyumbani kwangu . 


MWISHO SEASON 02!!!


USISAHAU SEASON 3 NDIO Final NA MAPEMA WIKI HI ITATOKA


Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text