YATIMA NA GEREZA LA KUTISHA ππ
Sehemu ya 6.
Nomani akiwa anazidi kushangaa alishuhudia yule pakaa anakata moto na kufa pale pale, mpaka hapo Nomani hakuelewa imekuwaje paka yule afe kwa taabu vile Mara tu baada ya kula kile chakula.
"Heeeee!! Nini hiki jamani!!" Nomani alizidi kushangaa, akiwa kule jikoni alipo piga macho juu ya kabati la pale jikoni, aliona kuna pakiti fulani nyeusi ikiwa imechanwa kidogo, Nomani aliisogelea ile pakiti na kuisoma, Nomani japo kuwa alikuwa kasoma kidato Cha kwanza tena muhura mmoja tu lakini maneno ya kingereza ambayo yalikuwa yameandikwa kwenye ile karatasi alielewa vyema.
"Heeeee!! Sumu!?? Au kile chakula kina sumu!?" Nomani alishituka na kuinusa ile karatasi, aligundua kweli ni sumu na ilikuwa inaonekana tayari imetumika.
Nomani akiwa kachanganyikiwa alikimbilia sebuleni kuangalia kile chakula, alijaribu kukinusa vizuri, aligundua ni kweli kile chakula kina sumu, na tayari Nomani alikuwa kala kijiko kimoja.
Nomani alijikuta ameanza kujizamisha vidole kwenye koo lake ili atapike kile chakula alicho kula,ila wala hakufanikiwa, na tayari Nomani alikuwa kaanza kusikia maumivu ya tumbo.
"Heeeee Mungu wangu inaamana ndo nakufa hivi hivi!!" Nomani jicho likiwa linamtoka alijisemea kimoyo moyo, ila akiwa yupo pale alishituka kuna watu wanakuja huku wakiwa wanaongea, na Nomani aliitambua sauti kwamba ni sauti ya Baba victor.
Nomani tayari alikuwa kashaanza kuona rangi harisi ya Baba victor mpaka hatua ile.
Nomani kitu alicho kifanya, kile chakula alikimwagia kwenye shati lake, na kwenda kujificha chooni, huku akiwa anahema muno.
Nomani akiwa kule chooni kabana alisikia sebuleni watu wanapiga makofi!!.
"Aisee safi kabisa! Yule kijana kala chakula chote, Dosomi wewe subiri majibu mazuri!!"
"Aisee una uhakika lakini kwamba uliweka sumu kwenye chakula!?"
"Dosomi niamini Mimi Sumu niliweka tena yote!"
"Heeeee Sasa huyo Nomani atakuwa kaenda wapi!?"
"Usijali atakuwa kaondoka kwenda kuomba msaada baada ya kuona tumbo linauma, na itakuwa ni Bora akifia huko njiani kuliko humu Ndani" .
Hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya Baba victor na yule mwanamke, na Nomani aliyasikia vyema hayo mazungumzo akiwa kajificha chooni, huku akiwa na chakula chake chenye Sumu kwenye shati lake.
"Aisee sikiliza! Mimi naondoka ila hakikisha unawasiliana na kina Damian waambie wahakikishe wanagundua mwili wa Nomani ulipo, yaani wahakikishe kasha fariki na kama bado basi wafanye juu chini wamalizane naye, maana nimechoka kila Siku lawama kutoka kwa Farhan na Zena, na nyie mnajua pesa zao tushakula!" Baba victor akiwa anaondoka mule Ndani alimwachia Mama yule maelekezo, na kila kitu Nomani akiwa kule chooni alikisikia vyema.
Hakika Siku hiyo Nomani alianza kuamini kwamba kila binadamu basi ni mbaya, yaani alikuwa hamuamini Mtu.
Nomani alikaa kule chooni huku tumbo likiwa linakata haswa, na bahati nzuri kwa Nomani ni kijiko kimoja tu alikuwa kala, ila kutokana na ukali wa Sumu hata kile kijiko kimoja kilikuwa kinamfanya Nomani aone kama dunia inazunguka.
Kijana Nomani baada ya kuona atafia mule chooni, bila hata kujali alitoka mule chumbani yaani alikuwa yupo tayari kwa lolote, maana alitoka akiwa hajali kama yule Mama yupo pale sebuleni au hayupo.
Bahati nzuri Nomani akiwa anatoka yule Mama alikuwa yupo chumbani kwake anawasiliana na watu wake anao wajua.
Nomani alifanikiwa kutoka mpaka nje kabisa, baada ya hapo hali yake ikiwa inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta msaada Sasa.
"Brother naomba nisaidie!! Nimekula chakula chenye Sumu nakufa mie!" Nomani katika tembea tembea yake basi alikutana na jamaa mmoja akiwa kapaki bodaboda yake kusubiri wateja.
"Dogo acha uhuni, au ndo nyie mumeanzisha mchezo wa kupora pikipiki hapa mjini, maana plani zenu ni hizo hizo!" Basi yule bodaboda baada ya kuona Nomani anamletea giza, aliongea kwa kufoka.
Ila Nomani pale pale damu zilianza kumtoka puani, huku macho yake yakianza kuwa mekundu.
"Heeeee!!! Dogo vipi kuna nini!??" Yule bodaboda baada ya kuona hali hiyo, hapo aligundua kwamba huwenda ni kweli Nomani kala Sumu.
Yule bodaboda alicho fanya alimshitua mwenzake mmoja, basi haraka haraka walimkimbiza Nomani hospital.
Bahati nzuri kuliko zote walipo fika pale hospital, Siku hiyo ilikuwa dhamu ya doctor Devi, kwa hiyo yeye ndo aliye mpokea na kuanza kumshugurikia.
Kutokana na kwamba Devi alikuwa tayari anamjua yule kijana na anayajua na mazingira yake alipambana kiukweli kweli kuokoa maisha ya Nomani.
Jitihada za doctor Devi zilifanya kazi maana baada ya Siku mbili Nomani alizinduka huku hali yake ikiwa inaendelea vyema.
"Dogo mbona unajitafutia matatizo wewe, kwanza Siku ile kwa nini ulitoroka pale kwangu kabla hujapona!?" Basi baada ya Nomani kuwa vizuri kidogo, doctor Devi alianza kumuuliza maswali.
"Daaaa!! Brother samahani, Mimi niliondoka kwa ajili ya kwenda kutafuta msaada zaidi, maana niliona kama nakupa mzigo hivi!"
"Duuuuu dogo bora ungeaga ujue, maana Mimi nilipata hofu kweli kweli, eheee vipi Awamu hii imekuwaje umekula Sumu kali kiasi hicho!?"
"Daaaa ni bahati mbaya tu, nilikula chakula ambacho walikuwa wametegea panya pasina Mimi kujua!" Nomani alikuwa anadanganya, yaani Nomani alijikuta tu hataki kumuamini mtu yeyote, yaani akili ya Nomani alikuwa anaamini Kwamba kama Mama yake kaweza kumsaliti je watu baki itakuwaje.
Basi Siku hiyo ilipita huku Nomani akiwa anazidi kupewa matibabu Zaid.
Siku nyingine ilipo fika yakiwa ni majira ya saa tatu usiku, Nomani alipo jigundua yupo sawa aliamua na kutoroka pale hospital bila hata kumwambia doctor Devi, yaani alikimbia hakutaka mazoea na mtu tena.
Nomani akiwa na hasira safari yake ilienda kumpeleka mpaka kwao, na Lengo lake ilikuwa ni kwenda kumchana Mama yake makavu na kumuuliza kwamba kwa nini anataka kumuua.
Nomani baada ya kufika getini alizuiliwa na mlinzi.
"Olenashi naomba niache nipite, leo nataka Mama akaniambie kwa mdomo wake Kwamba Mimi siye mwanae na nataka nikajue sababu za yeye kutaka kuniua!" Nomani alikuwa kachafukwa baada ya kukoswa koswa kufa Mara mbili.
"Nomani Mimi siwezi kukuruhusu wewe kuingia huko ndani kwa sababu najua unaenda kufa, kwa taarifa yako Mama yako alipewa taarifa kwamba wewe tayari umekufa, na muda huu naongea na wewe Bwana Dosomi na vijana wake wapo huko ndani, Sasa wewe nenda kama hujaenda kufia huko huko!" Olenashi alikuwa hataki kabisa Nomani aingie mule ndani kwa sababu alikuwa anajua uhatari wa kuingia kule ndani.
"Uncle olenashi aisee naomba niruhusu hapa ni Nyumbani na hizi ni Mali za Baba Yangu!" Nomani alizidi kuwa king'ang'anizi.
"Nomani wewe ubishi wako naona ni kama Baba yako, ujue Boss Fekon kama siyo ubishi wake huwenda hata asingekufa, wala asingemuoa huyo mwanamke, ila ubishi ndo chanzo Cha yote, naona sasa na wewe unafuata nyayo za Baba yako!" Olenashi aliongea maneno mazito ambayo yalifanya Nomani amkazie macho.
"Nomani kwa hiyo wewe ulikuwa unajua kama Baba yangu atakufa!? Nakuuliza kwa hiyo wewe ulikuwa unajua!?"Nomani aliuliza kwa jaziba.
"Nilikuwa sijui kama atakufa ila nilikuwa najua watu wanao mzunguka siyo watu wema, ila kila nilipo jaribu kumgusia alikuwa mkali na kuwa mbishi kama wewe ulivyo!"
"Uncle olenashi mbona kama unanificha Jambo ebu naomba niambie kila kitu kuhusu familia Yangu kama unajua chochote!?" Nomani ilibidi Sasa apunguze jaziba na kuanza kujitirisha Huruma.
"Nomani haya ntakayo kwambia naomba uniahidi kwamba itakuwa Siri yako na utayaweka kifuani, maana Mimi nishaamua kujiwekea Siri ili niwe salama, na naomba hata wewe ubakie kuyajua tu!!" Olenashi alionesha ana mambo mazito kayabeba ila ndo hivyo alikuwa anaogopa.
"Uncle we nambie Mimi sitamwambia Mtu!" Nomani alikubali ikiwa hajui ni Siri zipi!.
Basi wawili wale ilibidi waingie kwenye kibanda Cha mlinzi kwa ajili ya mazungumzo ya usalama zaidi.
"Nomani Mimi, Mama yako nilikuwa namjua vyema kabisa kwa sababu nilikuwa nimesoma naye shule ya Msingi huko kijijini.
Baada ya Mama yako kufiwa na mjomba yake ambaye alikuwa anamlea, basi Mama yako aliamua kuja mjini kutafuta maisha.
Baada ya kupita miaka kadhaa ya Mama yako kufanya biashara ndogo ndogo mjini, alibahatika kukutana na Baba yako na walianzisha mahusiano huku wote wakiwa wafanya biashara wadogo wadogo.
Kwa mjibu wa maelezo ya Mama yako aliyo nipatia ni kwamba Baba yako alikuwa kaachiwa mashamba na mifugo kijijini kwao, basi Baba yako alienda kuuza mashamba yote na mifugo yote na kitu hicho kilifanya ndugu wa Baba yako kumtenga Baba yako kwenye ukoo kwa sababu aliuuza Mali za urithi alizo achiwa na wazazi wake bila kuwapa taarifa ndugu zake wengine.
Baada ya Baba yako kupata Pesa walianza biashara za kuuza Simu na Mama yako, na hapo ndipo safari ya utajiri ilianzia mpaka Baba yako kuja kumiliki viwanda na makampuni.
Kipindi chote hicho Baba yako na Mama yako walikuwa hawajaowana kwa Hiyo baada ya kuwa na maisha mazuri na kujenga nyumba ambayo ndo ile anayo ishi Baba yake na Victor saizi, waliamua kuoana rasmi kwa ndoa.
Baada ya wawili hao kuoana Mama yako ndipo alipo rudi kijijini kutafuta mfanyakazi, ila bahati nzuri alikosa mfanyakazi wa kike na aliamua kunichukua Mimi ili nije nifanye kazi kwake.
Kwa Mara ya kwanza nililetwa mjini na Mama yako na nilianza kuishi na wazazi wako nikiwa kama mfanyakazi wa ndani, na tulikuwa tunaishi kwenye ile nyumba kabla ya hii kujengwa.
Dosomi alikuwa ni mfanyakazi wa karibu wa Baba yako, na pia Zena ambaye ndo Mama Samir alikuwa pika pakua na Mama yako yaani walikuwa kama Pete na kidole.
Maisha yalikuwa matamu haswa mwanzo kwa wazazi wako na pia kwa Mimi mwenyewe, maana nilikuwa naishi kama mwanafamilia, ila baada ya muda kupita niligundua Dosomi na Zena wanajuana na kuna mpango wapo nao japo sikujua ni mpango gani.
Dosomi Mara nyingi kazi ambazo alikuwa anapewa na Baba yako zilikuwa ni zile kazi za kutumia nguvu, labda kuna watu wanasumbua kwenye biashara, au kuna biashara za magendo anataka afanye ndo alikuwa anapenda kumtumia Dosomi.
Basi baada ya kama mwaka kukatika Mama yako alipata ujauzito, na ndo hicho kipindi huu mjengo ulikamilika, kwa hiyo tulihamia rasmi huku na pale tulipo kuwa tunaishi, Baba yako alimwambia Dosomi akae, na baada ya kuhamia huku Mimi sasa kazi Yangu ilitakiwa kukaa getini, na Mama yako alisema atatafuta mfanyakazi mwingne.
Kutokana na urafiki wa Zena na Mama yako, Mara nyingi Zena alijikuta anashinda hapa na muda mwingi alikuwa analala hapa, na alikuwa anamsaidia Mama yako kazi ndogo ndogo.
Kutokana na hali ya Mama yako ya ujauzito, Zena mwishoe alianza kuishi hapa, ila wakati anaishi hapa ndo kipindi niligundua yupo kwenye mahusiano na Farhan, maana Mara nyingi tu Zena alikuwa anatoka usiku kwenda kuonana na huyo jamaa.
Maisha yalizidi kusogea hatimaye miezi Tisa ya ujauzito wa Mama yako ilifika na hapo ndipo hiii Siri ninayo kwambia leo inaanzia, ilikuwa ni jumapili Siku hiyo Baba yako alikuwa yupo mikoani kusambaza mbolea, ikiwa ni mida ya saa moja za Jioni Mama yako alipatwa na uchungu.
Chanzo Cha Siri zote kilianzia hapa! Je ilikuwaje>
/p>
Tukutane sehemu ya 7
Chanzo cha siriπ₯² naigojea Kwa hamu na ngamu
ReplyDeleteAaah π₯π₯π₯π₯
ReplyDelete