YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA ðŸ˜ðŸ˜
Mtunzi: Mwaki Ze Done
Sehemu ya 11.
"Sasa ni muda wa kukamilisha ule mpango wetu, Dosomi mpigie Mama bonge atuletee mtu wetu ili tutimize mpango wetu!, Alafu Farhan na wewe hakikisha ile dawa inakuwa tayari, haitakiwa kukosea stepu hata moja, maana zaidi ya hapo tutaingia kwenye matatizo." Mama Samir akiwa anatabasamu aliongea.
Upande wa pili Nyumbani kwa Mama bonge, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Dosomi, ilibidi amuite Nomani kutekeleza kile alicho ambiwa.
"Noman! Mwanangu sikiliza nimeongea na Mama yako, kakili kabisa makosa yake na kaomba umsamehe Sana, na muda siyo mrefu kanipigia Simu kwamba uende ili mkajadili vizuri, ikiwezekana uweze kupewa baadhi ya Mali za Baba yako usimamie mwenyewe" hayo yalikuwa maneno matamu ambayo Nomani baada ya kuitwa aliambiwa na Mama bonge.
"Uuuuuu!! Aunt ya Kweli hayo, maana wale watu kwa roho mbaya yao wasije wakaniua!" Nomani japo kuwa alifurahia zile taarifa ila alikuwa na wasiwasi haswa.
"Nomani hiyo haiwezi kutokea, maana nao wanajua wakifanya hivyo watapata matatizo makubwa!" Mama bonge alikuwa anadanganya Nomani huku macho yake yakiwa makavu kama ndo kweli hivi.
Basi jioni ile kigiza kikiwa kinaanza Nomani aliondoka pale na kuelekea huko kwao, na alipewa na pesa ya kupanda daladala kabisa ili asichelewe.
Noman alifika pale kwao, kwanza kitu Cha kwanza, alikuta mlango wa pale getini upo wazi, alijaribu kumuita Bwana Olenashi ambaye muda mwingi alikuwa anashinda getini lakini hakuwepo kwa muda ule.
Nomani akiwa hana hata wasiwasi alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye mjengo, Nomani alifika mlangoni aligonga ule mlango kwa mashaka kidogo, maana alikumbuka kwa Mara ya mwisho kuingia mule Ndani alikuwa kakoswa koswa na risasi.
Nomani alisikia sauti ya karibu na ilikuwa sauti ya Mama Samir, basi kwa uoga Nomani alizungusha kitasa na kusukuma mlango! Kisha alizama Ndani.
"Heeee!!! Ucle Olenashi!!!" Baada ya kufika sebuleni, Nomani alishituka kuona mwili wa Olenashi upo chini huku damu zikiwa zimetapakaa chini, Nomani aliita kwa mshangao na uoga.
Ila muda ule ule akiwa kaduwa, bwana Dosomi alimvizia kwa nyuma na kumchoma sindano mgongoni.
Sindano hiyo ilikuwa ni sindano ya Aina yake, ilikuwa ni sindano ya kuvuruga akili kwa muda.
Baada ya Nomani kuchomwa ile sindano kwanza alianza kuhisi kizunguzungu, yaani alikuwa anaona vitu vyote mule Ndani vinazunguka.
"Wewe ndo uliye muua Olenashi na huyu binti!! Wewe ni muuaji Nomani!!" Akili ya Nomani ikiwa imevurugika huku kijana haelewi chochote, Mama Samir alimshikisha Nomani bastola huku akiwa anamwambia Maneno ambayo yeye alijua kwa nini anasema hivyo.
Baada ya hapo bastola ikiwa mikononi mwa Nomani, Mama Samir alimpiga risasi nyingine Olenashi huku akiwa kamshikisha ile bastola Nomani, baada ya hapo kijana Nomani alichomwa sindano nyingine.
Noman alianguka chini akiwa kashikilia ile bastola mkononi.
Mama Samir na watu wake walifanya walicho ona ni sahihi baada ya hapo waliondoka pale nyumbani huku wakiacha Milango wazi.
Masaa yalisogea, usiku mnene ulisogea huku Nomani akiwa bado hajazinduka, hatimaye palikucha mpaka asubuhi huku Nomani akiwa bado hajazinduka, muda huo Mama Samir na Farhan walionekana wakiwa hotelini.
"Farhan masaa si yanakaribia, tumpigie yule afande!!" Mama Samir alimuuliza Farhan, basi Farhan aliaangalia saa yake na kutikisa kichwa kwamba ndo muda mwafaka.
Upande wa huku Nyumbani Sasa kidogo kidogo Nomani alianza kurudisha fahamu huku akiwa anakohoa muno.
Baada ya dakika kama tano Nomani alizinduka kabisa huku kichwa kikiwa kinauma, kijana Nomani alipo angalia pembezoni mwake alikuta kuna maiti mbili, huku akiwa kashika bastola.
Kwanza Nomani alishituka huku jicho likiwa linamtoka, yaani kumbukumbu zote kichwani zilikuwa zimefutika! Alikuwa anakumbuka vitu vichache tu vilivyo tokea kwa Mara ya mwisho.
"Wewe ni muuaji Nomani, umemuua Olenashi!" Hayo ndo maneno ambayo yalikuwa yanazunguka kichwani mwa kijana Nomani, yaani alikuwa haelewi kipi ni kipi.
Akiwa anashangaa na bastola yake mkononi, Nomani alishituka kundi la watu wanazama mule Ndani, walikuwa ni askari wa kutosha.
"Mikono juu, upo chini ya ulinzi" hiyo ilikuwa ni amri kwa kijana Nomani, Nomani akiwa anageuka ili awaangalie vizuri wale Askari alipigwa risasi ya mguu, yaani alidondoka pale pale chini na kuzimia.
Yalipita masaa kama sita hivi Nomani ndo alikuja kushituka akiwa hospital, huku pingu ikiwa mkononi.
"Kijana afadhari umeamka, ebu nambie dogo ilikuwaje mpaka ukaua!?" Alikuwa ni doctor Devi kaingia mule ndani, na alimuuliza Nomani, ila Kijana Nomani ni kama akili zake zilikuwa zimehama, yaani alikuwa ni kama zezeta, alikuwa haelewi dunia inaenda vipi.
Doctor Devi alikuwa ni mtu anaye penda kufuatilia Mambo na kuchokonoa, pia alikuwa ni kijana anaye jua Mambo mengi na anaye aminika kwenye hospital kubwa kama ile.
Doctor Devi baada ya kuona Nomani hayupo Sawa, ilibidi achukue damu yake ili akapime kama kuna chochote alikula au kurishwa, maana alihisi huwenda alipewa hata madawa ya kulevyaa.
Siku hiyo ilipita, zilipita na Siku nne zingine, bado doctor Devi kipimo chake kilikuwa hakijasoma majibu, ila Siku ya nne usiku doctor Devi ndo majibu ya kipimo chake yalionekana, na aligundua kwamba kijana Nomani ndani yake kuna Sumu kali muno inayo muendesha, ila bahati mbaya hakujua ni sumu ya aina gani na tiba yake ni ipi.
Doctor Devi alijiapia kwamba lazima kesho yake aanze kufanya uchunguzi ili aweze kumtibia kijana Nomani.
Bahati mbaya Siku inayo fuata asubuhi asubuhi Nomani alikuja kuchukuliwa, kwa sababu ilikuwa ni Siku ya yeye kupandishwa mahakani, na Nomani hali yake ilionekana kuimarika kiasi kwamba angeweza kusimama mahakamani.
Ilikuwa ndani ya mahakama, ni watu wengi muno walikuwa wamejazana kuja kushuhudia muuaji aliye uwa watu wawili kwa risasi, kila mtu alipo muona Nomani pale mahakamani alibaki anashagaa kutokana na umri wa kijana yule.
Kesi ile ilianza kusikilizwa, ila Nomani kila alipo ulizwa jibu lake lilikuwa ni kwamba hajui na haelewi chochote, yaani alikuwa hana majibu kama kaua au hajaua.
Basi kesi ile Siku hiyo iliahirishwa na ilipangwa kusikilizwa baada ya wiki moja mbele.
Nomani kwakuwa alikuwa hajapona kabisa alirudishwa hospital, basi baada ya Nomani kurudishwa hospital doctor Devi ilibidi Sasa aanze kufanya uchunguzi wake kuhusu ile sumu na dawa ipi inaweza fanya kazi.
Baada ya Siku kama nne hatimaye doctor Devi aligundua dawa ambayo inaweza toa ile sumu, Siku hiyo hiyo alimuanzishia dozi kijana Nomani, na ilikuwa Dozi ya sindano ambazo zinachukua karibia wiki ili dozi ikamilike.
Doctor Devi alimchoma Nomani sindano siku tatu, akiwa kapanga kwenda kumchoma Siku ya nne alipo fika pale hospital asubuhi alikuta Nomani kachukuliwa kupelekwa mahakamani kwa Mara nyingine.
Awamu hii Nomani alionekana kuimarika vyema kiafya, hata akili yake ilikuwa imeanza kurudi taratibu baada ya kuchomwa sindano zile kwa karibia Siku tatu, yaani awamu hii Nomani kumbukumbu zilikuwa zinakuja zinapotea.
Bahati mbaya Siku hiyo mahakamani Nomani hakupewa nafasi kubwa ya kujielezea, yaani mashahidi wachache tu walisikilizwa na hakimu alitoa hukumu yake.
"Kwakuzingatia ushahidi ulio tolewa, na kuzingatia maelezo ya mtuhumiwa ni dhahiri kwamba, kijana Nomani alimuua bwana Olenashi na binti Sarah kwa makusudi kabisa, kutokana na makosa uliyo yafanya unafungwa kifungo Cha maisha gerezani" hayo yalikuwa ni maamuzi magumu ya hakimu, baada ya hapo nyundo iligongwa mezani kuashiria kesi imekwisha.
Muda huo doctor Devi ndo alikuwa anafika pale mahakamani, alikutana na stori tu kwamba dogo kapigwa kifungo cha maisha gerezani.
Doctor Devi aliwafuata Askari na kuwaomba Nomani akamalizie Dozi yake ya sindano zilizobakia, ila wale askari waligoma na kusema sheria hairuhusu, na walimtaka doctor Devi akalete hizo dozi watampatia wenyewe.
Ni kweli majira ya Jioni doctor Devi alipeleka dozi nzima na kutoa maelezo Namna ya kumpatia mgonjwa.
Baada ya hapo kijana Nomani alipelekwa gerezani, gereza hilo lilikuwa siyo mbali na pale mjini, ilikuwa ni nje kidogo ya mji.
Maisha mapya kwa Kijana Nomani yalianza huku akili yake ikiwa bado haijakaa vyema, yaani alikuwa bado haelewi kipi ni kipi, bahati nzuri kwa kijana Nomani wale Askari walio pewa ile dozi walikuwa na utu kidogo, kwa hiyo Walikuwa wanatekeleza kama walivyo elekezwa.
Baada ya Siku kama tano Nomani alimaliza ile dozi na hapo ndo kizazaa kilianza, maana kijana Nomani akili yake ilirudi kama kawaida,ila akili ilirudi tayari alikuwa ashachelewa.
Na Nomani alishangaa kuambiwa kapimiwa kifungo Cha maisha gerezani, hapo kijana Nomani aliona usinichezee, kwanza alianza kufanya vurugu mule mule gerezani.
Siku ya kwanza Nomani alitia vurugu za kutosha na aliishia kupigwa virungu na Maaskari gereza, bahati nzuri gereza hilo askari walikuwa na utu kidogo, pia waharifu wengi walio kuwa wanapelekwa hapo walikuwa ni wale wenye makosa madogo madogo, yaani lilikuwa siyo gereza la wababe! Nomani yeye alipelekwa gereza lile jepesi kutokana na kwamba alikuwa mtoto japo kuwa alikuwa kaua.
Nomani pamoja na virungu hakukoma kufanya zile vurugu na alikuwa anataka wampeleke akaongee na mkuu wa gereza lile kwa sababu yeye hana hatia, yaani Nomani kwa akili yake alikuwa anaona akifanya vile anaweza kuachiwa.
Siku hiyo Askari magereza wamlibeba mkuku mkuku kijana Nomani mpaka kwenye ofisi za mkuu wa gereza lile.
Noman aliambiwa aingie ndani, na kweli aliingia bahati mbaya mkuu wa gereza hilo alikuwa ni mtu na roho yake mbaya.
Kwanza baada ya Nomani kuingia tu alikula makofi mazito matatu, huku akiwa anamtishia Nomani kumfyatua risasi ya kichwa kwa kutumia bastola ambayo ilikuwa ipo pale mezani.
Basi Nomani kwa akili ya utoto alipo ona bastola pale mezani, akili yake ilimjia kwamba aichukue amteke au kumtishia yule mkubwa ili yeye aachiwe, yaani kiufupi Nomani alifikiria Namna kwenye TV watu wanavyo tekaga mtu ili kujilinda, aliona naye anaweza fanya vile.
Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona, na hapo ilibidi waanze kunyan'ganyana ile bastola na yule mkubwa, katika ile hali ya kunyan'ganyana Nomani alishika sehemu ambayo siyo, risasi ilifyatuka na kumpitia yule mkubwa kifuani, tena upande uliko moyo.
Hapa ndipo kizazaa na jina la hii Simulizi linaenda kujitokeza ungana nami katika sehemu ijayo
Tukutane sehemu ya 12
0 comments:
Post a Comment