Wednesday, November 29, 2023

KICHAA MPELELEZI 36 to 38


 ( 36-38)

SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 36.


Ilikuwa ni majira ya saa tisa alasiri mimi Clara tulikuwa tumeketi nje ya pango ambao tulijificha kule msituni, tulikuwa tumekaa kimahaba huku Clara akichezea chezea ndevu zangu kwa viganja vyake😀, nikiwa sina hili wala lile ghafla😳 nikashtukia tumezungukwa na mbwa wakubwa kama saba hivi, walianza kubweka kwa nguvu sana, punde wakatoka watu waliovalia mavazi ya kininja, yani mavazi ambayo yalifunika miili yao yote na kuacha sehemu ya macho tu🥷moja kwa moja nikagundua ni wenzake na Clara, wote wakaninyooshea bunduki walizokuwa wamebeba, sikuwa na shaka wala wasiwasi  maaana nilijua kwa mahaba na mapenzi motomoto ambayo nilikuwa nikipa Clara atanitetea lakini ghafla nikashangaa Clara anacheka😂 na waambia wale watu wake "Mfungeni mikono tuondoe naye " alisema Clara. "😣 Clara yani kabisa umedhamiria kunigeuka🥺" Nilimuuliza. "Sijakugeuka ila mwanzo nilikuvumilia tu kwasababu tulikuwa wawili msituni isitoshe mguu wangu mmoja ni mbovu hivyo singeweza kuleta pingamizi lolote juu yako zaidi ya kukubali chochote ambacho ungekita, lakini sasa nimepata tena nguvu baada ya kuwaona watu wangu😜" Alisema Clara hapo nikayakumbuka maneno ya babu aliyonihusia kuhusu wanawake, babu aliniambia kwamba "Silaha kubwa ya mwanamke anayoitumia kumpiga nayo mwanaume ni mapenzi, yani daima usijaribu kumrudia mwanamke ambaye mliachana naye katika mazingira ya shari, mazingira ya kutendeana mabaya kamwe usimrudie na kuanzisha naye mapenzi kwani hujui amerudi akiwa na dhamira ipi, pengine anataka kutumia mapenzi kama silaha ya kukuadhibu ama kulipiza kisasi kwa yale uliyomtendea" Niliyakumbuka🤔maneno hayo ya babu na kujilaumu sana kwamba kwanini nilijisahau na kurudiana na Clara, basi watu walinifunga minyororo migumu sana mikono kisha wakaninyanyua kwa vibongo na kuanza kuniongoza njia, huku wengine wakimbeba Clara kwani bado alikuwa hajaweza kutembea vizuri. Niliongozwa njia ghafla huku nikichapwa viboko kama ng`ombe anayeswagwa kwenda machinjioni.


Basi hatimaye tukatumia masaa 12 tukafanikiwa kutoka mule msituni, tulifika barabara walipopaki magari 🚗yako nikaingiwa ndani ya gari na bila kupoteza muda tukaondoka eneo lile, safari yetu ilikuwa ndefu sana hatimaye tukafika kwenye jengo moja kubwa sana lenye uzio mrefu kwenda juu kama ule wa yeriko, nikaingizwa ndani kumbe jengo lile ilikuwa ndio kambi ya majambazi wa Clara, maana tulipoingia ndani walipomuona tu Clara walishngilia mithili ya watu wanaoshangilia kuuona mwaka mpya🥺, ndani ya jengo lile walikuwepo majambazi wengi sana wasio na idadi kama utitiri, walikuwa wamezagaa ndani ya jengo lile huku wengine walikuwa wanavuta bangi, wengine waikuwa wanafanya mazoezi ya kuimarisha miili yao kwa kunyanyua vyuma🏋🏿‍♀️ kuruka sarakasi🤸‍♂️na wengine walikuwa wanacheza kamari huku wakinywa pombe kali🏏 lakini walipomuona Clara kabebwa juu juu wote walikusanyika sehemu moja huku nyuso zao zikionekana kuhuzunika😌 Clara aliletewa kiti na kuketishwa mbele yao. "Ni matumaini yangu kwamba hamjambo vipenzi vyangu, ee kama mjuavyo katika hii kazi yetu hapakosi changamoto, lakini safari hiii nilipoingia kazini nimepitia changamoto kubwa sana, wanajeshi wa kambi ya marekani wameniandama sana mpaka wakaniwekea na mpelelezi ambaye alijifanya kichaa ili aweze kuninasa, lakini nilifanikiwa kumdhibiti nikajua kwamba nimemuua akaja tena kwa njia nyingine ya kufanya sajari yani kubadilisha sura huku akishirikiana na mtu ambaye nilimwamini na kumuona kama mpenzi wangu kumbe anashirikiana na maadui zetu watuangamize, mtu mwenyewe ni huyu hapa tumekuja naye" alisema Clara watu wote wakanigeukia na kunitazama kwa macho makali😳 mpaka utumbo ukawa unacheza cheza😨 kutokana na jinsi walivyokuwa wananiangalia kikatili, Clara akaendelea kuongea " Si hayo tu huyuhuyu mtanzania ndiye kasababisha pesa zangu benki zimechukuliwa na ndiye kasabavisha goti langu limevunjika hivyo siwezi kupigana tena hata na mtoto wa miaka kumi" alisema Clara kwa kunishtakia kwa watu wake huku machozi yakimtoka😭 baadhi ya watu wake ambao walikuwa ni mabaunsa waliuma meno kwa hasira😬 baada ya Clara kuwaambia maneno hayo.


Basi Kapteni waoo akatoka mbele kuongea "Jamani huyu mchumba kajichanganya yani hapa ameyakanyaga☹️ tuliahidiana kwamba kiumbe yeyote atayejaribu kuingilia kwenye kazi yetu ili aturudishe nyuma au atuangamize adhabu ya kwanza kabla ya nyingine tutamgeuza mke wetu" alisema yule kapteni wa majambazi, nikashtuka sana😨kusikia hivyo huku nikitetemeka mpaka meno, akaendelea kuongea " Adhabu ya pili huyu mchumba atapitia makali kaba ya kwake kwa kutobolewa macho na chuma cha moto 🔥 chenye ncha kali na mwisho atanyongwa mbele ya halaiki yote," alisema yule kapteni wa majambazi na watu wote walishangilia sana huku wakipiga vifijo na nderemo. "Kwanza tumtoeni wenge kidogo" Kapteni wa jeshi alisema na bila kuchelewa jopo la watu wake likanivamia na kuanza kunishushia kipondo cha mbwa mwizi, sikuchukua hata dakika mbili nilipoteza fahamu, basi nilipozinduka nikapelekwa kwenye chumba cha mateso ambacho kilipewa jina la black room, ndani ya chumba hicho niliwakuta wanaume watatu wenye miili mikubwa kama tembo na iliyojazia kimazoezi, kazi ya wanaume hao ilikuwa ni kutoa mateso  kwa maadui watakaofikishwa kambini hapo, basi nikafungiwa nao ndani ya chumba kile, mmoja akasema "Mchumba vua nguo tukupe mimba " rohoni nikasema hapa bora nife kishujaa kuliko kulawitia, nikaruka mateke ya kuwashukiza, mmoja nilimpiga teke la macho,vumbi lote la viatu likaishia machoni kwake akadondoka chini huku akiyafikicha macho yake, na mwingie nilimpiga teke la pua akababiza ukutani na kupoteza fahamu, yule wa tatu nikamrukia mateke ya dabodabo moja likatua kifuani na lingine likamaliza kwenye paji la uso, akadondoka chini, nikamrukia juu yake na kumpiga ile minyororo niliyofungwa nayo mikonononi kichwani mwake mpaka akazimia, nikasogea sehemu ambapo walitumia kuwafungulia watuhumiwa minyororo baada ya kuhakikisha wamewalegeza kila kitu, hapo nikang`ang`ana kufungua mpaka minyororo ikafunguka, haraka nikachukua bunduki kubwa iliyokuwa ndani ya chumba kile na kuwamininia risasi zakichwani wote, kisha nikawavua mavazi yao kabla hayajaingia damu, nikayavaa mimi mavazi yale ya kininja tena kwa kuyasunda😁 yote matatu ili nionekane bonge kama walivyo wao, hapo nikajaza risasi zilizokuwa mule ndani mmifukoni mwangu huku mikononi nikiwa nimeshikilia mtutu basi, "kama nitakufa basi lakini n itahakiisha Clara anarudi marekani, acha nikapambane na huo utitiri wa majambazi nje" nikajisemea kimoyomoyo kisha nika😳......... 


Meza mate kwanza😂 usije ukaloanisha simu kwa udenda unaokutoka kama mtu aliyeona embe bichi. Just a joke 😂 narudi


SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI😳😭 37&38


Baada ya kufanikisha kuwaua wale manyemera kwenye chumba cha mateso kilichopewa jina la black room, niliwavua mavazi yako ya kininja🥷na kuyavaa mimi, tena niliyavaa mavazi ya wote watatu😁 ili nionekane bonge kama walivyo wao, baara ya kuvaa kila kitu na kuwa sawa nikajaza risasi nyijngi kwenye yale mavazi ambayo yalikuwa na mifuko kila kona kama sare za polisi kisha nikatoka nje huku nikiwa nimeshikilia mtutu wa bunduki, ile natoka tu nje nilianza kuwamiminia risasi za kutosha💥  wate niliwapukutisha akabaki Clara na walinzi wake watatu ambao aliwaamini, ile nataka kufyatua risasi ili niwamalizie walinzi wa Clara niondoke na Clara ajabu nikashangaa😨 risasi hazitoki, nilikuwa tayari nimekwishaishiwa na risasi nilizozikomba ndani ya chumba cha mateso, kwa bahati nzuri wao hawakuwa na bunduki, mikononi mwao walibeba majamvia yani mapanga maalumu kwa ajili ya kupigania, mmmoja akanikimbilia🏃🏿‍♂️ niliposimama huku akiwa ameushikilia upanga wake, ile anataka anifyeke shingo niliiinama 😀 haraka nikaudaka ule mkono wake ulioshikilia upanga bila kumremba nilimshindilia ngumi ya uso na pasina hiyari yake aliuachia mwenyewe upanga maana ngumi ya pua niliyomshindilia ilimpa mawenge mawenge na kumtupa chini🤧 huku damu zikimtoka puani, walinzi wawili wa Clara waliobakia walipoona vile kwa pamoja wakaanza kuja kwa kukimbia na mapanga yao mkononi🤺 ili wanikabili, ile wanataka tu kunikaribia haraka nikainama na kuzoa mchanga mwingi wa vumbi kwa mikono tangu nikawamwagia machoni😵 walitupa mapanga chini na kuanza kubabaika huku wakifikicha macho, hapo ikawa rahisi kwangu mimi kuwapiga ngumi👊 kama ngoma za mchiriku, hakuna aliyeweza kusimama ndani ya lile jengo nzima, Clara kuona vile, haraka akachukua sindano📌 ili ajimalize mwenyewe, na sijui ile sindano aliitoa wapi, nahisi aliiandaa kwa ajili yangu kwamba nitakapopewa mateso vya kutosha animalizie kunidunga sindano ile yenye sumu kali zaidi za sumu ya mamba ili nife kabisa😁 moyoni nikasema siku zote mcheza na tope humrukia Clara hana tofauti na mcheza na tope ama mchimba kisima ambaye mwisho wa siku huingia mwenyewe kwani dhamira yake ilikuwa ni kuniangamiza sasa anajiangamiza mwenyewe.


Wakati anataka kujidunga sindano ile ili afilie mbali haraka nilikimbia na kumuwahi kwasababu nilijua akijidunga sindano ile nitakuwa nimekosa malundo  niliyoahidiwa na wamarekani na nitakuwa nimevunja miiko ya kabila langu la kichaga yani kuzingatia maokoto😁 ile namkaribia, laaaaaa haulaaaa😳 tayari alishajidunga sindano mkoni, haraka nikachana ile lastiki ya kininja niliyokuwa nimejifunika nayo usoni kisha nikamfunga nayo mkononi kwa nguvu sana kusudi sumu isiendelee kusambaa maeneo mengine hatari ya mwili kama vile kichwani na kwenye moyo, kwa ushapu wa hali ya juu nikambeba na kumuweka ndani ya gari lililokuwepo pale na kwa bahati nzuri gari lenyewe lilikuwa sailensa, nikaliwasha na kutoka nje ya geti lile na kukimbilia hospitali za mexco, nilienda kwa kuulizia ulizia kutokana na ugeni wangu, hatimaye nikafanikiwa kumfikisha Clara hosmatairi  madaktari pamoja na manesi🧑🏻‍🍳walisaidiana na mimi kumtoa Clara kwenye gari kisha wakamuweka juu ya kitanda cha matairi mbio mbio walimkimbiza kwenye chumba cha huduma ya dharura baada ya kuwaeleza kwamba alijidunga sindano ya sumu,  basi mimi nikabaki nje sehemu ya mapokezi nikiwaachia madaktari wafanye kazi yao, yalipita masaa kama mawili hivi nikamuona daktari akitoka kwenye mlango wa chumba cha huduma ya dharura, haraka nikamkimbilia na kumuuliza "Samahani daktari mgonjwa anaendeleaje?" Nilimuuliza "eee kwa sasa anaendelea vizuri tumefanikiwa  kuokoa maisha ya mama na pia kichanga kilichopo tumboni kwake alisema daktari, kidogo nikapigwa na butwaa kwa mshangao😳 baada ya daktari kunieleza kwamba Clara ana mimba tena ya mwezi mmoja na nusu. " Huenda ikawa kweli ana mimba maana hizi wiki chache zilizopita amekuwa ni mtu wa visirani sana lakini je 🤔 mimba ni yangu au ni ya Mr. Michael maana ametembea na sisi kwa kipindi chote hiki cha mwezi mmoja na nusu" Nilijiuliza lakini akilini nikajiambia kwamba itajulikana tu nikimfikisha marekani, basi madaktari walimhudumia na kuniambia itabidi nimuache Clara pale hospital wamlaze aendelee kujiskilizia kwani amelegea sana mwili kiasi kwamba hawezi hata kuongea" waliniambia madaktari nikawatukana kimoyomoyo 😁 "Nyie wagonjwa nini yani mnataka nimuache afie hapa ili nikose maokoto yangu, hapa ni heri akafie kwenye ardhi ya kambi la jeshi la marekani kidogo nitaonekana ni shujaa" Niliwaza, kisha nikawaambia. " Kama ni kujisikilizia hali yake ataenda kujisikilizia nyumbani na kama atazidiwa basi nitamrudisha " Niliwaambia madaktari, wakaniruhusu niondoke naye licha ya kwamba alikuwa amelegea kama mlenda wa bamia na nyanya chungu hali kadhalika sauti yake ilikuwa haitoki lakiini niliondoka naye bila kumuonea huruma kwamba aendelee kutibiwa mpaka apone.


Nilitoka pale hospitali na gari nililombeba nalo Clara wakati wa kumpeleka hospitali, moja kwa moja nikaenda naye mpaka kwenye station ya treni za umeme zinazotoka mexco kwenda marekani, nikiwa pale station nikatoa kikaratasi kwenye boxer yangu na kutoa namba za Michael, kwasababu simu yangu ilivunjwa vunjwa siku ile niliyochezea kiligo cha mbwa mwizi kutoka kwa majambazi wenzie na Clara, na kikaratasi kile cheye namba ya ya Mr. Michael nilikihifadhi kama akiba kwani uwapo vitani kupoteza simu sio jambo la kuulizia,. Basi nikaomba simu pale station na kumpigia Michael, nikamueleza kwamba nipo station ya treni na Clara nimefanikiwa kuwaua wenzake wote na sasa nataka nimlete mareani ila nauli ndio sina " Sawa kamanda mimi nakuja hapo hapo station baada ya masaa mawili kamanda" alisema Michael, tukakaa pale station kumsubiri Michael afike, kweli ndani ya masaa mawili Michael alifika lakini baada ya kumueleza kwamba Clara ana mimba ya mwezi mmoja na nusu na sikumueleza kwamba nahisi ni yangu ama ni yake, kitu cha ajabu 😳 na cha kushangaza Michael aka.............


Jamani acheni ninywe kwaza chai maana kuna wanaume wanapenda watoto hata wa kusingiziwa 😂 Nyie nyie acheni tu, unahisi kipi cha ajabu Michael alikifanya mbele ya Brighton?

Share:

0 comments:

Post a Comment

List

Contact

Featured

YATIMA GEREZANI 12

  YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA 😭😭 Mtunzi: Mwaki Ze Done Sehemu ya 12. Nomani akiwa anachukua ile bastola bahati mbaya yule mkubwa alimuona,...

Sample Text